Menu
in , ,

STARS YAWASILI SALAMA

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasii salama leo alfajiri ikitokea nchini Afrika Kusini ilipokua ikishiriki michuano ya Kombe la Cosafa, baada ya kutolewa katika hatu ya awali ya makundi.

Stars ambayo jana jioni ilipoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Lesotho baada ya kufungwa bao 1 – 0, imerejea baadaa ya kupoteza michezo yote mitatu ya kundi B, baada ya kufungwa na Swaziland, Madagascar na Lesotho.

Mara baada ya mchezo wa jana dhidi ya Lesotho, kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij alisema amesikitishwa na matokeo ya timu yake katika hatua hiyo ya awali baada ya kupoteza michezo yote mitatu.

Nooij alisema, mpira wa miguu umebadilika kwani matarajio yake yamekua tofauti, kwani kiwango walivyoonyesha wapinzani wake katika kundi B vimemstajaabisha.

“Mpira wa sasa hautazami nani yupo juu katika renki za FIFA, tulikua na matarajio ya kufanya vizuri katika michuano hii lakini baada ya dakika ya 90 za kila mchezo matokeo hayakua mazuri kwetu” alisema Nooij”

Kuhusu kufuzu kwa AFCON 2017, Nooij amesema katika kikosi chake alichokwenda nacho Cosafa alikua na wachezaji saba aliowapandisha, anaamini wamepata uzoefu, na sasa atawajumuisha na wachezaji ambao hawakuweza kushiriki michuano hiyo kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.

Taifa Stars inatarajia kucheza kucheza mchezo wake wa kwanza wa kuwania kufuzu kwa AFCON 2017 dhidi ya Misri, tarehe 14 Juni 2015 katika uwanja wa Borg el Arab jijini Alexandria.

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Exit mobile version