Menu
in , ,

SIWEZI KUVAA JEZI YA SIMBA-MAYELE

Tanzania Sports

Jana kwenye mechi ya Yanga SC na KMC FC iliyochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi kulikuwepo na ugeni kutoka Congo ambapo mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Fiston Mayele alikuwa moja ya watu walioitazama ile mechi.

Baada ya mechi, Fiston Mayele ambaye aliwahi kuwa mfungaji bora wa ligi kuu Tanzania bara msimu wa mwaka 2002/20023 alipata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari ambapo pia Tanzania Sports ilikuwepo kwenye mazungumzo hayo ya Fiston Mayele na waandishi wa habari.

Fiston Mayele alipoulizwa kuhusu mechi ya Yanga SC na KMC FC alidai kuwa mechi ilikuwa nzuri ambapo KMC FC walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzuia vyema na kipindi cha pili walikuwa wanafanya mashambuliaji ya kushtukiza kwa kupambania spaces na kina Khalid Aucho.

Alipoulizwa pia kama amekuwa akifuatilia ligi ya Tanzania amedai kuwa amekuwa akiifuatilia na ligi inazidi kupanda na watu wengi kutoka nje wanaifuatilia. Fiston Mayele amedai kuwa kuna watu wanafuatilia pia wachezaji kwa ajili ya kuwasajili kutoka katika ligi ya Tanzania.

Alipoulizwa anaitazama vipi klabu yake ya zamani ya Yanga SC katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Fiston Mayele amedai kuwa kama wakiendelea kucheza hivo wanavyocheza watafika mbali sana kwenye michuano hiyo mikubwa ngazi ya vilabu barani Afrika.

Alipoulizwa kuhusu kuwa na matatizo na Yanga SC, Fiston Mayele alidai kuwa hana matatizo binafsi na Yanga SC na kama angekuwa na matatizo na Yanga SC asingekuja kuangalia mechi yao dhidi ya KMC FC.

Alipoulizwa kuhusu kurudi kuchezea Yanga SC siku moja alisema “Inshallah”. Na kuhusu kufanya mahojiano na Simba TV wakati yupo Misri mpaka akapewa jezi ya timu ya Simba SC, Fiston Mayele alionekana kushangazwa na taarifa za kupewa jezi.

Fiston Mayele alisema hakuchukua jezi ya Simba SC na kuhusu maneno ya viongozi wa Simba SC kudai wanataka kumsajili alidai kuwa hayo ni maneno tu lakini Yanga SC kwake yeye ni nyumbani.

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya martinkiyumbi@gmail.com

Leave a Reply

Exit mobile version