Zimebaki alama kumi na moja Simba SC kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa msimu huu, hii itakuwa mara tatu mfululizo wakilipa ile iliyofanywa na Yanga misimu mitatu nyuma.
Leo mipango ya kocha wa Simba Sven ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana hasa amewaza vyema kuweka wakata umeme Fraga pamoja na Said Ndemla.
Tusalie kwa Ndemla ambaye hakupata nafasi ndani ya timu ya Simba kwa muda mrefu.
Nyota huyo ameweza kutengeneza sababu ya kupatikana magoli mawili ya Simba huku akiwa na mchezo bora kabisa katika msimu huu.
Maswali ambayo atakuwa anauliza kwa shabiki zake juu ya mchezo mzuri aliouonesha dhidi ya Mwadui FC, jamani kuna mtu ana swali juu ya Ndemla?
Aliweza kuhaha kila sehemu ya uwanja kuhakikisha mipira yote inapitia kwake, huenda apewe nafasi nyingine tena ili aweze kuthibitisha ubora wake, ila kwa tunayemfahamu amecheza vizuri sana na ana kipaji cha hali ya juu.
Au tumshauri, ahaa!! Ndemla ukiona hapaeleweki basi taufta njia ya kutokea, lakini umeshasaini mkataba wa wa miaka miwili.
Luis Miquissone inawezekana ikawa njia ya kupita pale mitaa ya Msimbazi Kariakoo kuelekea katika soka la Ulaya kama umri wake ukiwa sahihi.
Wakiwa na mabeki watatu wa kati ambao ni Pascal Wawa, Erasto Nyoni na Kennedy Juma ilikuwa rahisi kwa Kapombe na Tshabalala kupanda na kushuka katika staili ya kisasa ambayo huitwa kama ‘Wing Backs’.
Anafanya vizuri sana na amecheza uzuri katika mchezo huo huenda kwangu akawa mchezaji bora namba mbili wa mchezo baada ya Said Ndemla.
Mwadui FC imecheza vizuri pia imepata 49% kwa 51% za Simba, ni tofauti ndogo sana inaonesha namna gani timu hiyo imefanya vizuri.
Imekosa watu wa kuweka chachandu pale mbele kuweza kufunga magoli.
Simba SC sasa imebakisha alama 11 kuweza kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara.
Hii ina maana kubwa sana kwa timu ya Simba na wachezaji wake.
Ibrahimu Ajibu atakuwa ametoa gundu kwani mara zote huwa akihama timu aliyohama inachukua ubingwa.
Wakati anatoka Simba anahamia Yanga timu yake ya zamani ilichukua ubingwa amerejea nyumbani ndio watu wanataka waangalie je atafeli.
Ila inavyoonekana ana nyanyua kwapa msimu huu kwani kilichobaki ni kidogo sana.
Huenda timu hiyo ikakosa zile alama 100 walizozitaka kutoka kwa msemaji wao ila wataweza kusogea hadi kufika 85 na kuendelea.
Mechi hii imekuwa tamu sana hasa ile ‘Performance’ ya timu zote mbili na huenda tukawa hatuna cha kuongea baada ya mechi ya kwanza na hizi zilizofuata.
Kilichovutia zaidi Mwadui FC nao hawakuiogopa Simba walifunguka na kuonesha soka safi kabisa.
Huku Sven akifanya mabadiliko makubwa ndani ya timu hiyo, akiweka Ndemla ndani, Fraga na Kenedy ikiwa ni hatua nyingine ya kuangalia kikosi chake katika kuelekea michuano ya kimataifa.
Swali pekee ambalo naweza kumuuliza Sven anijibu alikuwa wapi kumpa nafasi Said Ndemla?
Alikuwa wapi kuweza kubadilisha wachezaji kila baada ya mechi kadhaa akiona wamechoka ili kuwapa nafasi ya kufanya vizuri zaidi?
Hapa sasa ndipo unakumbuka ile ‘verse’ ya Ben Paul akisema kuwa ‘Kiziwi ukimwambia nakupenda hakusikii’, jamani hivi mnaona kama ninavyoona mimi?
Hivi mnamuona huyu kocha maisha yake ya msimu ujao kusalia unyamani licha ya kufanya vizuri kwa timu yake ya Simba.
Ila naamini atakuwa ametengeneza ‘CV’ kubwa sana ndani ya kikosi cha Simba akichukua ubingwa, hapo sasa sio ‘win win situation’ bali inakuwa ‘one win other lost’ yaani Simba ilitarajia itakuwa Sven atanufaika wakati na klabu yenyewe itanufaika.
Unaweza kuhoji kuwa kama ikichukua ubingwa Simba itakuwa haijanufaika ? Jibu lake rahisi tu, kweli wamenufaika ila kusudio lao wamefike mbali zaidi ya walipofika ligi ya Mabingwa.
Hadi sasa naamini Patrick Aussems ndiye kocha aliyewapa manufaa sana timu ya Simba kutokana na kuchukua ubingwa wakati huo timu imefika robo fainali ligi ya mabingwa Afrika.
Juu ya Sven huenda ukanielewa siku moja ikifika, naamini kabisa kwa sasa unaweza ukasema chochote juu ya maendeleo yake kwakuwa timu inafanya vizuri na utakuja kunikumbuka.
Ila ukitaka kutaja timu ambayo imefanya vizuri msimu huu na kuonekana kuwa na uwezo mkubwa na kuonesha kandanda safi kabisa ni Simba SC.
Wakati watu wa muziki wakizama Youtube kuangalia ngoma ya Ali Kiba ‘So hot’ huku wengine wakiendelea kutoa pongezi kwa Diamond kwa kufikisha watazamaji bilioni moja duniani kote kupitia you tube kesho kutakuwa na mtanange wa kukata nashoka Yanga watawakaribisha Azam FC, utakuwa upande gani bado linabaki swali kwako.
Usisahau kutoa maoni yako hapo chini juu ya haya tunayoendelea kuyaandika nawe unaweza kusema ya kwako na watu wengine wakayapitiaa na kupata faida nia soka la Tanzania liende mbele.
Comments
Loading…