Menu
in , , ,

SIMBA KUWAKABILI MBEYA CITY VPL

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia raundi yake ya tano kesho (Septemba 21
mwaka huu) kwa mechi huku vinara Simba wakiwakaribisha Mbeya City kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Uwanja wa Mkwakwani, Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo
Shooting Stars na Rhino Rangers ya Tabora. Mtibwa Sugar itakuwa mgeni wa
Tanzania Prisons katika pambano litakalochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine jijini Mbeya.

Nayo Kagera Sugar itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake wa Kaitaba mjini
Bukoba kuvaana na Ashanti United ya Dar es Salaam katika mechi
itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob Adongo kutoka Mara.

Ligi hiyo itakamilisha mzunguko wa tano keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu)
kwa mechi tatu ambapo Azam na Yanga zitacheza Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam huku JKT Ruvu ikikwaruzana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam
Complex.

Ruvu Shooting inayokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi itakuwa
mgeni wa Coastal Union katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga.

Wakati huo huo, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea wikiendi hii kwa
mechi kumi na moja. Kundi A kesho (Septemba 21 mwaka huu) kutakuwa na mechi
kati ya Transit Camp na Green Warriors (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam),
Tessema na African Lyon (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi).

Ndanda itacheza na Villa Squad kwenye Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati
keshokutwa (Septembe 22 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Polisi Dar es
Salaam na Friends Rangers katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Kundi B kesho (Septemba 21 mwaka huu) ni Mkamba Rangers dhidi ya Burkina
Faso kwenye Uwanja wa CCM Mkamba, na Mlale JKT itakuwa mwenyeji wa
Kurugenzi Mafinga kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Keshokutwa
(Septemba 22 mwaka huu) ni Majimaji na Kimondo katika Uwanja wa Majimaji.

Mechi za kundi C kesho (Septemba 21 mwaka huu) ni Pamba dhidi ya Polisi
Dodoma (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Stand United na Polisi Tabora
(Uwanja wa Kambarage, Shinyanga) na Kanembwa JKT itacheza na Mwadui kwenye
Uwanja wa Kawawa ulioko Ujiji. Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) Polisi
Mara na Toto Africans zitacheza Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

* *

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Leave a Reply

Exit mobile version