in

Simba kucheza kwa Hisani ya Maalbino

Chama cha waandishi wa habari za michezo hapa nchini (Taswa) kimeanda mchezo maalum wa kirafiki wa kupinga mauaji ya malbino hapa nchini

Mchezo huo utahusisha baina ya wachezaji wa nje ya Tanzania wanaocheza soka la kulipwa hapa nchini kwenye timu mbalimbali za ligi kuu Tanzania bara na timu ya Simba.

real-life-index-spl_675139a

Katibu mku wa Taswa Amir Mhando anasema mchezo huo utachezwa siku ya jumamosi May 2 /2009 kwenye dimba la Uhuru hapa jijini Dar es salaam na tayari wachezaji hao wa kulipwa wameshakubali kucheza mchezo huo

Kwa upande wake nahodha wa timu hiyo ya wachezaji wa kulipwa Boniface Ambani anaechezea timu ya YANGA toka nchini Kenya anasema wamefurahi kupata nafasi hiyo kucheza mchezo huo wa kupinga mauaji hayo ya Albino hapa nchini

Na kueleza wao wapo wakutosha na wameshajianda kwa kipute hicho na wanahakika elimu itafika kwa jamii kuhusu kupiga vita mauji ya albino

Nayo timu ya Simba kupitia kwa katibu wake Muhina Kaduguda amesema watacheza mchezo ingawa wameshitukizwa mno

Kaduguda anasema mara ya kwanza walijua timu ya Yanga ndio ingecheza mchezo huo lakini wamekata ila wao kutokana na lengo la mchezo huo wamekubali kucheza mchezo kwa nia moja tu ya kutoa elimu kwa Watanzania kuhusu kupiga vita mauji ya albino

Kwa upande mwingine Kaduguda anasema kwasababu mchezo huo umeandaliwa na chama cha waandishi wa habari na Simba inapata msaada mkubwa toka kwao basi hawawezi kuwaangusha

Baadhi ya wachezaji toka njee ya Tanzania wataunda timu hiyo ya wachezaji wa kulipwa ni pmoja na Boniface Ambani, Ben Mwalala, Mike Barasa na Morisi Sunguti (Yanga – Kenya), Wisdom Ndlovu (Yanga – Malawi) Eme Ezechuku (Simba – Nigeria) Mike Katende (Kagera Sugar – Uganda) Osebon Manday (Azam FC – Kenya) Vladil Niyokuru (Azam Fc – Burunndi) Dan Wagaruka(Azam Fc Uganda) na wengine wengi

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply
  1. MECHI IMEBADILISHWA SIMBA WATACHEZA NA ZANZIBAR HEROSE JAMAA WAMEENDA KWAO WAMESHINDWA KUELEWA ZIMA YA MCHEZO HUO KWA SABAB KWAO HAKUNA MAUAJI HAYA. PONGEZI SANA AMBANI KWA JUHUDI ZAKO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Could you please ASSIST

Barcelona 0-0 Chelsea