*Evra Juventus, mbadala wa Cole atua Chelsea
*Arsenal, Man U, Chelsea wagombea mchezaji
*Kocha mpya wa Manchester United, Louis van Gaal anataka kumsajili Wesley Sneijder.
Arsenal wamekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Barcelona, Alexis Sanchez kwa gharama ya pauni milioni 35.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile aliyewika sana kwenye fainali za Kombe la Dunia amechezea Barca mechi 141 na kufunga mabao 47.
Sanchez (25) hakuwa akipata muda wa kutosha dimbani kwa kutopangwa kwa kuwa na nyota wa kimataifa Barca, ndiyo maana akaamua kuondoka.
Ilikuwa apelekwe Liverpool kama sehemu ya dili la Barca kumsajili Luis Suarez (27) lakini Sanchez alikataa, akisema anaipenda Arsenal.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekuwa Brazil kwa ajili ya kuchambua mechi za Kombe la Dunia kwa Kituo cha Televisheni cha Ufaransa na alikutana huko na wakala wake na yeye mwenyewe.
Sanchez alisema ana furaha kujiunga na klabu yenye kocha mzuri kama huyo na wachezaji wanaojituma wakiwa na washabiki wengi kote duniani.
Arsenal wanakaribia kukamilisa usajili wa beki wa kulia, Mathieu Debuchy (28) wa Newcastle United ambaye tayari ameshafanya vipimo vya afya.
Wachezaji ghali zaidi waliokamilisha usajili kiangazi hiki ni David Luiz aliyekwenda Paris St-Germain kwa pauni milioni 40 kutoka Chelsea na
Diego Costa aliyejiunga Chelsea kutoka Atletico Madrid kwa pauni milioni 32.
Naye Cesc Fabregas alijiunga Chelsea kutoka Barcelona kwa pauni milioni 30, Ander Herrera kutoka Athletic Bilbao kwenda Manchester United kwa pauni milioni 29 na Luke Shaw kutoka
Southampton kwenda Manchester United kwa pauni milioni 27.
Adam Lallana ametoka Southampton kwenda Liverpool kwa pauni milioni 25 huku Fernando akitoka Porto na kujiunga Manchester City kwa pauni milioni 12.
Man U wamtaka Sneijder, Blind
Sneijder (30) alikuwa na Robin van Persie kwenye michezo ya fainali za Kombe la Dunia na wote wakiwa Wadachi wanaweza kuwa sura mpya hapo.
Sneijder kwa sasa yupo Galatasaray ya Uturuki wanaosema wanaweza kumwachia kwa pauni milioni 16.
Manchester United, Liverpool, Chelsea na Arsenal wanapigana vikumbo kumsajili winga wa Benfica, Joao Filipe (15) aliyebatizwa jina kla ‘Cristiano Ronaldo’ ajaye.
Kadhalika wanamgombea kipa Joao Virginia mwenye umri huo huo wa miaka 15 pia.
Wakati Liverpool wakielekea kukamilisha mauzo ya Luis Suarez kwa Barcelona, Fifa wamekataa rufaa ya mchezaji huyo kupinga kufungiwa kwa miezi minne kwa sababu za utovu wa nidhamu.
Suarez anauzwa kwa pauni milioni 75 huku Arsenal wakiwaambia Fiorentina ya Italia wawapatie pauni milioni sita ili wamsajili kiungo wao Mikel Arteta (32) aliye katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake.
Roma wamewapa Manchester City hadi Julai 21 kumsajili beki wao wa kati wa Morocco Mehdi Benatia (27).
Chelsea nao wanajaza pengo la Ashley Cole kwa kuanza mchakato wa kumsajili beki wa kushoto wa Atletico Madrid, Filipe Luis (28) kwa pauni milioni 20.
Cole (33) anahamia Roma huku Arsenal bado wakisikilizia iwapo wanaweza kumpata kiungo Mjerumani Sami Khedira (27) wa Real Madrid.
Winga wa Colombia, Juan Cuadrado (27) huenda akahamia Manchester United kutoka Fiorentina.
Mshambuliaji wa Liverpool, Iago Aspas (26) anatarajiwa kujiunga na Sevilla baada ya kushindwa kung’ara Anfield.
Brendan Rodgers anafikiria pia kumnunua beki wa kushoto wa Swansea, Ben Davies (21) kwa pauni milioni 10.
Man U pia wanataka kumsajili beki wa kushoto wa Wolfsburg na Uswisi, Ricardo Rodriguez (21) iwapo beki Patrice Evra atatekeleza matakwa yake ya kuhamia Juventus.
Evra aliyekuwa nahodha msaidizi wa Man U alisaini mkataba mpya wa mwaka mmoja Old Trafford, lakini sasa amewaambia kwamba anataka kwenda Juventus.
Kocha Louis van Gaal pia anataka kumsajili beki Mdachi mwenzake, Daley Blind (24) kutoka kwao Feyenoord.
Liverpool wanakamilisha usajili wa Lazar Markovic (20) kwa pauni milioni 20.
Sunderland wanataka kumsajili kiungo wa Nigeria,
Michel Babatunde (21) anayecheza Volyn Lutsk ya Ukraine.
Aston Villa wamemsajili Joe Cole (32).
Manchester United wametoa nafasi ya mwisho kwa mshambuliaji Bebe (23) na kiungo Anderson (26) kuonesha uwezo wao kwenye ziara nchini Marekani.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata (21) anakaribia kunaswa na Juventus.
Comments
Loading…