in , , ,

SAMATTA MTAA UNAKUHITAJI ILI UKUBEBE.

Ligi mbalimbali barani ulaya zimeisha, mapumziko yanatupa nafasi ya
kuusubiri mwezi wa nane ambapo ligi ndipo zitakapoanza tena.

Burudani mpya yenye kila kitu kipya tutaanza kuishuhudia kwenye mboni
zetu za macho.

Matunda ya usajili tutakuwa tunayashuhudia kama ni matunda mema au
siyo mema, vipaji vipya vitakavyotawala katika ulimwengu wa soka
vitakuwa kwenye masikio yetu wakati waandishi mbalimbali na
watangazaji mbalimbali wakivisifia.

Ushindani wa ufungaji magoli katika ligi mbalimbali baina ya
washambuliaji mbalimbali ukiongeza utamu wa mchezo huu unaoitwa soka.

Mchezo ambao una mashabiki wengi kila kona ya dunia, mchezo ambao
ukifanikiwa unakuwa umefanikiwa kweli.

Mchezo ambao unaingiza pesa nyingi sana nje na ndani ya uwanja. Ndani
ya uwanja pesa huingia kipindi pale mchezaji anapokuwa katika kiwango
kikubwa mpaka kupata mkataba na marupurupu mengi ndani ya timu yake.

Nje ya uwanja ni pale mchezaji anapofanikiwa kuwa balozi wa makampuni
mbalimbali ya kibiashara na hapa ndipo watu wengi huingiza pesa nyingi
sana.

Kiwango cha ndani ya uwanja kinamchango mkubwa sana kwa mchezaji kuwa
balozi wa makampuni mbalimbali ya kibiashara, lakini hii haitoshi
kwake yeye kuongeza idadi ya makampuni.

Hapa kitu pekee kinachombeba mchezaji ni uso wake unavyotazamika mbele ya jamii.

Ukaribu wako na jamii ukoje? Jamii inakutazamaje? Unashirikiana vipi
na jamii na kwa kiwango gani?

Haya ni maswali muhimu sana ambayo mfanyabiashara yoyote hujiuliza
kabla hajaamua kumpa mchezaji kuwa balozi wa bidhaa yake.

Mwisho wa siku mfanyabiashara atahitaji faida , na faida inatokana na
wateja wake, wateja wake ni jamii na jamii hii ndiyo inayotakiwa iwe
karibu na mchezaji husika ambaye atakuwa na msaada mkubwa kwa bidhaa
ya mfanyabiashara kufika kwa jamii.

Kwa hiyo hapa ukaribu wa mchezaji na jamii ni kitu cha muhimu sana ili
kuwa na muunganiko mzuri wa kibiashara kuanzia kwa mfanyabiashara.

Mfanyabiashara atavutika sana anapomuona mchezaji yuko karibu na jamii
kwa kiasi kikubwa kwa sababu hiyo itakuwa nafasi nzuri kwake kumpa
ubalozi wa bidhaa yake ili aweze kuifikisha vizuri kwa wateja wake
ambao ni jamii iliyo karibu na mchezaji.

Kipindi cha mapumziko ya ligi hutumiwa vizuri na wachezaji kwa
mapumziko, kukaa karibu na jamii ili kujitengenezea mazingira mazuri
ya kibiashara.

Mchezaji unapokuwa karibu na jamii mfano kutembelea kwenye vituo vya
kulelea vipaji vya vijana. Hivi vituo huitaji morali kutoka kwa
wachezaji wakubwa.

Vijana waliopo kwenye vituo hivi huitaji zaidi morali ya kupigana ili
kufika sehemu ambayo mchezaji yupo.

Asilimia kubwa ya hawa vijana hawajui jinsi ya kuishi katika mazingira
ya kiuweledi katika soka, huitaji mtu ambaye atawaingizia neno lenye
nguvu ndani yao.

Kupeleka mipira au vifaa vya michezo kwenye vituo hivi vya mpira
havitoshi, uwepo wa mchezaji kwenye vituo hata kwa dakika 30 akicheza
nao na kuwapa mawazo vina maana kubwa.

Ndipo hapo Nike, Adidas , Puma atavutika kuja kuwekeza kwako kwa
sababu kaono unajali vipaji vya mpira, na wao wanahusika kuuza bidhaa
za michezo, wataogopa nini kuwekeza kwako na kukupa hata nafasi ya
kuwapelekea vifaa vya michezo viongozi wa vituo hivi ?

Kuna mashirika mengi ya haki za binadamu ambayo yanahitaji mabalozi
wao wa kupigania haki za binadamu, wakati huu wa likizo ndiyo ulikuwa
mzuri kwa mchezaji kuwa karibu na jamii amabazo zinanyanyasika na
kuwafariji.

Utapata dhawabu ,pia Mungu atakuletea shirika la haki za binadamu
ambalo litakutaka uwe balozi wao na wewe ukaingiza pesa.

Ndicho kitu ambacho Samatta anajisahau, jamii inamwitaji sana kipindi
hiki ili imbebe.

Inasikitisha sana kwa Samatta kutoonekana hata kwenye mechi mbalimbali
kila akiwepo Tanzania.

Wiki iliyopita Sakho alihudhuria mechi katika uwanja wa Amani
iliyoandaliwa mahususi kumuaga Ninja.

Hii inaonesha hajitengi na jamii kama ilivyo kwa Victor Wanyama
kuhudhuria Ndondo Cup. Kuna mengi ya kufanya ili uwe karibu na jamii,
ili jamii ikubebe.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

HIZI VURUGU ZINAFUATA MAELEKEZO YA KOCHA AU TUNAFURAHISHA MASHABIKI?

Tanzania Sports

RONALDO DE LIMA ALIKUWA NA ROHO YA KIJERUMANI KWA WAJERUMANI..