Yanga wamepunguza gepu la alama 5 hadi 2 dhidi ya kinara wa msimamo wa Ligi Kuu Simba, Mnyama ana pointi 54 huku Wana jangwani wakifikisha alama 52 kutokana na ushindi wa goli 2 kwa 0 na maafande wa Ruvu
Mchezo huo, ulianza kwa kasi ya chini kwa kila upande kushambuliana kwa zamu hadi dakika ya 32 Msuva akiifungia Yanga goli la kwanza kwa mkwaju wa penati lililo dumu kwa kipindi cha kwanza
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi hasa kwa timu ya RUVU wakilisakama lango la Yanga ili kusawazisha goli, wakati mpira ukielekea ukingoni Emmanuel Martin akaiandikia Yanga goli la pili akimalizia krosi murua ya Simon Msuva.
Mambo manne tuliyo jifunza kwenye mechi ya RUVU Shooting na Yanga
1.Marefa bado ni changamoto kwenye Ligi yetu
Refa wa mchezo huu alishindwa kabisa kutafsiri sheria kwa ufasaha hasa kipindi cha kwanza, alikataa goli sahihi la Yanga lilofungwa na Chirwa, alitoa penati kwa upande wa Wana jangwani ambayo beki hakuwa ameunawa mpira, hali kadhalika kadi nyekundu ya kimakosa kwa Mzimbabwe Obrey Chirwa
2.Kessy, Mahadhi, Martini na Mwashiuya wanaitaji kupata dakika nyingi uwanjani
Bila shaka kiwango walicho onesha nyota hao dhidi ya RUVU bila shaka wanaitaji kupata dakika nyingi kuliko kukaa benchi, wakiendelea kuaminiwa watakuja kuwa msaada ndani ya klabu kwa miaka ya hivi karibuni
3.RUVU Shooting ili ukosa ubora wa Abraham Mussa wa siku zote
Abraham Mussa amekuwa ndiye mchezaji tegemezi ndani ya kikosi cha Maafande hao, licha ya kucheza kwa dakika zote uwanjani lakini hakuwa kwenye wakati mzuri, alishindwa kuipenya ngome ya Yanga licha ya kuwa pungufu kwa muda mwingi uwanjani.
4.Yanga pumzi hukata hasa kipindi cha pili
Kocha Lwandamina inabidi awe makini na tatizo la hivi karibuni timu pumzi kukata mapema hasa kipindi cha pili, tumeshuhudia kwenye mechi za hivi karibuni mfano dhidi ya Wacomoro Ngaya na Simba, hata kwenye mechi na RUVU walionekana wamechoka kipindi cha pili kama umakini wa Maafande hao ungekuwa mkubwa basi Yanga wangekuwa na wakati mgumu