in , , ,

Ronaldo namba moja Real Madrid


*Apewa gari ya ‘Audi’ ghali kuliko wenzake
*Bale atupwa mbali kuliko Ramos, Alonso

Nani alisema Gareth Bale ndiye mchezaji muhimu zaidi kwa Real Madrid kwa usajili wa pauni milioni 85? Bado Cristiano Ronaldo ndiye anatamba.

Kana kwamba kuthibitisha hilo, klabu hiyo imetoa magari kwa wachezaji katika utaratibu wake wa kawaida, na Ronaldo amepewa Audi ya bei ghali zaidi.

Hiyo ni sehemu ya ushirika kati ya Los Blancos na kampuni ya Audi, ambapo wachezaji 23 wa kikosi cha timu hiyo na kocha hupewa gari jipya kabisa aina ya Audi kila mwaka.

Hii ni moja ya hamasa kubwa kwa wachezaji kukipiga Santiago Bernabeu lakini wakishaingia lazima waonyeshe uwezo, vinginevyo hawadumu.

Makabidhiano ya funguo za magari hayo yamefanyika na kugeuzwa kuwa hafla ya promosheni na kushuhudiwa na kushangiliwa na wengi.

Mgawanyo wa nani anapata modeli ipi umeonekana kama ishara ya ni mchezaji yupo yupo juu zaidi, na japo Bale alimzidi Ronaldo katika bei ya kuwanunua, Audi wamempa Ronaldo gari ya ghali zaidi, tena kwa mbali kulinganisha na aliyopewa Bale.

Audi ya ghali zaidi iliyotolewa ni RS6 ambayo bei ya kuanzia ni €129,100, na mchezaji pekee aliyepewa hiyo ni Ronaldo ikiwa na vikorombwezo vingi na nafasi kubwa.

Hata baada ya Ronaldo, anayefuata si Bale bali ni
Xabi Alonso aliyechukua Audi ya thamani ya €96,110 S7, huku Sergio Ramos ambaye ni nahodha msaidizi alipewa RS5 lenye thamani ya €90,730.

Kocha Carlo Ancelotti alipewa Audi aina ya A8, ambayo bei yake inaanzia €85,320, na kocha mwenyewe alionekana kutoamini macho yake kwa jinsi alivyolipenda.

Wachezaji wengine ‘wakubwa’ waliofuatia kwa zawadi ya Q7 zenye thamani ya €59,900 ni Gareth Bale, Iker Casillas, Fabio Coentrao, Angel Di Maria, Sami Khedira, Asier Illarrramendi, Isco, Jese, Marcelo, Luca Modric, Nacho na Pepe.

Chini yao wamekuja akina Karim Benzema, Alvaro Arbeloa na Alvaro Morata waliopewa SQ5 zenye thamani ya €58,500.

Baada ya hapo kuna Carvajal na Diego Lopez wote wakipata gari yenye thamani ya €37,240, modeli Q5. Mwisho ni kipa namba tatu, Jesus Fernandez aliyepewa Audi ya thamani ya €23,830, aina ya A3 Sportback.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Steven Gerrard kuwa beki?

Arsenal raha tupu kileleni