OFISI ya Mwendesha Mashtaka ya serikali ya Uswisi imefungua jalada la uchunguzi wa makosa ya jinai dhidi ya rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu duniani, Gianni Infantino. Mchakato huo unafanyika kutokana na mwendesha mashtaka mkuu, Stefan Keller kudai kikao kilichowahusisha Infatino na mwanasheria mkuu wa serikali ya Uswisi, Michael Lauber na mwendesha mashtaka wa Upper Valais, Rinaldo Arnold kina dalili zote za uvunjaji wa sheeria
Kwa mujibu taarifa iliyotolewa kutoka ofisi ya mwendesha mashtaka imesema, mwendesha mashtaka mkuu Stefan Keller amebaini kuwa kikao cha watatu hao Infantino, Michael Lauber na Rinaldo Arnold ni kina dalili za makosa ya jinai.
“Kuna matumizi mabaya ya ofisi ya umma ambayo ni kinyume cha sheria ya makosa ya jina Ibara ya 312, uvunjaji wa sheria ya faragha ibara ya 320 ya sheria ya makosa ya jinai, kushiriki kutenda na kulinda maksoa ya jinai kwa mujibu wa ibara ta 305 na mengine yanayohusiana nayo. Nyongeza ya makosa ya jinai na kanuni zinazoongoza kufanyika uchunguzi zaidi,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Hivi karibuni ilitolewa taarifa ya kuthibitisha kwamba Stefan Keller ameomba kibali kwa Kamati ya Bunge la Uswisi kufungua kesi ya jinai dhidi ya mwanasheria mkuu Michael Lauber.
Taarifa ya Keller imehitimisha kwa kusema, “Kesi hiyo imetokana na mwenendo wenye mashaka wa mwanasheria mkuu Michael Lauber, rais wa Fifa, Gian Infantino na mwanadesha mashtaka wa umma mwendesha mashtaka wa umma Rinaldo Arnold.”
Lauber na Infantino walikutana mara mbili mwaka 2016 ambao Infatino alichaguliwa kuwa Rais wa shirikisho la mpira wa miguu duniani, Fifa.
Mwezi uliopita katika mkutano wa Baraza la Fifa wajumbe walimuuliza Infantino juu ya madai hayo, lakini Rais huyo alisema ni upuuzi na tuhuma dhidi yake zipuuzwe. Katika taarifa yake Infatino alisema “Kukutana na mwendesha mashtaka mkuu au mwanasheria mkuu wa serikali ya Uswisi ni haki kisheria na dalili heshima kubwa. Hakuna sheria iliyovunjwa, wala si kukiuka sheria yoyote ile. Kwa muktadha huo, pia ni sehemu ya majukumu yangu nikiwa Rais wa Fifa.
“Kumekuwa na mlima wa maswali. Kwahiyo ni heshima kwangu kumkaribisha na kumwomba mwanasheria mkuu wa serikali ya Uswisi kutoa ufafanuzi juu ya kikao hicho ili kuondoa mashaka yaliyopo, nikiwa na matumaini kuwa endapo kuna uvunjaji wa sheria za makosa ya jinai na kuchafua taswira ya FIFA kwa namna yoyote yaoneshwe kwa mujibu wa sheria,”
Kwa upande wake FIFA na Infantino wamethibitisha kuwa watatoa ushirikiano katika uchunguzi huo.
Infantino ameongeza kuwa, “Lilikuwa lengo tangu siku ya kwanza na litabaki kuwa lengo langu kutoa ushirikiano kwa mamlaka za serikali katika uchunguzi wowote ambao unahisiwa kukiuka sheria za nchi,Fifa. Maofisa wa Fifa wamekutana na mwendesha mashtaka katika nchi mbalimbali duniani kwa madhumuni ya namna hii ili kuondokana na mashaka,”
“Watu waliobainika kuvunja sheria wamekutwa na makosa na wengine kufungwa, lazima tuishukuru Fifa kwa ushirikianoinaotoa, na hasa kwa nchi kama vile Marekani ambako ushirikiano wetu Fifa na mamlaka zinazohusika umeleta matokeo ya takribani watu 40 walikutwa na makosa kutenda jinai. Kwahiyo, ninabaki katika msimamo uleule naunga mkono michakato yote ya kisheria na mahakama. Hivyo basi, ninaunga mkono mchakato huo, na Fifa itabaki kuwa mshirika nambari moja wa mamlaka za Uswisi.
Comments
Loading…