UVUMI umeshika kasi kwenye kolido la Man City kuhusiana na kocha wao aliyewapa mataji 6 ya Ligi Kuu. Tena akitwaa mataji hayo kwa soka safi, kiwango maridadi huku mashabiki wao wakitembea vifua mbele kujivunia timu yao. Hata hivyo wahenga wanasema, mambo yote mazuri lazima yafike mwisho. Hivi ndivyo inavyoonekana kwa utawala wa Pep Guardiola. Licha ya kusaini mkataba wa miaka miwili mwaka jana, lakini uvumi wa kuondoka mapema umeshika kasi na uwezekano wa kocha huyo kung’atuka upo mbioni.
Ishara za mashabiki wa Man City na taarifa za ndani za uongozi wa klabu hiyo umekiri kuwa kwenye makakati kabambe wa kutatua matatizo yanayowakabili msimu huu ya kupata matokeo mabaya, na kushuka viwango vya kwa baadhi ya wachezaji.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la hapa England limekariri vyanzo vya taarifa ndani ya klabu ya Man City ambazo zinadai kuwa Mhispania huyo amekusudia kutatua changamoto za Man City ikiwemo kuorodhesha wachezaji wa kusajiliwa ili kuimarisha kikosi chao kwa msimu ujao. Lakini pia taarifa ya pili inaeleza kuwa suluhisho lingine huenda likawa yeye kuondoka kwenye klabu hiyo. Man City wanashikilia nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu England, pamoja na kwamba wapo nafasi hiyo lakini upo uwezekano wa kufuzu nafasi nne za juu kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao jambo ambalo linaaminika kuwa litavutia wachezaji wengi kujiunga na klabu hiyo kwani watakuwa na uhakika wa kushiriki mashindano ya Ulaya pamoja na kupata marupurupu zaidi.
“Kadiri hali mbaya inavyoongezeka, ndivyo inavyokuwa vigumu Pep kubaki. City wanaitazama hali halisi wanaoyokabiliana nayo sasa, wanasubiri msimu umalizike na kuelekeza akili zao msimu ujao. Wanatakiwa kupambana kumaliza nafasi nne za juu. Wiki chache zilizopita kama watu wangehoi uwezo wa Man City kumaliza nafasi tano za juu huenda lingekuwa rahisi kwa sababu hawashindwi kufanya hivyo. Lakini lipo lingine linajirudia, Pep alikuwa anasema labda ameishiwa mbinu za kuongoza City, ingawa si kweli kaishiwa ila inawezekana lipo jambo nyuma hasa la kuondoka,” lilieleza Daily Mail.
Tetesi zimeibuliwa kuwa huenda Mkurugenzi wa Michezo wa Man City, Hugo Viana akaelekeza nguvu zake kumshawishi Mirco Silva kujiunga na Man City kama kocha mkuu akichukua nafasi ya Pep Guardiola.
“Man City walipoteza kwa Nottingham Forest, walistahili kufungwa kwa sababu hawakuwa kwenye kiwango kikubwa. Kisha wakaenda kuchuana na Brighton, kwahiyo walipotza pointi tano ndani ya wiki mbili na haraka hali ngumu ikawazingira tena.”
Licha ya kwamba Man City wameendelea kubaki na kocha wao, lakini upo uwezekano akaondoka katika klabu hiyo kama njia ya kupisha mawazo mapya kuelekea mafanikio kama aliyoyaleta. Upo uwezekano wa klabu hiyo kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chao, huku wachezaji wakongwe kama Kevin De Bruyne, Bernando Silva na Ilkay Gundogan wakioneshwa mlango wa kutokea.
Kevin De Bruyne na Gundogan mikataba yao inamalizika msimu huu 2024/2025 wakati tetesi zinaeleza kuwa mkurugenzi mpya Hugo Vianna ataangalia uwezekano wa kikosi hicho kusonga mbele bila Bernado Silva baada ya kuporomoka kiwango chake. Nafasi nyingine inayotazamiwa kufanyiwa mabadiliko ni golikipa ambapo Ederson amekuwa wakifanya makosa mengi yaliyoigharimu timu hiyo na anadaiwa kupungua umakini wake langoni.
Awali ilidhaniwa katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari huenda Man City angemsajili Andrea Cambiaso kutoka klabu ya Juventus. Pia nafasi ya kiungo na mabeki wa kulia na kushoto zinahitaji wachezaji wapya. Vilevile klabu hiyo inaangaalia uwezekano wa kuwaachana na baadhi ya wachezaji ili kukusanya fedha kwa ajili ya kusajili wachezaji wapya. Uamuzi huo unafanyika bila kuingiliana na ushiriki wao kwenye mashindano ya Klabu bingwa ya Dunia.
Kiwango kibovu cha wachezaji wa Man City kimechangia baadhi yao kukosolewa na kocha mkuu wa England, Thomas Tuchel ambaye amedai wamekosa makali kwenye eneo la mawinga ambako alimpanga Phil Foden na Marcus Rashford wa Aston Villa.
Aidha, Pep Gaurdiola bado ni lulu katika mchezo wa soka, hivyo inatarajiwa hata baada nya kuondoka kwake huenda akapata nafasi ya kufundisha timu nyingine. Lakini wakati fulani amewahi kubainisha kuwa akiondoka Man City atakuwa anaelekea kuwa kocha wa timu ya Taifa. Raia huyo wa Hispania anaweza kuajiriwa na timu mbalimbali ikiwemo nchini yake. Pia Brazil ni miongoni nchi ambazo ziliwahi kuhusishwa nazo. Lakini haifahamike kama atakuwa kocha nchi gani.
Kama zilivyokuwa zama za akina Arrigo Sachi, Jose Mourinho, Jupp Heykness,Luis Felipe Scolari, Guus Hiddink, Alex Ferguson, Arsene Wenger na wengineo ndivyo ambavyo machweo ya Guardiola yanavyomjia na kuungana na jopo la makocha wahenga.
Comments
Loading…