Historia inanionesha ukurusa mzuri na wenye kuvutia kwenye vitabu vya hawa watu wawili ambao hawakupewa nafasi kubwa.
Watu ambao wametoka kwenye ardhi ambazo zina mchanga wenye damu inayoitwa mpira wa miguu. Ardhi ambazo zinaheshimika sana kwenye mpira wa miguu.
Ardhi ambazo zimetoa nyota wengi wa mpira wa miguu. Leo hii ukimtaja beki Paolo Maldini moja kwa moja akili yako itakupeleka kwenye nchi ya Ufaransa.
Ndivo ilivyo kama nitakavyotaja hata jina la kipa Michael Platin. Akili yako itakuonesha sura ya nchi ya Ufarañsa, mabingwa wa kombe la dunia Mara mbili.
Nchi ambayo iliwahi kujaliwa vipaji maridhawa sana na mpaka sasa inazidi kuzaa vipaji maridhawa sana kwenye dunia ya mpira wa miguu.
Unamkumbuka Thierry Henry?, mshambuliaji bora na hatari kuwahi kutokea katika uso huu wa dunia ? Huyu katokea hapa Ufaransa.
Wakati Ufaransa wakiwa na Claudio Makelele , Italy waliwahi kubahatika kuwa na Gattuso, viungo wawili wa eneo la ulinzi .
Viungo ambao walikuwa wanaogopeka sana, wao nguvu ndizo zilikuwa sababu kuu yao ya kuendelea kuishi kwenye dunia ya mpira.
Wakati Italy ikiwa inajivunia kuwa na Gatusso ambaye alikuwa anatumia nguvu nyingi, dunia iliwapa zawadi watu wa Italy kuwa na Andrea Pirlo.
Mwanadamu pekee ambaye aliwekewa komputa ya mpira kichwani mwake. Kichwa chake kilikuwa na maarifa mengi sana ya mpira.
Kichwa chake kiliweza kukokotoa hesabu kali sana za mpira wa miguu ambazo zilionekana na watu wengi kuwa ni ngumu.
Kwa kifupi huu ndiyo upekee wa soka la Ufaransa na Italy. Yani soka ambalo limejaa vipaji haswaa , vipaji ambavyo vilikuja kuweka alama kubwa duniani.
Vipaji vya soka la Italy na Ufaransa halijawahi kuishia kwa kutoa wachezaji mahiri pekee tu kwenye mpira wa miguu.
Hata makocha wengi bora wametoka kwenye nchi hizi. Unamkumbuka Arrigo Sanchi ?, mwanamapinduzi mkubwa wa soka la Italy ?
Kwa sasa unaweza kuwatazama kina Carlo Ancelotti, Maurizio Sarri, Antonio Conte kama makocha ambao wanafanya vizuri pia.
Hii inatosha kuonesha kuwa soka la Italy huwa linatoa makocha bora kabisa, lakini kuna makocha ambao waliwahi kupewa timu kwa mashaka na wakoondoka kwa fedheha.
Chelsea imekuwa timu ambayo ina damu nzuri ya makocha kutoka Italy kufanya vizuri sana. Makocha wengi waliofanya vizuri Chelsea wametoka Italy.
Di Matteo anaweza kukumbukwa Chelsea kwa kuipa kombe la ligi la mabingwa barani ulaya. Kocha huyu alikuwa hapewi nafasi kubwa.
Aliichukua timu kama kocha wa muda, lakini alifanikiwa kuifikisha katika fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya na kubeba kombe hili.
Hadithi kama hii iliwahi kutokea kwa Real Madrid,baada ya Rafael Benitez kufukuzwa , Zinedine Zidane alikabidhiwa timu kama kocha wa muda baada akawa kocha mkuu kama ambavyo ilikuwa kwa Di Matteo.
Zinedine Zidane aliipa mafanikio makubwa sana Real Madrid, alichukua makombe 9 ndani ya miaka miwili na nusu, ikiwemo kuchukua ligi ya mabingwa barani ulaya mara tatu.
Lakini tofauti ya hawa makocha wawili ni moja tu. Wanafanana jinsi walivyoingia, walitumia mlango wa aina moja kuingia.
Lakini walivyotoka, Di Matteo alitolewa kwa fedheha ya kufukuzwa na Zinedine Zidane alijiudhuru kwa heshima.
Hapa ndipo ninapoanza kuwaza, Ole Gunnar anaweza akachukua sura ya nani kati ya hawa watu wawili ambao anafanana nao namna ambavyo ameingia kwenye timu.