|
||||
WACHEZAJI maarufu wa mpira wa kikapu kutoka Marekani walioko ziarani nchini wamesema ziara yao inalenga kusaidia maendeleo ya mchezo huo ili uzidi kukua na kuwafundisha vijana na wanaamini kuwa hilo litawezekana .
Pamoja na wachezaji kuja kutoa mafunzo Ubalozi wa Marekani nchini umetoa mipira 100 ya mchezo huo kwa Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini (TBF) ili kusaidia maendeleo ya mchezo huo kwa shule za sekondari.
Mchezaji mstaafu wa kikapu kutoka Chama cha Mpira wa Kikapu Marekani (NBA) ambaye pia aliwahi kupata medali ya dhahabu kwenye michuano ya Olimpiki, Jennifer Azzi alisema kwa upande wake atakazania zaidi mafunzo kwa kwa wasichana kwani anaamini wanawake wakipewa kazi wanaweza kuifanya vizuri zaidi.
”Nitafundisha maana ya mchezo huo, ribaundi,kucheza na hasa nataka kuwafundisha wanawake wenzangu kwani ni wachapakazi na ukiwafundisha pia wao wanaweza na wataupaisha mchezo huu,” alisema.
Alisema hiyo ni programu iliyoanzishwa ya kutembelea nchi mbalimbali barani Afrika kufundisha mchezo huo kwa vijana na mwaka huu ilikuwa ni zamu ya Tanzania.
” Nashukuru kufika hapa kwa niaba ya NBA , najisikia faraja kufundisha mchezo huu hasa kwa vijana na nafurahi kwa sababu mpira wa kikapu ni mchezo wa urafiki na upendo na mimi nataka sana kufundisha wanawake ili waje kuwa kama mimi.
”Ingawa wengi wanafikiri mchezo huu ni kwa ajili ya watu warefu, lakini sivyo kwani mpira wa kikapu unataka akili zaidi, unaweza ukawa mfupi, lakini ukacheza kiakili na ukashinda, hilo lisiwavunje moyo watu,” alisema.
Naye mchezaji wa timu ya San Antonio Spurs, Matt Bonner amewataka vijana kuwa ndoto za kuja kuwa wachezaji wa kulipwa hapo baadae.
”Mimi tangu mdogo nilikuwa na ndoto za kuja kuwa mchezaji nyota wa mpira wa kikapu na hilo limetimia, na kwa sababu hiyo nakuwa na deni la kutumia kipaji changu kuwafundisha vijana ili waje kuwa wachezaji nyota kama mimi.”
”Na ndio maana leo niko hapa kufundisha vijana jinsi ya kucheza mpira wa kikapu, kuwa kiongozi bora, nataka kuwafundisha jinsi ya kuwa mchezaji bora, kufanya vizuri shuleni na kuwa mtu mzuri,” alisema Bonner.
Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Lawrence Cheyo alisema wamefarijika na ugeni huo kwa sababu ni mara ya kwanza kupata ugeni wa hadhi ya NBA.
”Shukrani zimwendee Rais Jakaya Kikwete kwa kufanikisha hili ikiwa ni juhudi zake za kuendeleza michezo pia kampuni ya FHI ambayo iko mstari wa mbele kuhamasisha vijana kupima na kupambana na gonjwa la ukimwi.”
Cheyo alisema kozi zitakazoendeshwa na wachezaji hao zitahusisha shule za sekondari 13 kutoka jijini Dar es Salaam na wachezaji mbalimbali waliopatika kwenye mashindano ya mpira wa kikapu ya mitaani yanayoendelea.
Baadhi ya shule zitakazoshiriki mafunzo hayo ni Makongo, Jitegemee, Shaban Robert, Dar es Salaa, Loyola, Tegeta, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.
“Tulitaka hadi twende mikoani lakini muda wao wa kuwa hapa nchini ni mdogo, hivyo tunatarajia yale mafunzo ambayo watapata baaahi ya wahezaji mashuleni tutawapelekea na mikoani ili nao waweze kupata kitu cha kuwasaadia,” alisema Cheyo.
Saria, hongera sana kwa hii website yako, ila hongera zangu nyingi kwa Kasesela kwani anatumia ukaribu wake na mkuu wa nchi kuleta maendeleo ya kikapu katika Tanzania.
Na hili ni muhimu sana katika maendeleo ya kikapu Bongo. nawakilisha