in

Nyota wa Afrika wameyeyuka ‘Top Five’ Ulaya

Kanu

Hivi karibuni nilikuwa natazama picha mbiliza vikosi vya timu ya taifa ya Afrika kusini maarufu kama Bafana Bafana ya mwaka 1996 iliyoshiriki mashindano ya AFCON yaliyandaliwa nchini humo na wenyeji kutwa ubingwa mbele ya Tunisia na nyingine ya Cameroon wakati walipoibuka mabingwa wa AFCON mwaka 2002.

Katika picha ya Bafana Bafana ilikuwa na kama vile Lucas Radebe (amewahi kuwa nahodha wa Leeds United ya England), Mark Fish, Phil Masinga (alikuwa nyota wa Bari F.C ya Italia), Andre Arentes, Dokta Khumalo,Erick Tinkler na wengineo. Kilikuwa kikosi cha wanaume wa shoka.

Katika picha ya Cameroon ilikuwa na mastaa kama Rigobert Song, Piere Wome,Achile Webo, Patrice Mboma,Raymond Kalla, Samuel Eto’o Fils,Geremi Njitap na wengineo. Mastaa hawa walikuwa wakubwa si kwenye AFCON pekee bali hata Ligi za Ulaya kama England,Italia,Ufaransa,Ubelgiji,Hispania na Ujerumani pamoja n zingine.

Rudisha kumbukumbu ya fainali za AFCON mwaka 2000 kisha tazama vikosi vya Nigeria na Cameroon utagundua mastaa wengi walikuw wawanacheza timu kubwa barani Uaya.

Rudisha kumbukumbu kwenye fainali za AFCON mwaka 2002 utaona namna mastaa wa kiafrika walivyokuwa wanatamba barani Ulaya. Vikosi vingi vilikuwa na mastaa waliotokea Chelsea,Barcelona,Real Madrid, Manchester United,

Rudisha kumbukumbu kwenye fainali za AFCON mwaka 2004 utaona mastaa wengi walikuwa wanakipiga katika vilabu vya Ligi Kuu barani Ulaya. Walikuwa nyota waliotamba katika nafasi mbalimbali. kuanzia mabeki,viungo,mawinga na mwashambuliaji.

Vikosi vya timu za taifa kama vile Mali,Nigeria,Senegal,Cameroon,Afrika kusini, Ghana, Ivory Coast, Tunisia, Morocco kwa kuzitaja chache kwenye fainali za Kombe la dunia walikuwa na wachezaji ambao wanatamba katika vikosi vya vilabu mbalimbali barani Ulaya. Hata hivyo hali imekuwa tofauti.

Ukitazama Ligi Kuu tano bora za Ulaya utagundua nyota wengi wa Afrika hawapo. Ni kama wameyeyuka hivi na sababu za kutoweka kwenye vikosi vya timu vigogo.

Binafsi hali hiyo nilianza kuona mara baada ya fainali za Kombe la dunia mwaka 2002 zilizofanyika nchini Japan na Korea kusini. Fainali hizo kwangu ndiyo bora zaidi na ambako nyota wa Afrika wengi walikuwa wanakipiga katika timu kubwa barani Ulaya.

EPL (ENGLAND)

Zitazame timu kubwa nne za juu katika msimamo wa Ligi Kuu England. Liverpool wana staa wa Senegeal Sadio Mane na Nabi Keita wa Guinea. Hawa ni nyota waliofurukuta kupenya kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Lakini ukigeukia timu zingine kama Manchester United, Manchester City, Leicester City ama vigogo wengine kama Chelsea na Arsenal wachezaji wa kiafrika wameyeyuka. Arsenal wanaye Piere Aubameyang (Gabon), Mohammed Elneny (Misri) na Thomas Partey (Ghana), wakati Man City wanaye Riyad Mahrez, Leicester wanaye Kelechi Iheanacho na Wifred Ndidi raia wa Nigeria.

Nje ya hapo utaona vilabu vikubwa vya England havina mastaa wa kutosha kutoka Afrika. Ni kama vile wameyeyuka, tofautyi na mwanzoni mwa miaka 2000 ambapo kwenye kikosi cha kwanza unaweza kukutana nao watatu hadi wanne wakianza. Nyota wa Afrika wamezidi kuyeyuka barani Ulaya.

SERIE A (ITALIA)

Vigogo wa Serie A kama vile Juventus Turin,AC Milani, Inter Milan,Atalanta sio tmu zenye kuwabeba mastaa wa Afrika. Nyakati zimebadilika sana, hakuna nyota kaliba ya George Weah, KwadoAsamoah, Mohammed Kallon au Eto’o kwenye vilabu vikubwa. Ukiondoa AS Roma wenye beki wa kati mahiri kabisa Kolibaly timu zingine hazina wachezaji angalau watano katika vikosi vyao vya wachezaji 18 kuanza mechi. Timu za Serie A nazo ni kama wametosa vipaji vya Afrika. Ukibisha hilo tazama vikosi vyao jinsi vilivyo.

LA LIGA (HISPANIA)

Zitazame Barcelona, Real Madrid,Atletico Madrid, Sevilla au Atletico Bilbao hawana nyota wa kiafrika kamamzamani. La Liga hawana mastaa wengi kutoka frika. Zamani Barcelona walikuwa na nyota kama Samuel Eto’o lakini hakuna dalili kama nyota wa Afrika mwingine anaweza kuvalisha viatu vya Eto’o.

Geremi Njitap alikuwa nyota wa Real Madrid lakini siku hizi kikosi hicho hakina mastaa kutoka Afrika. Kana kwamba vipaji vimeadimika. Atletico Madrid walikuwa na Thomas Partey ambaye ameuzwa kwenda Arsenal, lakini kwa sasa hali ni tofauti kwani nyota wa Afrika wameyeyuka katika kikosi cha Deigo Simeone.

Klabu pekee ambayo imekuwa ikilinda utamaduni wa kusajili nyota wa Afrika ni Sevilla ambao nyota wengi kutoka Tunisia na Morocco wana historia nzuri. Lakini nako kama kulivyo kwingineko nyota wa Afrika wamekuwa adimu mno. Ingawaje pale Sevilla hakuna staa mwingine wa kiafrika mwenye jina kubwa kama Fredrick Kanoute aliyekipiga Mali baada ya kushindwa kupata nafasi kikosi cha Ufaransa.

BUNDESLIGA (UJERUMANI)

Bayern Munich wana nyota kutoka Afrika? Jibu ni hapana. Watazame kwenye kikosi chao cha sasa kilichoko kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Dunia hawana staa kutoka afrika. Hapa nina maana ya nyota wenye kuzichezea timu za taifa za Afrika sio waliochukua uraia wa Ujerumani kama Jerome Boateng,Kingsley Comman na uraia wa Ufaransa na wengineo.

Watazame Borussia Dortmund, kisha wageukie Schalke 04 na Bayer Leverkusen bila kuwataja Eitratch Frankfurt na FC Cologne, utaona nyota wa Afrika wameyeyuka katika timu kubwa za Bundesliga.

LIGUE 1 (UFARANSA)

Ligi Kuu Ufaransa ndiko mahali pekee ambako mastaa wa Afrika wamekuwa wakipata nafasi ya kuonesha vipaji vyao. Kuanzia klabu kama vile Auxerre, Olympique Lyon, PSG na Olympique Marseille zimewahi kuwa na nyota wakubwa kutoka bara la Afrika. Lakini kwa sasa hali ya mambo ni tofauti kwani nyita wengi wameishia kuchezea vilabu vya madaraja ya chini. Ukitazama ‘Top five’ ya Ligue 1 huwezi kuwaona nyota wa Afrika wanne kwenye vikosi vya kwanza. Hakuna akina El Gadji Diouf (Senegal), Joseph Desire Job (Cameroon) wengine.

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Mikel Arteta anataka nini kwa mshambuliaji wake?

Marvin Park

Mfahamu mchezaji mwenye uraia wa nchi nyingi