WAKATI jina lake likitajwa kuchukua jukumu la kuinoa Borussia Dortmund, wadaau wa soka walijiuliza swali moja tu: ni kipi ambacho kijana huyo angeliweza kukifanya kwa klabu hiyo yha Bundesliga? Kama unaongelea vipaji vilivyowahi kuonekana hapa duniani basi Nuri Sahin ni miongoni mwao. Usidhani ilikuwa rahisi kwa Real Madrid kumwaga fedha zao kumsajili mwanasoka mwenye asili ya Uturuki tena wa kuitwa Nuri Sahin.
Ndiyo, Florentino Perez na viongozi wenzake walimaliza kikao katika ofisi zao jijini Madrid na kulipitisha jina la Nuri Sahin kuwa mchezjai wao mpya wa kiungo. Kama umemwona Rtan Giggs akiwa amehamishwa kutoka winga hadi kiungo mshambuliaji ndivyo ambavyo ungemwona Mesut Ozil akiwa anakokota mpira kwa madaha kuelekea lango la adui. Katika miguu hiyo ya Ozil na Giggs ndipo ingeona namna Nuri Sahin angeuchezea mpira na kukimbia kwa kasi kuelekea lango la adui.
Je Nuri Sahin alikuwa mchezaji wa aina gani?
Nuri Sahin alikuwa mchezaji wa nafasi ya kiungo wa ushambuliaji. Angeweza kucheza namba nane au 10 na wakati mwingine unaweza kumlazimisha acheze winga wa kulia au kushoto. Ni mchezaji ambaye aling’arisha nyota ya Waturuki katika Ligi ya Ujerumani. Ni miongoni mwa vipaji ambavyo vimepamba mchezo wa soka na kutoa burudani.
Tatizo la Nuri Sahin lilikuwa ni nini?
Alipokuwa mchezaji tatizo lake kubwa ni kama lile la Prince Dube wa Yanga ambapo akiwa Azam alikuwa majeruhi mara kwa mara, lakini akiwa mzima wa afya njema shughuli yake ni kubwa mno. Au ungesema maisha yake kama mchezaji yalikuwa kama Waziri Mahadhi wa Yanga enzi hizo alikuwa kiungo mahiri sana, lakini naye kama gari bovu au spana mkononi. Akicheza mechi tano mfululizo basi kuanzia ya sita anakuwa majeruhi na kushinda kwenye vitanda vya hospitali.
Je ni ipi nafasi ya Nuri Sahin katika ukocha?
Makala haya hayalengi kuzungumzia umahiri wake katika uchezaji wa mpira na kuwa majeruhi wa mara kwa mara ama kuelezea matarajio ambayo hayakufikiwa akiwa mchezaji wa Real Madrid. Katika kufanya tathmini za kazi za makocha huyu ni miongoni mwa wale wanaovutia . timu yake inapocheza unaona dhahiri inaleta kitu cha kiufundi na ambacho hakuna mtu anaweza kukipinga. Kila madau wa soka anaweza kukubaliana na tathmini hii kuwa
Nuri Sahin anawakilisha kizazi kipya cha makocha ambao kinaonesha mpira wa miguu upo katika mikono salama licha ya changamoto za kulazimisha aina moja ya soka. Nuri Sahin sio kama Pep Gaurdiola. Nuri Sahin anataka kufuata njia ya Jupp Heykness kwa kuthamini vipaji na kuwaruhusu kuwa na ubunifu binafsi katika uchezaji. Pia timu yake huwa inacheza kwa kasi na inamudu presha yoyote. Kiufundi anaweza kucheza 4-3-3 au 3-1-3-2-1 ambapo msingi wake unaanzia kwenye nafasi ya kiungo yaani katikati ya dimba.
Nuri Sahin ukitazama mechi nyingi za Ligi ya Mabingwa au Bundesliga unagundua kwamba amewapa uhuru kiasi wachezaji wake kutumia maarifa yao katika kuwapngua maadui kwenye ngome zao. Ingawa ameweka mfumo wa kutumia lakini hajawabana wachezaji, ama kama anavyosema Ancelotti “kuwanyima taarifa nyingi ili kuepusha kuua vipaji vyao”. Kwamba wachezaji wanapopewa taarifa nyingi za mchezo na dhidi ya wapinzani wao wanapoteza maarifa binafsi ukiwemo ubunifu.
Kwahiyo uchezaji wa Borussina Dortmund ni miongoni mwa timu zinazolea vipaji na kutunza maarifa binafsi ya wachezaji kulikuwa kuwa watumwa wa mfumo wa kucheza (Style of play). Tangu Juni 14 mwaka 2024 alikabidhiwa jumu la kuinoa Borussia Dortmund. Ameiongoza timu hiyo katika michezo 2 na kushinda 12 pamoja na kutoka suluhu mara 4. Jumla tangu alipokuwa kocha wa Antalyaspor Oktoba 5 hadi Desemba 31, 2023 alicheza mechi 94 na kushinda 39 pamoja na kutoka sare mechi 24. Kiujumla ameongoza timu zake katika michezo 117 na kushinda mechi 51 na kutoka sare michezo 28.
Je kiufundi ana mbinu gani?
Kocha huyu kijana anatumia zaidi viungo na mawinga kumaliza mchezo wake. Anatetegemea upande wa kulia na kushoto kisha viungo kama injini ya timu yake, huku mshambuliaji akiwa mchezjai wa amwisho kukamilisha kazi ya timu. Mara nyingi mabao ya timu yake hufungwa kutoka eneo la 18, huku mashuti na pasi fupi fupi ndani ya boksi ni sehemu inayowapa wakati mgumu wapinzani wake. Ingawaje ni msimu wake wa kwanza kuongoza timu kubwa lakini ameonesha dhahiri aendako atahitaji kuvuka mipaka au kupanda juu zaidi kuinoa timu kubwa kuzidi Borussia Dortmund. Ukizingatiwa Bundesliga imejaa makocha wapya vijana ni dhahiri Nuri Sahin anakuwa miongoni mwa wale ambao wanaweza kuonesha makucha zaidi kiufundi.
Comments
Loading…