KATIBU mkuu wa Chama Cha Riadha Tanzania(AT) Suleimani Nyambui ameomba apewe robo ya fedha zinazotumika kudhamini mchezo wa soka ili aweze kurudisha hadhi ya mchezo wa riadha nchini kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Nyambui alisema kwamba tokea kuingia madarakani kwa rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete kumekuwa na muitikio mzuri wa wadhamini katika mchezo wa soka kuliko michezo mingine hali inayofanya michezo hiyo kudidimia kila siku zinavyokwenda mbele.
Alisema kwamba kama atapewa robo ya fedha zinazoelekezwa katika mchezo wa soka basi atazitumia katika kuibua vipaji vya wanariadha na kuweka mikakati endelevu ya kurejesha hadhi ya mchezo huo kama ilivyokuwa katika kipindi chao.
Mwanariadha huyo aliyetamba katika michezo ya olimpiki kwenye miaka ya 1970 alisema kwamba pamoja na wadau kudhamini zaidi mchezo wa soka lakini mchezo huo bado umeshindwa kuliletea heshima taifa zaidi ya kufanya vibaya kila kukicha.
Aliongeza kwamba kama mchezo wa riadha ambao una historia nzur ya kuliletea taifa heshima ukidhaminiwa kama mchezo wa soka basi leo hii taifa lingepata heshima kubwa sana kupitia mchezo huo
Aidha Nyambui alilaumu watendaji wa serikali kutoa kipaumbele zaidi katika mchezo wa soka hali inayofanya mchezo kama riadha, ngumi na michezo mingine kudidimia siku hadi siku.
“watendaji wengi wa serikali wamejikita zaidi katika kuendeleza mchezo wa soka na kusahau kabisa michezo mingine, hali inayofanya michezo hiyo kufa,”Alisema Nyambui.
Nyambui alisema kwamba kuna makampuni mengi tu nchini yanayotaka kudhamini michezo mingine lakini kwa sababu yanakosa msukumo kutoka kwa watendaji serikalini yanajikuta yakishindwa kufanya hivyo.
Alitoa mfano alipokuwa safarini nchini Australia aliwahi kusafiri na mmoja wa watendaji wa mgodi wa North Mara ambaye alimueleza kwamba wao wanachotaka ni maelekezo tu kutoka serikali ili watoe udhamini wao.
“alinieleza kwamba tunahitaji maelekezo kutoka serikali na aliniambia kwamba wanaweza kutoa mauzo ya jiwe moja tu la dhahabu na michezo nchini ikapiga hatua kubwa”alisema kwa uchungu Nyambui.
Nyambui aliongeza kwamba huo ni mfano mdogo tu wa wadhamini kutoka mgodi wa North Mara lakini anaamini kuna wadhamini wa aina hii lakini wanarudishwa nyuma na uwajibikaji mbovu wa watendaji wa serikalini.
Alisema kwamba kama kila kampuni nchini angalau itajitokeza kuwaendelezea walau wanariadha wawili kila moja basi mchezo huu utarudi kama ulivyokuwa miaka ya nyuma ambapo kulikuwa na wanariaha mashuhuri kama vile Filbert Bayi, Ikangaa na wengineo.
“Kuna akina Ikangaa wengi sana katika nchi yetu lakini ukosefu wa udhamini wa uhakika na udhaifu wa baadhi ya watendaji katika serikali yetu ndio unasababisha washidwe kufikiwa,”alisisitiza Nyambui
Maneno ya Nyambui yaliungwa mkono na Mjumbe wa Cha Cha Riadhaa Tanzania(AT) Juma Ikangaa aliyedai kuwa kukosekana kwa mipango na sera madhubuti ndiko kunaifanya riadha na michezo mingine kama ngumi ifikie hapa ilipo.
Alidai kwamba hakuna mipango madhubuti ya kuendeleza michezo hiyo hapa nchini hali inayothibitisha kwamba viongozi wengi serikalini hawana nia ya dhati kuona michezo hiyo inailetea sifa taifa kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Alidai kwamba wapo wanariadha wengi sana vijijini wenye uwezo kama wake lakini wanashindwa kuibuliwa kutokana na kukosekana kwa mipango ya kueleweka katika michezo hiyo.
Ikangaa mwanariadha wa zamani wa kimataifa aliyeshinda medali ya dhahabu katika mashindano ya marathoni yaliyofanyika New York Marekani kwenye miaka ya 1980 alisema kwamba anaamini watendaji wa wizara wamepelekewa mipango mizuri tu ya kuendeleza mchezo huo na AT lakini hawako tayari kuitekeleza.
Alisema kwamba kuna utofauti mkubwa sana wakati wakichezo mchezo huo kipindi chao na sasa ambapo kwa sasa mchezo huo unahitaji udhmani mkubwa ili mafanikio yaweze kufikiwa.
“Kipindi chetu tulijawa na uzalendo wa kupenda nchi na hata maisha hayakuwa magumu kama sasa, hivyo nyakati hizi mahitaji ya mchezo huo ni makubwa sana,”alisema Ikangaa
Ikangaa ambaye pia ni kocha wa timu ya taifa ya riadha inayojiandaa kwa michezo ya Afrika “All African Games” inayotarajiwa kufanyika jijini Maputo Musumbiji mapema mwezi ujao alisema kwamba kwa hali ilivyo itakuwa ngumu kwa timu yake kufanya vizuri.
Alisema kwamba mashindano hayo kwa kawaida huwa ni magumu pengine kuliko mashindano ya Olimpiki hali aliyodai kuwa inahitaji maandaliz mazuri ili waweze kufanya vizuri.
— On Tue, 7/12/11, Israel Saria <[email protected]> wrote:
From: Israel Saria <[email protected]>
Subject: Re: hiyo kaka
To: “Clecence Kunambi” <[email protected]>
Date: Tuesday, July 12, 2011, 5:17 AM
Ok.ngoja niipitie basi….thanks
Send from my Iphone
On 12 Jul 2011, at 13:06, Clecence Kunambi <[email protected]> wrote:
Na Clecence Kunambi
MICHUANO ya kombe la Kagame ilifikia tamati wiki hii kwa mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga kutangazwa wafalme wapya wa kombe hilo.
Yanga imefanikiwa kutwaa kombe hilo kwa kuwafunga wapinzani wao wakubwa Simba kwa bao 1-0 katika muda wa nyongeza, bao lililowekwa kimiani na mshambuliaji wao Kenneth Asamoah kutoka Ghana.
Mshambuliaji huyo kipenzi cha wanajangwani alizima ndoto za mabingwa hao wa kihistoria kuweka rekodi ya kutwaa kombe hilo kwa mara ya saba alipofunga bao kwa kichwa akiunganisha krosi nzuri ya kiungo mchezeshaji Rashid Gumbo.
Gumbo, mchezaji mwenye kipaji cha pekee cha kumiliki mpira aliingia akitokea benchi katikati ya kipindi cha kwanza kuchukua nafasi ya kiungo mkabaji Juma Seif aliyeumia, aliambaambaa na mpira kwenye wingi ya kushoto akiwatoka wachezaji Mohamedi Banka na Saidi Cholo na baadaye kutoa krosi murua iliyounganishwa kiufundi na mshambuliaji huyo wa zamani wa Fc Jagodina ya Serbia.
Mara ya mwisho Yanga kutwaa kombe hilo ilikuwa ni mwaka 1999 huko Kampala Uganda ilipoifunga Sports Club Villa ya nchini humo kwa mabao 4-5 kwa njia ya penati, ambapo matokeo katika muda wa dakika 90 yalikuwa ni 0-0 na hivyo kulazimu kwenda muda wa nyongeza.
Kwa ushindi huo Yanga imeandika historia mpya ya mashindano hayo, kwani ni kombe lake la nne ikiwa imewahi kutwaa kombe hilo kwenye miaka ya 1975 huko Zanzibar, mwaka 1993 na 1999 huko Kampala Uganda na mwaka huu katika ardhi ya nyumbani.
Katika michuano hii ya mwaka huu Tanzania iliwakilishwa na timu tatu ambapo ni mabingwa watetezi Simba kwa maana ya msimu uliopita, washindi wa pili Yanga na kwa upande wa Zanzibar walikilishwa na timu ngeni kabisa katika mashindano hayo, timu ya Ocean View.
Katika michuano hiyo ya wiki mbili hakukuwa na kipya sana kutoka kwa timu zetu kubwa za Simba na Yanga kwa maana ya ubora wa kiwango cha uwanjani na wachambuzi wa masuala ya soka wanasema kwamba uenyeji na uzoefu wa timu hizo katika mashindano hayo kwa kiwango kikubwa vilichangia timu hizo kufika hatua ya fainali.
Timu pekee kutoka Tanzania ambayo ilionyesha kiwango bora ni Ocean View ya Zanzibar ingawa uchanga wake katika michuano hiyo uliifanya itolewe katika hatua ya makundi, lakini ilicheza soka la kifundi na kitimu tofauti na Simba na Yanga.
Katika michuano hiyo ambapo Yanga na Simba zote zilikuwa katika kituo cha Dar es salaam kutokana na utashi wa Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati(CECAFA) na Shirikisho la Soka nchini, TFF zikiamini kuwa kuziweka kituo hicho kungetengeneza faida kubwa ya mapato kutokana na ukweli kwamba mkoa huo maarufu nchini ndio wenye washabiki wengi wa soka wa Simba na Yanga na wenye vipato vya kuingia mpirani.
Katika kituo hiki cha Dar es salaam Simba ilipangwa kundi A ikiwa na timu za Vitalo ya Burundi, Ocean View ya Zanzibar na Etincelles ya Rwanda.Simba ndio ilikuwa ya kwanza katika kundi hili ambalo halikuwa gumu, ingawa ilipata wakati mgumu ilipocheza na Vitalo na Red Sea kwani haikuweza kupata bao hata moja.
Yanga ndio ilikuwa kundi la kifo, kundi B lililokuwa na timu za El Merreikh ya Sudan, Bunamwaya ya Uganda na Elmani ya Somalia. Merreikh ndio ilionekana kama timu tajiri kwa kuwa wachezaji wake wengi ghali, ilicheza soka la kuvutia na la ufundi wa hali ya juu, katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Yanga zilitoka sare ya mabao 2-2.
Bunamwaya iliundwa na wachezaji wengi chipukizi ilimaliza ikiwa ya tatu katika kundi hilo na kupata kucheza hatua ya robo fainali kama timu iliyoshindwa kwa taabu, “Best Loser” sambamba na Yanga vinara wa kundi hilo na Merreikh walioshika nafasi ya pili.
Elman timu kutoka Somalia kama kawaida yake ingawa angalau ilijitahidi katika mashindano ya mwaka huu, hasa katika mchezo wao dhidi ya Yanga ambapo iliwabidi mpaka dakika za lala salama kuweza kupata mabao, katika ushindi wake wa mabao 2-0 dhidi ya timu hiyo.
Kituo cha Morogoro kilikuwa na timu za St.George, Ulinzi ya Kenya na APR ya Rwanda ambayo ndio ilikuwa bingwa mtetezi wa mashindano hayo na Ports ya Djibout.Lilikuwa kundi gumu kwa maana timu zote hizo zilikuwa na ubora wa hali ya juu ukiachilia mbali Ports ambayo ndio ilikuwa kapo la magoli.Wachunguzi wa mambo wanaamini hili ndilo lilikuwa kundi lenye timu ngumu na St George ndiyo ilikuwa timu bora kwa maana ya soka la kiufundi.
Katika hatua ya robo fainali Simba iliifunga timu ngumu ya Bunamwaya kwa mabao 2-1,Yanga ikaifunga Red Sea kwa penati 4-3,El Merreikh ikiitoa Ulinzi Kenya kwa penati na St George ikaifunga timu ya Vitalo ya Burundi na kutinga hatua ya nusu fainali.
Mpaka zinaingia fainali Simba na Yanga zote hazikuonyesha kandanda la kuvutia zaidi ya kucheza kwa uwezo wa mchezaji mmoja mmoja na kwa shinikizo la mashabiki wao zaidi kuliko muunganiko wao kama timu.
Makocha wa timu hizi mbili, Sam Timbe wa Yanga na Mosses Bassena wa Simba hakuna hata mmoja kati yao aliyewahi kukiri kuwa timu zao zilicheza vizuri zaidi ya kufurahia matokeo na kusema kwamba wanayatumia mashindano haya katika kutengeneza timu zao kwa ajili ya michuano kimataifa kama vile klabu bingwa Afrika na kombe la shirikisho.
Ukiachilia mbali ukweli wa kwamba timu zote hazikupata muda mzuri wa maandalizi kutokana na kwamba ndio ligi ilikuwa imekwisha na wachezaji kuwa mapumzikoni, kuchelewa kupatikana kwa mdhamini wa kuandaa mashindano hayo, kuliathiri kwa namna moja au nyingine maandalizi ya timu hizi, lakini kuna kitu kimejificha ndani ya timu hizo.
Hakika timu hizi zinaundwa na wachezaji wengi wapya kila msimu kitu ambacho hata zipewe muda gani, bado itakuwa ngumu kuweza kuwaunganisha, wakazoeana na kucheza pamoja kama timu, achilia mbali mabadiliko ya mara kwa mara ya makocha.
Uthibitisho ni vikosi vya timu hizo vilivyoshiriki mashindano haya vilikuwa na sura nyingi mpya kuliko zilivyokuwa msimu uliopita.
Wachezaji Rashidi Gumbo,Julius Mrope,Oscar Joshua, Kenneth Asamoah, Hamisi Kiiza, Godfrey Taita waliocheza karibu mechi zote za Yanga ni wapya na hivyo kufanya washindwe kuzoeana na kuleta radha ya soka safi.
Kadhalika wachezaji kama Dereck Walulya, Patrick Mafisango, Saidi Chollo, Haruna Moshi,Ulimboka Mwakingwe, Athumani Idd, Isihaka Rajabu na Mwinyi Kazimoto ni wageni katika kikosi cha Simba cha mwaka huu.
Hao wote ni wachezaji wanaoonekana kuwa ni wenye vipaji vya hali ya juu, lakini vipaji vyao havikuweza sana kuleta kandanda safi zaidi ya kila mmoja kuonyesha uwezo binafsi na sio muunganiko wao kama timu.
Mbali na kushindwa kuunganika kama timu lakini pia walionekana katika muda mwingi wa mashindano hasa mechi zilizokwenda mpaka muda wa nyongeza kukosa stamina na kuchoka haraka hali iliyotoa picha halisi ya kukosa mazoezi ya kutosha kama timu.
Kadhalika hakukuwa na ubunifu kwa wachezaji hao zaidi ya mashabiki wao kuucheza mpira kuliko wao wenyewe, kwa maana shinikizo la kelele pindi wachezaji hao wanapopata mpira, hawaachwi huru kufanya maamuzi binafsi.
Washabiki wakimwambia mchezaji fulani piga, naye hufanya hivyo muda huo huo, kitu kinachothibitisha kwamba ni mashabiki wanaoucheza mchezo kuliko wachezaji wenyewe na hii hufanya washindwe kuwa wabunifu na mwisho wa siku kushindwa kuonyesha uwezo wao na kuharibu radha nzima ya soka.
Ungependa kuangalia jinsi timu kama za El Merreikh, St. George au Bunamwaya zilivyokuwa zikicheza, zilicheza kitimu, kwa malengo kulingana na staili ya timu wanayokutana nayo, hali inayoonyesha kuwa walikuwa pamoja kama timu kwa muda mrefu.
Kwa kawaida ya mashindano mara nyingi vipaji vipya huweza kuvumbuliwa kupitia mashindano ambayo timu zao zinacheza, kwa mfano katika fainali za kombe la dunia zilizofanyika Ufaransa mwaka 1998 mchezaji Michael Owen aliweza kuvumbuliwa hasa alipofunga bao safi la ushindi katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Argentina, Owen alikuwa na miaka 17 kipindi hicho.
Cha kusikitisha katika michuano ya mwaka huu ya kombe la Kagame ukiangalia ushiriki wa timu zetu hasa Simba na Yanga, hakuna chipukizi hata mmoja aliyepewa nafasi ya kuonyesha uwezo wake, sura nyingi zilizong,ara ni zile zile.
Hakuna jipya kwa wachezaji kama Haruna Moshi, Ulimboka Mwakingwe, Mohamedi Banka wa Simba wala Oscar Joshua, Juma Seif, Julius Mrope, Rashidi Gumbo, Nurdin Bakari kutoka Yanga kwani ni wachezaji ambao tayari uwezo wao unajulikana.
Yale yale kwa timu zetu kwa timu hizi kuendelea na tabia zao za kushindwa kuwa na sera nzuri za kuendeleza wachezaji chipukizi, zaidi ya kutaka ambao tayari wameshavumbuliwa.
Chipukizi kama Salum Telela, Omega Seme,David Luhende,Abuu Ubwa kutoka Yanga ambao wapo katika timu ya taifa ya chini ya miaka 23 majina yao hayakuorodheshwa katika wachezaji walioshiriki michuano hii, nini kukaa benchi.
Kadhalika Shomari Kapombe na Kelvin Chale kutoka Simba ambao nao wako katika timu ya taifa chini ya miaka 23 nao hawakupata nafasi ya kushiriki mashindano haya, kwani kama wenzao wa Yanga nao majina yao hayakuorodhezeshwa kwa ajili ya michuano hii.
Kinachoonekana hapa ni muendelezo wa tabia za wanachama, viongozi na makocha wa timu hizi kutaka matokeo na sifa binafsi zaidi na sio kuendeleza mchezo wenyewe wa soka kwa manufaa ya taifa letu, kwa maana ya kuja kuwa na timu ya taifa imara kwa siku za usoni.
Cha kufanyika ni kusajili kwa umakini mkubwa na kuhakikisha timu hazibadiliki badiliki kila inapofika mwisho wa msimu, mashabiki kuacha wachezaji huru waonyeshe uwezo wao uwanjani, muda mzuri wa maandalizi ikiwemo suala la kupatikana kwa mdhamini wa mashindano mapema na ziweke sera zitakazotoa nafasi kwa wachezaji chipukizi kuonekana.
Comments
Loading…