in , , ,

NILICHOKIONA KWENYE MECHI YA SIMBA NA YANGA JANA.

*Simba 2-Yanga-1*

Sehemu pekee ambayo ilianza kuonesha mwanga kwa ushindi wa Simba ni
baada ya Kamusoko kuumia na kutolewa.

Kuingia kwa Said Juma Makapu kulifanya Yanga iwe na viungo wa aina
moja kiuchezaji ( yani Saidi Juma Makapu na Justine Zullu) wote ni
viungo ambao kiuhalisia wanakaba .

Inawezekana wazo la Lwandamina lilikuwa zuri la kumwingiza Said Juma
Makapu kwa sababu ya kulinda goli alilokuwa amelipata .

Lakini vitu viwili vilikuja kuharibu, cha kwanza ni kwamba Zullu na
Makapu ni aina ya viungo ambao hawana uwezo mkubwa wa kukaa na mpira
pamoja na kupiga pasi nyingi kwenye timu.

Wachezaji wa yanga, wakifurahia goli lao.

Baada ya ingizo lao, tulishuhudia kina Msuva, Chirwa wakipata mipira
michache sana kwa sababu hakukuwepo na mtu mzuri wa kuwahudumia .

Kitu cha pili ambacho kilikuja kuharibu ni kwamba Simba walikuwa na
viungo ambao kiuhalisia walikuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira,
kukaba na kupiga pasi kwa washambuliaji wao.

Hali iliyofanya Simba kuwa na mpira muda nwingi na Yanga kutokuwa na
mpira muda mrefu .

Kelvin na Dante ilijihidhirisha tokea kombe la Mapinduzi kuwa ni watu
ambao hawawezi kucheza katika kiwango bora wakiwa pamoja.

Jana ,Dante alikosa mtu wa kumuongoza.Kelvin siyo kiranja mzuri sana
na ni ngumu Dante kucheza vizuri bila ya kiranja mzuri.

Pili, wote wawili siyo bora kwa kucheza mipira ya juu. Ukiachana na
hawa wawili kutokuwa bora kwa jana wakiwa pamoja ,pia Haji Mwinyi jana
alicheza katika kiwango cha Chini sana.Hata magoli yote mawili
yalipitia upande wake.Marking yake ilikuwa mbovu sana kwa jana.

Kuna uwezekano Chirwa alikuwa anatusikiliza tu tulivyokuwa tunamzomea,
kitu kizuri kwake ni kwamba amebadilisha zile kelele tulizokuwa
tunamzomea na kuwa wimbo mzuri.

umati wa wapenzi wa yanga, ukifuatilia mchezo huo

Kama ilivyokuwa kwa Chirwa ndivyo ilivyokuwa kwa Mavugo.Kipindi
alichopitia Chirwa ndicho hicho hicho alichopitia Mavugo.

Lakini kwa pamoja wameanza kutuaminisha tofauti na tulivyokuwa tunawafikiria.

Pamoja na kwamba Simba walipata ushindi, lakini jana Lufunga na Banda
hawakucheza vizuri na kwa kuelewana vizuri.

Pia kulikuwa na mawasiliano hafifu sana kati ya Kipa wa Simba na
Mabeki wake wa kati ,kiasi kwamba kama Yanga wangewa presha zaidi
Simba kwa mashambulizi kulikuwa na uwezekano mkubwa kupata goli
kutokana na uhafifu wa mawasiliano kati ya kipa wa Simba na Mabeki
wake wa kati.

Ubora wa Simba kwa jana ulikuwa pale kati, hata kabla ya kuingia Mkude
,Kotei alikuwa mzuri zaidi kwenye kukaba, aliporudishwa kucheza kama
beki wa kati, Mkude alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuicommand timu.

Ndemla akafanya kazi nzuri sana ya kuichezesha timu .Alihakikisha timu
ikiwa na mipira muda mwingi mwa mchezo.

Kasi ya Ajib ilikuwa na work rate kubwa na nzuri sana kwenye mechi ya
jana ,na key passes nyingi zilikuwa zinatoka kwake.

Heka heka uwanjani…

Kichuya alikuja kuongeza kasi na ubunifu mkubwa sana baada ya
kuingia.Krosi yake iliyosababisha goli, na goli lake lilikuwa na
msaada mkubwa sana.

Inawezekana Mzamiru asiimbwe sana katika mchezo wa jana .Ila jana
kafanya kazi kubwa sana.

Kwa mchezo wa jana kacheza katika majukumu manne. Jukumu la kwanza ni
la box to box middfielder, jukumu la pili ni la Central Attacking
Middfielder, jukumu la tatu alicheza kama winger na jukumu la nne
alicheza kama beki wa kulia.Na kila jukumu alilokuwa anapelekwa
kucheza alijitahidi kwa kiasi kikubwa kutimiza ipasavyo majukumu yake.

MabadiliKo ya mwalimu Joseph Omog yalikuwa yanafaida sana kwa upande wa Simba.

Pia Omog alifanikiwa kwa kiasi kikubwa katika maeneo yafuatayo baada
ya ile kadi nyekundu ya Busungu.

Moja, Aliwafanya wachezaji kutoka nje ya mchezo baada ya ile kadi
nyekundu, mbili alifanikiwa kwa kiasi kikubwa timu iongeze hali ya
kupigana baada ya ile kadi nyekundu.

Kitu kikubwa baada ya ile kadi nyekundu.Simba walihakikisha Yanga
wasiweze kumiliki mpira, waliwanyima uhuru wa wao kumiliki mpira na
kila walipokuwa wanajaribu kumiliki mpira Simba walikuwa wanawakaba
hali iliyowafanya Yanga wasiwe na uwezo wa kumiliki mpira hata kwa
sekunde 20. Na kila Simba walivyokuwa wanawapokonya Yanga mipira
walikuwa wanaanzisha mashambulizi haraka haraka.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

MAENEO KUMI MUHIMU KATIKA MECHI LEO YA SIMBA NA YANGA

Tanzania Sports

Man U wanachekelea