Kuna kitu kimoja ambacho eneo la kiungo cha Simba walikuwa wanakikosa
zamani ila kwa sasa kimepatikana Kupitia Kotei.
Kipindi ambacho Mkunde anacheza eneo la kiungo cha kuzuia alikuwa
anashindwa kuleta ugumu eneo la kiungo cha Simba.
Lakini kwa mechi hii kuna mfupa umejengeka eneo la kiungo cha Simba
kwa sababu ya Kotei.
Kwenye mechi hii, Kotei na Mkude kwa asilimia kubwa hasa hasa kipindi
cha kwanza walipewa jukumu la kufanya ugumu zaidi eneo la katikati mwa
uwanja. Jukumu la kujilinda kwao lilikuwa kubwa zaidi kuliko jukumu la
kushambulia.
Na hii ndiyo ilikuwa approach kubwa ya timu zote mbili. Timu zote
kipindi cha kwanza ziliingia zikiwa na tahadhari zaidi ya kujilinda na
kushambulia kwa kushtukiza.
Hatukuona nafasi nyingi zikitengenezwa pande zote mbili kwa kipindi cha kwanza.
Kitu pekee ambacho Simba walikitegemea ni wao kutaka kupitia pembeni
ndiyo maana wakamweka Mzamiru na Kichuya pembeni huku Mohamed Ibrahim
akicheza kama false 10.
Hii ilikuwa na maana kubwa sana kwa Simba kwa sababu Mohamed Ibrahim
kwa kiasi kikubwa anaweza kutoa huduma zifuatazo .
Kwanza huduma ya kusambaza mipira pembeni mwa uwanja na kwa
mshambuliaji wa kati.
Pili Mohamed Ibrahim anauwezo wa kufunga hasa hasa anapocheza eneo
ambalo yuko nyuma ya mshambuliaji.
Sasa kitu ambacho kilikuja kuharibu mpango huu ni hiki hapa.
Yanga wakimweka Said Juma pamoja na Kamusoko na wote wakapewa jukumu
moja na kuzuia zaidi.
Kwa kipindi cha Kwanza Kamusoko hakujihusisha kwa asilimia kubwa
kwenye jukumu la kushambulia ingawa anauwezo mkubwa kwenye jukumu
hilo.
Muda mwingi mwa kipindi cha Kwanza Walikaa nyuma, na hii ikamnyima
Uhuru mkubwa Mohamed Ibrahim wa kutimiza majukumu yake.
Ndiyo maana kwa kiasi kikubwa Kichuya na Mzamiru ambao Walikuwa
wanatokea pembeni wakipata mipira michache sana.
Kuna kitu kimoja kwa Mzamiru, kwenye mchezo huu kitu pekee
kilichomkaba ni nafasi ambayo alikuwa jana.
Mzamiru siku zote huwa anaonekana bora zaidi pindi anapocheza kama Box
to box Midfielder. Nafasi hii inampa uhuru sana wa kutokuwepo eneo
moja. Mzamiru ni aina ya wachezaji ambao hucheza kwa furaha na
kujiachia kama wakicheza eneo ambalo watakuwa uhuru kutembea eneo
lolote la uwanja.
Yanga kwa kiasi kikubwa waliingia kwa ajili ya kujilinda na kucheza
direct football ( yani mpira wa moja kwa moja).
Na hii inatokana na matokeo ya mechi iliyopita ambapo walicheza sana
open football ( mchezo wa wazi).
Hawakuingia na mpango huo tena, walichokifanya ni kucheza mipira mirefu.
Kitu pekee ambacho kilisababisha mbinu hii kutofanikiwa ni kwa sababu,
ili Yanga iweze kuwa hai kwenye eneo la kushambulia lazima eneo la
pembeni liwe hai.
Bukungu na Mohamed Hussein kwa kiasi kikubwa walifanikiwa kuwafanya
Kaseke na Msuva wasipate uhuru wa kucheza.
Mfano, kwa kiasi kikubwa Bukungu hakuwa akipanda zaidi mbele
kushambulia , hii ilimpa uhuru mdogo Msuva kulazimisha mashambulizi.
Kitu kingine, Timu ya Yanga inapocheza mipira ya juu na mipira mirefu
ya moja kwa moja tegemea huduma ya mtu kama Niyonzima kutokuwa nzuri
ukilinganisha na kama Yanga ikiweka mpira chini.
Unapokosa huduma ya Niyonzima moja kwa moja unakuwa umekosa ubunifu wa
pasi za mwisho kwa mshambuliaji wa mwisho.
Ndiyo maana kwa kiasi kikubwa mipira ambayo alikuwa akiipata Tambwe
ilikuwa inakuja katika eneo ambalo ni ngumu kwake kufanya maamuzi (
alikuwa akipata mipira isiyokuwa na madhara).
Kuna kitu ambacho mabeki wa Yanga wanatakiwa wawe makini nacho kwa
kiasi kikubwa.
Nacho ni wao kujipanga wakati timu inashambuliwa kwa kushtukizwa.
Nakupa mfano, kuna shambulizi moja la kushtukiza ambalo lilitokea
eneo la kulia mwa Yanga. Juma Abdul alikuwa amepanda kushambulia.
Yondani alikimbia kucover eneo lake, lakini Juma aliporudi alikimbia
kwenda eneo alipo Yondani badala ya kwenda eneo aliloacha wazi
Yondani.
Kuna kitu kikubwa sana kwa Said Juma anatakiwa kujifunza kutoka kwa Mkude.
Yeye ndiye anayetengeza ni njia ipi ya kupitishia mipira kwenye timu.
Au ni aina gani ya mchezo muda huu timu inatakiwa icheze.
Ili uweze kufanya hivyo unatakiwa uwe na uwezo mkubwa wa kupiga pasi
ili kusukuma timu yako. Lakini hiki Said Juma anakosa ingawa ni Mzuri
sana kwa kukaba.
Martin Kiyumbi