Mabingwa watetezi wa Afrika, Nigeria wameshindwa kufuzu kwa michuano ya Klabu Bingwa Afrika (AFCON), hivyo kutema ubingwa rasmi.
Nigeria imeshindwa kufuzu katika kundi ‘A’ ilikokuwa, hivyo itayasikia tu mashindano hayo yaliyopangwa kufanyika nchini Guinea ya Ikweta baada ya Morocco waliokuwa waandae kutofautiana na Shirikisho la Soka la Africa (Caf) juu ya masuala ya Ebola.
Katika mechi ya mwisho iliyofanyika Jumatano hii, Nigeria walibaniwa na Afrika Kusini mjini Uyo, wakaenda sare ya 2-2 hivyo kumaliza michuano nje ya nafasi mbili za juu kwa kundi lao.
Wangeweza kutarajia kupata nafasi ya timu bora zaidi katika nafasi za tatu lakini pia napo wameangukia pua, kwa sababu wana pointi nane tu. Afrika Kusini wamewakata maini Nigeria maana tayari walishafuzu kabla ya mechi hiyo, kwa mashindano yatakayofanyika kuanzia Januari 17 hadi Februari 8 mwakani.
nchi nyingine zilizofuzu kwa mashindano hayo makubwa Afrika ni Algeria, Burkina Faso, Cameroon, Cape Verde, Kongo Brazzaville, Kongo Kinshasa, Guinea ya Ikweta kwa nafasi ya wenyeji, Gabon, Ghana, Guinea, Ivory Coast, Mali, Senegal, Tunisia na Zambia waliofiwa na Rais Michael Satta majuzi.
Comments
Loading…