Yanga nao wanasema haiwezekani washindwe kuifunga timu ambayo imepata kibahati nafasi ya tatu. Kwa ufupi timu zote zinatumia neno hili ‘haiwezekani”.
Maskani ya Simba na Yanga ni Dar es Salaam, lakini zilikimbilia Zanzibar. Simba ilibana Unguja Yanga ikapanda mpaka Pemba.
Zimejigamba na kujisifu vya kutosha lakini leo Jumamosi ni ukweli utajulikana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba haina nafasi ya kushiriki michuano mikubwa mwakani, lakini ina uhakika wa Sh. 25 milioni kama zawadi ya mshindi wa tatu wa ligi na inaikabili Yanga leo Jumamosi jioni kwenye Uwanja wa Taifa kulinda heshima na kukamilisha msimu.
Yanga tayari ni mabingwa na wana uhakika wa Sh.70 milioni za mshindi wa kwanza.
Simba na Yanga zilirejea jana Ijumaa Dar es Salaam zikitokea Zanzibar zilipokuwa zimepiga kambi wakati Yanga ilikuwa Pemba, watani wao Simba walikuwa Unguja.
Kocha wa Simba, Patrick Liewig amesisitiza kwamba timu yake ina morali na wachezaji wake vijana wametulia kisaikolojia tayari kuikabili Yanga ambayo bosi wake Ernest Brandts amesema watafanya vitendo uwanjani.
Itaingiza kikosi kitakachoundwa na mabeki; Nasor Said ‘Chollo’, Haruna Shamte, Mussa Mude na Shomari Kapombe kumlinda Abeil Dhaira.
Katika kiungo watacheza; Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto,William Lucian na Haruna Chanongo,wakati kwenye ushambuliaji watasimama Mrisho Ngassa na Felix Sunzu.
Katika benchi lao watajaza vijana wengi kama Christopher Edward, Ramadhani Singano, Miraji Adam, Abdallah Seseme, na Hassan Khatib.
Comments
Loading…