* Nimeshaingia studio za BBC London, kukuchambulia mchezo huu wa ufunguzi. Kupitia Idhaa ya kiswahili ya BBC na radio washirika.
SIJASOMA kwa kina historia ya mipira inayotumika kwenye fainali za kombe la dunia inapewa vipi majina kulingana na utamaduni. Kama nikisema nielezee chanzo cha majina ya mipra hiyo, bila shaka itachukua mada nzima.
Kila mwaka wa fainali za kombe la dunia kunakuwa na majina ya mpira inayotumika. Afrika Kusini ilikuwa mwenyeji wa fainali za mwaka 2010 na mipira ikapewa jina la Jabulani.
Mipira ililalamikia kidogo, lakini bingwa akapatikana. Mwaka huu kuna mipira ya Brazuca, huku wenyeji Brazil wakiwa na matumaini ya kutwaa ubingwa huo.
Kocha Luis Felipe Scolari amekariri kuwa Brazil na Argentina zitacheza fainali ya mwaka. Scolari anaonekana kuzibeza timu za ulaya, lakini wengine wanazipa nafasi Hispania, Ujerumani, England na Italia kufanya vizuri.
Leo pambano la ufunguzi linaanza mjini Sao Paulo. Brazil watakuwa na kibarua mbele ya Croatia ambayo imekuwa timu inayokwenda kimya kimya. Kwamba Croatia haizungumzwi sana kama wenyeji Brazil.
Wengi wanachukulia kama Brazil imeshinda mchezo huo. Katika mechi hii kuna kazi ya kufanywa na Brazil. Kwanza ni kuhakikisha Luka Modric hachezi wka uhuru kama anavyofanya akiwa Real Madrid.
Pili kuhakikisha Ivan Rakitic hapati uhuru kama ule anaofanya pale Sevilla. Kama mpenzi wa soka alitazama mechi ya nusu fainali ya Europa, kati ya Sevilla na Valencia, ataelewa ninachozungumzia.
Kwamba kosa kubwa walilofanya Valencia lilikuwa kuamini wamefuzu, kisha wakaruhusu kiungo huyo apandishe zaidi timu yake dakika za mwisho, kabla ya bao la kichwa la Stephane Mbia kutibua ndoto zao.
Mbia asingefunga bao lile kama Ivan Rakitic kuongeza maarifa kwenda mbele na kusababisha faulo. Kocha Niko Kovac anategemea sana uhodari wa wawili hawa kuibuka na ushindi.
Lakini ushindi huo utachangiwa na umakini wa washambuliaji wao wawili, Ivica Olic anaekipiga Wolfsburg, na Eduardo anayeichezea Shakhtar Donetsk. Pia yupo Nikica Jelavic aliyeko Hull City pamoja na Ante Rebic wa Fiorentina.
Kwa hakika kocha wa Croatia anaweza kuibuka na ushindi ikiwa atachanganya uhodari wa Olic na Eduardo, huku Rebic na Jelavic wakiwa ‘sub’ za maana. Kwakuwa anapendelea mfumo wa 4-3-2-1, nadhani atahitaji mtiririko ambao utakuwa unaingia ndani ya boksi moja kwa moja. Kocha NiKo Kovac akihitaji mpango wa pili, basi atalazimika kumtegemea Nikica Jelavic ambaye anaweza zaidi kupambana na mabeki kuliko Olic mwenye kucheza kwa kasi na kuwapunguza mabeki. Jelevic anahitaji nafasi chache sana kufunga mabao.
Kwa upande wa Scolari hana kazi kubwa kuwapanga vijana wake. Scolari ameshaeleza kuwa Oscar dos Santos ataanza badala ya Willian. Anachotaka Scolari kwa Oscar ni rahisi sana, mchezaji wa pili ambaye atakwua karibu zaidi na nyota wake Neymar da Silva.
Wakati Neymar akitokea upande wa kushoto, atahitaji mchezaji wa pili ambaye atakuwa nje ya eneo la 18 akisubiri pasi zake, ama atoe pasi ili mshambuliaji huyo wa Barcelona aelekee kucheka na nyavu.
Oscar ni mjanja kucheza kitimu, na ana vitu vya ziada ndiyo maana Philipe Coutinho ameachwa. Hulk atakuwa na kazi kutokea kulia kuingia eneo la hatari, lakini mbadala wa Oscar na Hulk ni Willian.
Kwamba Willian anatakiwa kuingia kubadilisha matokeo, iwapo timu inakuwa haijafunga bao ama imefungwa. Jo anaweza kuwa mbadala wa mbinu za kufunga mabao kwa krosi, lakini Willian ni mzuri kulinda lango, na ataingia kucheza kwa mtindo uleule nyuma ya washambuliaji.
Katika eneo la nyuma ya washambuliaji, Scolari anapanga viungo watatu au wawili ili kumzunguka Fred na kupa mwanya wa kufunga. Eneo la kiungo sidhani kama litabadilika, kwamba Luis Gustavo na Paulinho wataongoza jahazi.
Kuna ktu kimoja, Brazil iliyocheza na Hispania fainali ya Kombe la Mabara, ndiyo ninayotarajia kuiona kwenye michuano hii. Na mechi yao ya leo roho za mashabiki wa timu zote mbili zimebebwa na Neymar kwa Brazil na Luka Modric kwa Croatia.
Comments
Loading…