in , , ,

Newcastle, Norwich washuka daraja

Sasa ni rasmi, Newcastle na Norwich wameshushwa daraja kutoka Ligi Kuu
ya England (EPL) hadi Championships ambayo ni sawa na Ligi Daraja la
Kwanza.

Hayo yamebainika usiku wa Jumatano baada ya Sunderland waliokuwa juu
yao kidogo kupata ushindi mnono dhidi ya Everton na kufikisha pointi
38, wakijiweka salama katika nafasi ya 17, idadi ya pointi ambazo
Newcastle na Norwich hawawezi kufikia.

Wengine ambao walishashuka daraja kitambo ni Aston Villa ambao
wamekuwa mkiani kwa muda mrefu licha ya kubadili makocha. Villa wana
pointi 17 kutokana na mechi 37, Norwich wanazo 34 sawa na Newcastle,
wakifungana pia kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Norwich walijitutumua na kufanikiwa kuwafunga Watford 4-2, lakini
hawakuwa na uwezo wa kuamua hatima yao wenyewe, bali kutegemea
Sunderland wafungwe hiyo jana na pia kwenye mechi ya mwisho wa ligi
Jumapili hii na pia kuomba Newcastle wafungwe, lakini sasa hatima yao
ni kushuka daraja.

Sunderland waliowachoma Everton 3-0 kwenye mechi hiyo, wamekuwa katika
EPL kwa miaka 10 mfululizo, mara kadhaa wakinusurika kushuka daraja,
ikiwa ni pamoja na msimu uliopita walipookoka mwishoni wakiwa na kocha
Dick Advocaat.

Norwich city......
Norwich city……

Walikuwa kwenye eneo la kushuka daraja kwa siku 237 msimu huu wakati
hadi mwisho wa msimu Villa watakuwa wamedumu kwenye eneo hilo hatari
kwa siku 233. Sunderland walitaja kikosi kile kile cha wachezaji 11 wa
mwanzo katika mechi saba mfululizo, na kuokoka kwao kunachukuliwa
kwamba ni kutokana na mchango mkubwa wa kocha Sam Allerdyce
aliyechukua timu wakiwa pabaya.

Mabao ya jana yalifungwa na mabeki Lamine Kone na Patrick van Aanholt
ambao pamoja na kusaidia mashambulizi tangu mwanzo wakipanda na
kushuka, walikuwa imara kwenye ngome kuhakikisha hawafungwi, ili ndoto
za kubaki EPL ziwe kweli.

Kufungwa 3-0 kwa Everton kwa mara ya pili mfululizo kunakowaacha
katika nafasi ya 12 kunazidi kumweka pabaya kocha wao, Roberto
Martinez ambaye washabiki wameshaanza kutaka afutwe kazi, hivyo kwenye
mechi ya mwisho nyumbani Goodison Park atakuwa na wakati mgumu dhidi
ya Norwich, awe tayari kuzomewa.

Katika mechi nyingine Jumatano hii, Liverpool walikwenda sare ya 1-1
na Chelsea na kuweka ndoto za Liverpool hai kwa ajili ya kuwa kwenye
sita bora ili mwakani washiriki Ligi ya Europa. Mwaka huu wameingia
fainali. Mabao yalifungwa na Eden Hazard kwa Chelsea dakika ya 32 na
Christian Benteke saa moja baadaye.

Liverpool sasa wamefikisha pointi 59 wakiwa kwenye nafasi ya nane
baada ya timu zote 20 kucheza mechi 37, zikibakisha moja Jumapili
wanapokwenda kufunga pazia la msimu wa 2015/16.

Wanazidiwa kwa pointi moja na Southampton wakati West Ham wanazo 62 na
Manchester United wamefikisha 63. Mabingwa Leicester wana pointi 80,
zikiwa ni 10 zaidi ya Tottenham Hotspur huku Arsenal wakizidiwa na
mahasimu wao wa London Kaskazini kwa pointi mbili na Manchester City
wakiwa na pointi 65.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Man United hoi

Tanzania Sports

PAZIA LA EPL KUFUNGWA: