Mwanariadha Nasria Hashir wa Mjini Magharibi Zanzibar akiruki viunzi vya mita 110 wakati wa mashindano ya riadha ya taifa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana.Pichan na Jackson Odoyo.
MIKOA ya Singida, Arusha, Mbeya na Manyara imeanza kwa kishindo kwenye mbio za mita 1500 na hata 800 na 400 katika michuano ya riadha ya Taifa wenye lengo la kupata wanariadha watakaokilishi nchi kwenye Michezo ya Afrika.
Mashindano hayo yanayomalizika leo kwenye Uwanja wa Taifa yameonekana kukosa msisimko kutokana na kutokuwa na mashabiki wanaokwenda kuyatazama, idadi ndogo ya washiriki huku pia baadhi ya wachezaji wengi wakicheza bila vifaa hasa viatu na nguo za kukimbilia.
Katika mbio za mita 1500 kwa wanaume ambao watachuana katika fainali leo, Korinel Panga wa Arusha aliongoza baada ya kukimbia kwa kutumia dakika 3: 48: 12 akifuatiwa na Enock Benyamin wa Shinyanga aliyekimbia kwa muda wa dakika 3: 27:72.
Wengine ni Basil John wa Manyara 3:49: 37, Uwezo James ( Mbeya) 3:49:80, Juma Hiti( Unguja) 3:50:80, Emanuel Willium (Singida) 3:50:84, Pascal Ramadhan (Mbeya) 3: 51: 31, Paulo Goti( Kusini Pemba) 3: 53: 02, Fabian Nelson ( Manyara) 3:54:34, Mohamedy Iddi( Dar es Salaam) 3 : 54:85, Samwel Muyombo(Kagera) 4:03:38 Ndebile John (Mwanza) 4:04:15, Juma Kito (Singida) 4:04:17 na Ronaldo Sumwa ( Dar es Salaam) 4:26:21.
Kwa upande wa wanawake Anastazia Msandai wa Arusha aliongoza kwa kukimbia kwa muda wa dakika 4: 31:05 akifuatiwa na Siaja Romanus wa Morogoro aliyekimbia kwa dakika 4: 33: 45 akifuatiwa na Natalia Elisante wa Dar es Salaam aliekimbia dakika 4:33:94
Wengine ni Maria Sikalika( Mbeya) 4:36:30, Asha Salim (Singida) 04: 39:66, Zakia Abdallah 4: 39: 66, Sara Maja( Kilimanjaro) 4: 42: 78, Faudhia Shaban ( Singida) 4: 49: 47, Fanuna Mohamedy (Arusha) 4: 59:63, Warda Alei( Kusini Unguja) 5:22:41, Monica Charles( Simiyu) 5:24:59 na Sara Bahati wa Mbeya 5: 26: 04.
Leo kutakuwa na fainali za mita 800 kwa wanaume na wanawake, kutupa kisahaani, kurusha tufe, miruko mitatu na kupokezana vijiti.
Katibu msaidizi wa Chama cha Riadha mkoani Arusha, Michael Washa alilitaka Shirikisho la mchezo huo Tanzania (RT) kufanya maandalizi mapema ili kupata wadhamini watakaodhamini michuano hiyo ili iweze kufanyika kwa muda mrefu.
ìYaani hapa inaonekana mashindano hayakutangazwa, mashabiki hamna, wachezaji ni wachache na hiyo imetokana na RT kutoa nafasi chache kwa mikoa kuleta wachezaji, mfano sisi Arusha tuliambiwa tulete wachezaji 20 tu wakati mwaka jana tulikuja 30.1
Kingine RT wawe wanaanza maandalizi mapema kwani mimi sioni sababu ya kukurupuka wakati kalenda ya mashindano inajulikana, watafute wadhamini ili mashindano yafanyike kwa siku nyingi, kwani siku mbili hazitoshi zinawachosha wachezaji,î alisema Washa
Comments
Loading…