in

Mwanariadha alalamikia polisi kwa ubaguzi wa rangi

Bianca Williams

Mwanariadha wa Uingereza aliyekamatwa na mwenza wake kwa kutolewa kwenye gari na kufungwa pingu, amesema amefanyiwa hivyo kwa sababu ya rangi yake nyeusi.

Mwanariadha huyo, Bianca Williams anasema haikuwa sahihi kukamatwa na kufungwa pingu huku mwanawe mvulana akiachwa kwenye gari wakati wakirudi nyumbani kwao magharibi mwa London hivi karibuni.

Williams (26) anashikilia rekodi ya kuwa mwanamama wa tano kwa kukimbia kasi zaidi kwenye mbio za kilometa 200, alikuwa na mwenza wake, Ricardo dos Santos. Anasema ameachwa na uzoefu wa uchungu kwamba kuwa mweusi ni sawa na jinai. wanaishi Maida Vale, London.

Ushughulikiaji wa suala hilo na maofisa polisi umezua zogo kubwa, polisi wakidaiwa kwamba ni wabaguzi wakubwa. Klip ya wenza hao wakikamatwa ilirushwa kwenye mitandao ya jamii, Williams akionekana wazi kuwa na msongo wa mawazo, akisikika akiwalalamikia polisi na kusema akirudia rudia; “mwanangu yuko ndani ya gari.”

Kiongozi wa Chama cha Upinzani cha Labour, Keir Starmer aliyepata kuwa mkurugenzi wa mashitaka, alisema hakuona uhalali wa kutumia pingu kwenye tukio hilo. Williams alisema alihisi kwamba lazima alisemee suala hilo, ikitiliwa maanani tawasifu yake, kwamba kwa wasiojulikana kabisa watadhalilishwa kupita kiasi.

“Kuna haja ya hatua kuchukuliwa. Ikiwa si mimi ninayetakiwa kulisemea na kupaza sauti nani tena atafanya hivyo? Hili hutokea dhidi ya wanaume wengi weusi katika Uingereza na si kila mmoja yupo katika hali ya kuweza kusimama na kupaza sauti.

“Nilifikiri kwamba ni muhimu nilisemee hili, basi watu huko nje ni muhimu kujua kipi kinatokea hata kwa watu wanaowakilisha nchi hii. Yaweza kutokea kwa yeyote, yaweza kutokea kwa kaka yang una hata kwa mtoto wangu akishakuwa mkubwa. Nitamfundisha juu ya haya atakapokuwa ameweza kwenda shuleni peke yake au kwenda out na rafiki zake. Lazima kuwa makini kwa sababu kuwa mweusi sasa inaonekana kana kwamba ni jinai,” analalamika Williams.

Polisi wa Jiji la London wanadai kwamba kusimamishwa kwa Williams na mwenza wake na mwana mchana was aa sab ana ushee kulitokana na doria ya kawaida ya askari wanaolenga kudhibiti vurugu zilizoongezeka kwenye maeneo husika na kwamba askari wao hawajahusika na mwenendo mbaya kazini.

Wakasema kwamba gari hiyo ilikuwa na vioo vyeusi na namna lilivyokuwa linaendeshwa liliacha shaka kubwa, ikiwa ni pamoja na kuendeshwa kwenye upande usiotakiwa wa barabara na kuongeza kasi kubwa kabla ya kusimama kwa hiari. Kwamba baada ya kutopata chochote kibaya kwao au ndani ya gari, wahusika waliachiwa.

Williams anasema taarifa hiyo ya polisi imemchanganya, akidai kwamba gari haikuwa upande usiotakiwa kwani liliacha eneo pana vya kutosha kwa gari nyingine kupita. Anasema vioo vya nyuma kuwa wazi si kinyume cha sharia na kwamba lilikuja hivyo hivyo kutoka Mercedes.

Akasema kwamba Dos Santos (25) raia wa Ureno anayeshikilia rekodi ya kukimbia kasi zaidi kwa umbali wa mita 400, alipata kusimamishwa na polisi mara kadhaa kabla na kwamba anachukulia ni kawaida na tendo la asili kwa sababu humtokea kila mara, hali anayosema inasikitisha.

Kwamba walipofungwa pingu wote wawili siku hiyo, Dos Santos alisema; “karibu ulimwenguni mwangu,” kitu anachosema kinamuumiza na haikutakiwa kuwa hivyo au kuchukulia ni kawaida, kwani watu weusi watazidi kuumizwa kwa ubaguzi usiokuwa na sababu halali.

Williams anasema wasiwasi wake wa awali ulikuwa juu ya mwenza wake aliyekuwa akiendesha gari, lakini kisha kwa mvulana wao wa miezi mitatu, Zuri-Li. 

“Moyo wangu ulizama tu na nilitaka kumsaidia Dos Santos na walipoanza kunizonga kunikamata nikawaza; Mungu wangu, sijafanya chochote kibaya, lakini mwanangu yuko kwenye gari, siwezi kuja, mwanangu yuko kwenye gari,” anasema.

Kiongozi wa Upinzani – Starmer, anasema hadhani kwamba maofisa hao walishughulikia suala hilo ipasavyo, ikizingatiwa uwapo wa mtoto huyo kwenye gari. 

“Matumizi ya pingu ni utata na siwezi kabisa kuona uhalali wa kuzitumia dhidi yao. Ni juu ya polisi sasa kuonesha uhalali wa vitendo vyao. Kwanza nashindwa kuelewa sababu ya kuwasimamisha hata. Ninachojua ni kwamba iwapo ningekuwa ofisa mwandamizi ninayetazama video ile, ningejihisi vibaya juu ya jinsi tukio lilivyokuwa,” anasema Starmer.

Meya wa London, Sadiq Khan, anasema amefungua malalamiko na Polisi wa London, kwamba tukio linaonekana kuhusisha ubaguzi wa rangi. Anasema ni muhimu kwa polisi kujielekeza vizuri ili wabaki kuaminiwa na umma wa watu wote bila kujali rangi zao.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Simba 4 Yanga 1

Simba Atoa Kichapo kwa Yanga

Benard Morrison

Morrison amejimaliza mwenyewe..