Waswahili husema miluzi mingi humpoteza Mbwa, wanamaana kubwa katika maisha ya kawaida ya mwanadamu, hii inatokana na tamaa au kutoelewa sehemu sahihi ya kwenda.
Kabla sijaingia kilichonileta, waswahili hawa wa Pwani ya Afrika Mashariki walimaanisha kuwa unapohitaji kufanya jambo lako lolote usijaribu kuyumbishwa maana kunakuwna na watu wengi watakupigia kelele , nawe usiwasikilize basi simamia msimamo wako.
Nondo ni beki kisiki kwa sasa Tanzania haina ubishi kuwa kwa sasa ndiye beki bora wa kati ambaye anayechezea timu ya soka ya Coastal Union kutoka Tanzania anahitajika na mapacha wa Kariakoo.
Tenakwa timu hizo za Kariakoo zinakuwa kama mwamba ngoma siku zote anavutia kwake kwa ajiri ya kupata saini ya nyota huyo ambaye huduma yake kwa miaka miwili sasa inaonekana ipo juu kuanzi timu ya taifa na klabu anayocheza.
Wanaopuliza miluzi ni Simba na Yanga ambao wanahitaji saini yake sasa namshauri asiende katika mluzi usiokuwa na tija maana atapotea, kuna mifano mingi ya wachezaji waliowahi kutakiwa kwa mbwembwe katika vilabu hivyo baadae wakapotea kabisa katika ramani ya soka.
Mchezaji wa zamani wa Yanga Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ pamoja na Thomas Kipese waliwahi kusema kuwa Nondo ndiye beki bora na anafanna kabisa na kipindi ambao wao wanasakata kabumbu.
“Ukimuangalia umbo la nyota huyo pamoja na nguvu alizo nazo anatumia akili nyingi katika kuondoa hatari unaweza ukaaamini kuwa ni beki bora hapa Tanzania kwa sasa pia ni wakati wake, aliwahi kucheza kama mimi zamani,”alisema Malima.
Baada ya hayo yote sasa ndio unapata maana halisi ya nyota huyo asipokuwa makini atageuzwa kitoweo cha sikukuu.
Wakati tunaendelea hebu tuangalia nafasi atakayoenda kucheza ndani ya vilabu hivyo.
Yanga wana mabeki wengi, Lamine Moro,Kelvin Yondani, Juma Makapu, Andrew Vicent, Ally Ally na Ally Sonso.
Katika mabeki tajwa hapo juu Lamine Moro ndio aliyejihakikishia nafasi ya kudumu katika kikosi hiko huku Juma Makapu akifuatia kupata nafasi akisaidiana na wengine.
Kwa uwezo wa Nondo ambaye ameonekana akifanya maamuzi magumu katika idara ya ulinzi moja kwa moja anaweza kuingia katika kikosi hiki akiwa sambamba na Lamine Moro na atacheza ukizingatia Kelvin Yondani umri ushamtupa mkono ambaye huenda ndio anaweza kufanya afikirie nafasi yake ndani ya kikosi.
Vipi kuhusu mishahara ipo vizuri au kama zamani wazee wa bakuli, kulijibu hilo Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema kuwa hakuna shida ya mishahara kwa sasa.
Ushahidi wa hiyo kweli tunaona GSM wameweka mambo sawa na kila kitu kinaenda vizuri kwa sasa ndani ya timu hiyo.
Kwa upande wa Simba nako pia kuna changamoto kama zile za Yanga, mabeki waliopo, Yusuph Mlipili ambaye hajapata nafasi muda mrefu,Erasto Nyoni umri unamtupa mkono,Serge Pascal Wawa umri na amepewa mwaka mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo na Kenedy Juma.
Wanaopata nafasi ya kucheza mara kwa mara ni Erasto Nyoni pamoja na Pascal Wawa ambao jua inaelekea kuzama, kwa mtaji huo Nondo anauwezo wa kuja Simba na kucheza ndani yake na akapata mafanikio pia.
Kuhusu mshahara hapa hakuna tatizo kabisa wanamfumo tayari ambao hakuna mawazo ya mshahara kabisa.
Kwa mtazamo huo jamaa anaweza kuingia moja kwa moja katika vikosi vya timu hizo mbili, kumbe katika uhakika wa nafasi ya kucheza anaweza kuingia moja kwa moja kikosini na kukichafua baina ya vilabu hivyo pendwa viwili hapa Tanzania.
Nini anatakiwa afanye basi aangalie dili kubwa huenda ikawa ndio maslahi yake makubwa kuwahi kusaini licha ya umri wake kuwa mdogo, kwa uzoefu wa ligi hii aangalie maslahi sasa kama anavyopandisha dau lake.
Taarifa zisizo rasmi kupita vyombo vya habari zinasema kuwa nyota huyo ataelekea Yanga, lakini bado hapo hapo Simba wameingia tena kuharibu dili hivyo anatakiwa asome alama za nyakati wakija kichwa kichwa awababue tu apate maslahi.
Naye isje kuwa baadae anahojiwa katika vipindi vya radio sitaki nije nisikie kuwa kipindi anacheza hakukuwa na maslahi wakati utajiri upo miguuni mwake.
Wakala wa mchezaji huyu pia anatakiwa atulie sana na aanaglie wapi sehemu sahihi ya kumpeleka nyota huyo, baada ya tovuti hii kufanya uchunguzi wa namba na kuona anaweza kucheza sehemu gani basi yeye pia anatakiwa aangalie wapi sasa ampeleke kwani popoe anaweza kupata namba.
Nondo ni nyota wa timu ya taifa atakuwa msaada mkubwa sana katika taifa anatakiwa atulize akili aache sifa bandia ilia acheze soka kwa muda mrefu..
Wachezaji waliowahi kucheza nafasi yake kama Victor Costa,Boniface Pawasa,Nadir Haroub na wengine wengi walichagua sehemu sahihi na ndio maana wamecheza kwa mafanikio makubwa na kuandikwa kama mabeki bora kwa vipindi vyao.
Utakavyofika mjini nitakukariisha rasmi kupitia tovuti hii nikueleze mambo muhimu hapo Kariakoo yalivyo na nini ufanye ili ucheze kwa muda mrefu.
Pia nitakukarisha rasmi Dar es Salaam nitakupa mifano ya wachezaji waliokuwa wamepotea baada ya kuingia katika jiji pendwa Tanzania, hivyo nawe utapata wusia huo kwa mapana yake.