BINGWA wa zamani wa uzani wa juu wa ngumi duniani, Muhammad Ali yupo taabani kwa ugonjwa kitandani.
Rahman Ali, ambaye ni ndugu yake Muhammad, amesema kwamba kaka yake anaumwa hivyo kwamba amefikia hatua ya kushindwa kuzungumza. Nyota huyo aliyetamba kwa muda mrefu na kupendwa sana, aligundulika kuwa na ugonjwa wa kutetemeka mwaka 1984.
Ali (72) alikuwa mgonjwa hivyo kwamba Jumatano iliyopita alishindwa kwenda Hollywood kwa ajili ya kushuhudia filamu kuhusu maisha yake iitwayo ‘I Am Ali’, ambapo Rahman alikwenda na bintiye Ali. Filamu hiyo itazinduliwa nchini Uingereza Novemba 28.
“Sikuweza hata kuzungumza na kaka yangu (Ali) juu ya filamu hii kwa sababu ni mgonjwa sana na anazungumza kwa shida. Alishatukubalia tuendelee na kazi hii kwa hiyo ni wazi anaona fahari kwa sisi kuwa hapa,” akasema Rahman Jumatano hiyo akiandamana na binti wa Ali, Maryum mwenye umri wa miaka 46.
Rahman ni mdogo kwa Ali kwa mwaka mmoja tu, na amesema kwamba kaka yake amekuwa shupavu kupambana na ugonjwa huo kwa karibu miaka 30 sasa.
Comments
Loading…