Tanzania imekuwa ikisuasua katika soka hususani timu ya taifa huku maoni ya wengi yakisema kocha wa timu ya taifa anatakiwa awe mzawa kwa manufaa ya nchi.
Tanzania imekuwa ikiajili makocha wa kigeni kwa muda mrefu ikiwaacha wazawa walio nasifa za kuifunza timu ya taifa wasipate kazi.
NAUNGA MKONO HOJA
Turejee michuano ya AFCON iliyofanyika mwaka jana Ivory Coast, timu yetu ilifunzwa na Adel Amruche mechi ya kwanza Stars ikala 3 mtungi, baada ya hapo kocha mkuu wa Stars aliongea maneno yasiyofaa amefungiwa na Chama cha Soka Afrika CAF timu ikapewa wazawa Hemed Morroco na Juma Mgunda.
Mchezo uliofuata ulikuwa dhidi ya Zambia Stars ilitoa sare na ilihitaji alama tatu katika mchezo wa mwisho dhidi ya Congo ili iandike historia ya kutinga 16 bora bahati mbaya ilitoa sare.
KWANINI TUWAPE WAZAWA
Makocha wazawa wana wafahamu vizuri wachezaji wa ndani na namna walivyo na udhaifu wao na nafasi gani halisia wacheze.
Licha ya kuwafahamu bado wachezaji wa ndani hawapati nafasi katika timu zetu zinazofanya vizuri Kimataifa mfano Yanga, Simba na Azam FC hivyo muda makocha wazawa wangeweza kuwafahamu maana na wao wapo wanaangalia ligi inavyoenda.
Wanafahamu tabia za wachezaji wetu jinsi walivyo na utaratibu wao ni jambo la msingi sana kila sehemu ina utaratibu wake.
Makocha wa kigeni hawaweza kutambua hayo japo mpira ndio huo huo unaochezwa popote ulimwenguni ila kwa Tanzania nafikiri bado hatujafika huko.
MAKOCHA WENYEWE KINANANI ?
Unaweza kujiuliza makala inatuambia makocha wazawa kinanani na wanasifa ?
Hawa nitakao wataja hapa wana sifa za kuwa makocha wakuu wa timu ya taifa ya Tanzania.
Juma Mgunda
Huyu mchezaji wa zamani wa Coastal Union na aliwahi kuhudumu kama kocha lakini baadae amepata shavu Simba uwezo wake wala hauna kifani ni kocha aliye na sifa zote kwani leseni yake inaruhusu kuwa kocha mkuu angalia Simba akiachiwa japo kwa nafasi ndogo anavyoifanya.
Charles Boniface Mkwasa
Mchezaji wa zamani wa Yanga, nahoddha wa Yanga, Katibu mkuu wa Yanga na amewahi kuhudumu kama kocha mkuu wa timu hiyo, pia alifundisha Ruvu Shooting amewahi kuhudumu timu ya taifa ya Tanzania kama kocha na mchezaji.
Ana sifa za kila aina kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania.
Jamhuri Kihwelo
Nyota wa zamani wa Simba kocha wa zamani wa Simba , kocha wa zamani wa Stars alihudumu Namungo, Singida Fountain Get FC ana sifa za kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa.
Hemed Suleiman Morroco
Kocha wa zamani wa Namungo, Mbao FC Zanzibar Heroes na sasa ndio kocha wa muda wa Stars, anaweza kuwa kocha mkuu kwani ana vigezo vyote.
Wengine ambao wataweza kuwa makocha wakuu au wasaidizi ni pamoja na Saleman Matola, Denis Kitambi, Abdallah Kibaden aliwahi kuwa kocha mkuu wa Stars.
Hao wote na wengine ambao sijawataja wataweza kutufikisha nchi ya ahadi, niwaombe TFF kwa kipindi hiki tuwape imani na tuangazie jicho kwa wazawa wakati tunaendelea kutengeneza mifumo imara ya kuwa na wachezaji bora.
Licha ya hayo yote TFF wanapowapa nafasi makocha wetu hawawapi mahutaji muhimu, mfano wanapokuja wageni wanatafutiwa watalaamu wa kusoma mchezo na wataalamu wengine katika kila sehemu, wanapowapa kazi makocha wazawa waangalie vigezo hivi pia.
Sikatai kuwa tunatakiwa kutengeneza mifumo mizuri ya kupata wachezaji safi lakini inategemea wanaoongoza soka wana mipango gani.
Comments
Loading…