Menu
in

Mtanzania kuwania ubingwa wa WBC

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Omary Ramadhani amechaguliwa kuwania ubingwa wa vijana wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) dhidi ya bondia wa Hungary, Gabor Veto.

Pambano hilo limepangwa kufanyika Aprili 17 nchini Uswisi, kwa mujibu wa Rais wa Chama Cha Ngumi za Kulipwa cha TPBO, Yasin “Ustaadh” Abdallah.

Abdallah alisema kuwa Ramadhan kwa sasa yupo kazika mazoezi mkali kwa ajili ya pambano hilo la raundi 12 lililopangwa kufanyika kwenye ukumbi wa ArteCad Arena, Tramelan chini ya promota Angelo Fasolis.

Alisema kuwa Mtanzania huyo anakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na ukweli kuwa Veta hajapoteza hata pambano moja kati ya 14 aliyocheza na ameshinda 11 kwa knock out (KO). Ramadhan ameshinda mapambano saba na kupoteza manne huku moja akitoka sare.

Alifafanua kuwa kutokana na ukali wa pambano hilo, TPBO imeamua kumpekela bondia huyo nchini Kenya kwa ajili ya mazoezi na kuzoea hali ya hewa kwani inafanana na ile ya Uswisi ambayo ni ya ubaridi.

Alifafanua kuwa akiwa huko atakuwa chini ya kocha maarufu, Julius Odhiambo ambaye atamnoa kabla ya kupanda ndege huko huko kwenda kuopeperusha bendera ya Tanzania.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version