in , ,

Moyes awaadhibu Welbeck, Cleverley na Young

*Ni kwa kukesha wakijirusha baada ya kufungwa

Kocha wa Manchester United, David Moyes amewaadhibu wachezaji wake Danny Wellbeck, Tom Cleverly na Ashley Young kwa makosa ya ulevi na kustarehe baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL).
Wachezaji hao watatu wameonekana wakiwa mitaani, wakicheza na kurukaruka, kuzungumza na wasichana huku waionekana wana furaha kubwa wakati walikuwa wamepoteza mechi.
Moyes amewaonya wachezaji hao kwa kutokuwa na maadili na kwamba hatima yao inaweza kuwa mbaya klabunini hapo kwa kujirusha saa chache tu baada ya timu yao kuadhibiwa kwenye mashindano pekee ambayo wangeweza kupata kombe msimu huu.
Wachezaji hao ambao pia wamo kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya England, Three Lions, walikuwa katikati ya Jiji la Manchester ambapo waliendelea kujirusha hadi asubuhi ya Ijumaa.
Moyes aliwaita watatu hao kwa mazungumzo kwenye makao makuu ya United yaliyomo Carrington na baadaye aliwafanyisha mazoezi ya ziada wakiwa peke yao nje ya kikosi cha timu ya kwanza.
Moyes pia amewapiga faini wachezaji hao, lakini haijaeleweka hasa kama aliwatoza faini ya mshahara wa wiki moja au wiki mbili ikiwa ni siku chache kabla ya Moyes kukiongoza kikosi chake kwenda kucheza dhidi ya timu yake ya zamani ya Everton Jumapili hii.
Wakati huo huo, kuna tetesi ambazo hata hivyo zimekanushwa, zikidai kwamba wamiliki wa klabu hiyo, familia ya Glazer kubwa wamekutana na Kocha wa Timu ya Taifa ya Uholanzi, Louis Van Gaal anayemaliza muda wake na timu hiyo baada ya kichuano ya Kombe la Dunia.
Hali hiyo inaacha maswali mengi iwapo Glazer watamkabidhi Moyes au Van Gaal kitita cha pauni milioni 150 zilizopangwa kwa ajili ya usajili mkubwa kwa ajili ya msimu ujao ambapo wachezaji wengi wanatarajiwa kuondoshwa kwa kutolewa mikopo, kuuzwa au wale ambao mikataba yao inaisha isihuishwe.
Mshambuliaji wa Man U, Robin van Persie alionekana akiwa na kocha Van Gaal akitazama mechi baina ya n PSV Eindhoven na klabu yake ya zamani ya Feyenoord. Inadaiwa kwamba akina Glazer walikutana na Van Gaal nchini Uswisi majuzi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Azam mabingwa wapya Tanzania

Arsenal wawatega Everton