Menu
in , , , ,

Mosquera aipa Arsenal ushindi dhidi ya Wolves..


Haijawahi kutokea katika historia ya soka la England timu kuwa na rekodi mbaya zaidi ya ligi baada ya mechi 15 kuliko Wolves — katika ngazi yoyote ya soka la kulipwa. Mavuno yao ya pointi mbili yalionesha ukubwa wa hali mbaya waliokuwa nayo, ingawa hayakueleza kila kitu.

Inasemekana kipimo cha mabingwa wa kweli ni kushinda hata unapocheza vibaya.
Kwa kipimo hicho, Arsenal iko sahihi..

Kabla ya mechi kuanza, waendesha kamari waliwapa Wolves uwezekano wa 28-1 kushinda; sare ilikuwa 8-1. Ilibidi uwape heshima mashabiki wao 3,000 walio safiri ambao walichukua tiketi zote walizopangiwa. Hakukuwa na treni za kurudi Wolverhampton, napafahamu vizuri, Dada yangu anaishi hapo.. Kazi isiyowezekana? Hii ilikuwa safari ya gharama sana kwa mashabiki.

Hata hivyo, Wolves walipambana na wakashangaza. Kwa sehemu kubwa ya mechi, ilionekana kana kwamba tunashuhudia matokeo ya kushtua ya msimu yakitokea. Arsenal walikuwa mbali kabisa na kiwango chao. Vinara wa Ligi Kuu wangeweza kutaja uchovu kama kisingizio. Pia iliwezekana kujiuliza kama kulikuwa na hali ya kujiridhisha — hata miongoni mwa mashabiki katika Emirates Stadium, ambako hali ilikuwa ya kawaida mno na isiyo na msisimko, hasa kipindi cha kwanza.

Timu ya Mikel Arteta ilicheza karata yao ya ushindi dakika ya 70; kutoka kwenye kona, kama ilivyo desturi. Kidogo sana, bahati iliwaendea vyema katika mchezo wa wazi. Ilikuwa ni Bukayo Saka aliyepiga kona ya ndani kutoka upande wa kulia, ndipo dunia ya Sam Johnstone ikaporomoka. Kipa wa Wolves alikosea mwelekeo wa mpira na alipokuwa akijaribu kurudi, alionekana kuugusa mpira dhidi ya nguzo ya mbali. Mpira ukarudi, ukampiga yeye mwenyewe na kuingia golini.

Tanzania Sports

Jambo la kushangaza ni kwamba wageni wa Rob Edwards hawakukata tamaa. Arsenal walijaribu kulinda uongozi wao kuelekea mwisho wa mechi na wakajiondoa nyuma, karibu kuwaalika wapinzani wao washambulie. Arteta alikuwa na hasira kali kuhusu hili baadaye.

Wolves walisukuma mashambulizi dakika ya 89, mchezaji wa akiba wa Arsenal, Myles Lewis-Skelly, akilazimika kufanya tackle muhimu dhidi ya Tolu Arokodare, naye pia akiwa ametoka benchi. Kisha ikatokea. Wakati mchezaji mwingine wa akiba, Mateus Mané, alipovusha mpira kutoka kushoto, Arokodare alimzidi Piero Hincapié na kupiga kichwa kilichompita David Raya. Mtangazaji wa Emirates alitangaza bao hilo kuwa la Mané. Lakini kama yeye alikuwa amechanganyikiwa, basi kila mtu alikuwa hivyo.

Arsenal walipata jibu ndani kabisa ya muda wa nyongeza; bao la kuzuia maafa, kufunika nyufa — kwa shida tu. Arteta alikuwa amemuingiza Gabriel Jesus, naye akajiweka vizuri mbele ya lango wakati Saka aliposhusha ‘jaro’ mpira kutoka kulia. Mpira ukaingia golini kupitia kichwa cha Yerson Mosquera. Bao lingine la kujifunga; pigo kubwa kwake na Wolves. Beki huyo alilala chali uwanjani kwa muda mrefu sana.

Ahuweni kwa Arsenal ilikuwa dhahiri. Arteta alikuwa ameona uongozi wa timu yake kileleni mwa ligi ukipungua hadi pointi mbili baada ya kipigo cha 2-1 dhidi ya Aston Villa Jumamosi iliyotangulia. Hakuweza kuvumilia kuteleza tena. Alihitaji kuweka presha kwa Manchester City kabla ya ziara yao Crystal Palace Jumapili. Tafsiri chanya ilikuwa kwamba kushinda kwa tabu ni alama ya mabingwa. Hakika ilikuwa mechi mbaya kwa sura ya uchezaji.

“Kulikuwa na kipindi cha dakika mbili au tatu ambapo tulikuwa tumerudi nyuma, tulikuwa wa kutazama tu, na tulikuwa na tabia mbaya kabisa za kujilinda,” Arteta alisema kuhusu muda huo wa mwisho. “Hicho hakikaribii kabisa kiwango kinachohitajika. Tunajisikia nafuu kwa sababu tuliweza kufunga bao mwishoni na kushinda, lakini lazima tuboreshe hilo, bila shaka. Tulifanya mambo kuwa magumu zaidi kwa jinsi tulivyokubali bao. Hilo halikubaliki.”

Wolves walikuwa wameweka kiwango cha chini sana kwa uchezaji wao katika kipigo cha 4-1 nyumbani dhidi ya Manchester United Jumatatu iliyopita, lakini hata hivyo, huu ulikuwa uchezaji bora zaidi kuanzia filimbi ya kwanza. Kujituma kulikuwepo, hasa katika mapambano ya ana kwa ana. Emmanuel Agbadou alikuwa mfano wake katika safu ya ulinzi, akimzuia kabisa Viktor Gyökeres. Toti alikuwa mzuri pembeni yake, na João Gomes pia alifanya kazi kubwa katikati ya uwanja.

Arsenal walikuwa wabaya sana kipindi cha kwanza. Polepole, wa kutabirika. Karibu kila kitu katika mchezo wa wazi kilipitia kwa Saka upande wa kulia, lakini licha ya jitihada zake na ujanja wake, hakuweza kufanya mambo yatokee. Timu ya Arteta ilikuwa na nafasi moja kubwa tu kabla ya mapumziko, ambayo bila kushangaza ilitokana na kona ya ndani ya Declan Rice. Gabriel Martinelli alikuwa huru kabisa nyuma ya nguzo ya mbali lakini aliielekeza krosi yake ya kichwa juu ya lango. Martinelli alikuwa na nafasi nyingine mbili za hatari lakini akakosa uthubutu.

• Bao la kujifunga la Yerson Mosquera lilikuwa bao la 18 la ushindi la dakika ya 90 la kujifunga katika historia ya Ligi Kuu. Asilimia 33 ya mabao hayo yamekuwa kwa ushindi wa Arsenal (6 kati ya 18), mawili sasa dhidi ya Wolves katika Emirates Stadium (pia José Sá Februari 2022).


• Wolves sasa wamefunga mabao mawili ya kujifunga katika mechi moja ya Ligi Kuu mara tatu, mawili kati ya hayo yakiwa dhidi ya Arsenal (pia Molineux katika kipigo cha 4-1 Novemba 2009). Hakuna timu iliyofunga mabao mengi ya kujifunga katika mechi tofauti zaidi.


• Hii ilikuwa mara ya saba timu kufunga mabao mawili katika mechi ya Ligi Kuu ambapo mabao yote yalikuwa ya kujifunga, na ya kwanza tangu Leicester walipopoteza 2-1 dhidi ya Liverpool Desemba 2022. (Opta)

Tukio lililoinua mapigo ya moyo kipindi cha kwanza lilitokea upande mwingine, Wolves walipovunja mashambulizi baada ya kuzuia kona ya dakika ya 27. Hwang Hee-chan alikimbia kutoka nusu yake ya uwanja bila mtu yeyote mbele yake isipokuwa Raya, huku kundi la wachezaji wekundu likimfuata nyuma; kama paka katikati ya njiwa. Aliendelea kukimbia na akapiga shuti, Raya akijitupa chini na kuokoa. Hincapié alifanya vyema kuzuia jaribio la Jørgen Strand Larsen dakika ya 45 baada ya awali kuteleza.

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Leave a Reply

Exit mobile version