*Algeria wawapiga Korea
*Marekani na Ureno sare
Mzaliwa wa Kenya aliyeamua kuchezea Ubelgiji badala ya Harambee Staras, Divock Origi amelivusha taifa hilo katika hatua za makundi.
Akitokea benchi, Origi (19) alipachika bao dakika mbili kabla ya mechi dhidi ya Urusi kumalizika Jumapili hii.
Mechi ilikuwa ngumu na ilielekea kumalizika kwa suluhu, bada ya Alexander Kokorin kukosa bao la wazi katika nusu ya kwanza akiwa umbali wa yadi sita tu.
Shuti la Kevin Mirallas nalo liligonga mwamba dakika sita kabla ya mechi kumalizika ndipo Origi aliponasa majalo ya Eden Hazard na kupachika bao la ushindi.
Origi anayechezea Lille aliingia kuchukua nafasi ya Romelu Lukaku ambaye hakufurahishwa na kutolewa kwake nje, lakini Origi alionesha umuhimu wake.
Urusi wamebaki na pointi moja tu.
ALGERIA WAWATUNGUA KOREA 4-2
Algeria wamefanikiwa kupata ushindi wa 4-2 dhidi ya Korea Kusini.
Mabao ya Algeria yalifungwa na Islam Slimani, Rafick Halliche, Abdelmoumene Djabou na Yacine Brahimi.
Mabao ya Korea yalifungwa na Song Heung-min na Koo Ja-cheol. Huu ni ushindi wa kwanza kwa Algeria tangu 1982.
Algeria watatakiwa kupata ushindi dhidi ya Urusi kwenye mechi ya mwisho kujihakikishia nafasi katika hatua ijayo ya mtoano.
MAREKANI SARE NA URENO
Ureno wamefufua matumaini ya kusonga mbele baada ya kupata pointi moja kwenye mechi dhidi ya Marekani.
Ureno walipata bao la kusawzisha dakika za mwisho mwisho kupitia kwa Silvestre Varela.
Akitokea benchi, Varela alifunga kwa kichwa majalo ya nahodha Cristiano Ronaldo. Bao la kwanza la Ureno lilifungwa na winga wa Manchester United, Nani.
Marekani walipata mabao yao kupitia kwa Jermain Jones na Clint Dempsey.
Comments
Loading…