in , , ,

MICHAEL CARRICK KWENYE UBETI MMOJA NA FUNDI AKILI

Solomon Carter Fuller alikuwa ni mwanafizikia wa kimarekani mwenye asili ya kiafrika aliezaliwa nchini Liberia kwenye karne ya 18. Alikufa kwenye karne iliofuata akiwa ni Shujaa asiyeimbwa lakini mwenye mchango mkubwa katika kulitafutia utatuzi ugonjwa wa Azeima (maradhi yanayodhoofisha akili).

Inawezekana ni kwa sababu alikuwa mwafrika lakini pia kundi la watu waliomsomesha ambao alikuwa nao pamoja pia kina Ekil Kraeptin na mwenyewe bwana Alois Alzheimer waliofanya asitajwe miongoni mwa wengi.

Carter Fuller alisambaza ujuzi wake kwa wingine lakini alipata kuitwa baada ya taasisi za tiba kadhaa pale ambapo ni wazi mchango wake ulikuwa ni mkubwa kulikuwa alivyochukuliwa.

Michael Carrick nae amekuwa kwenye kundi la watu wachache duniani kwenye nyanja mbalimbali asiyeimbwa licha ya mchango mkubwa aliokuwa nao kwenye kuifanya klabu ya Manchester United kupambwa kwa miaka takribani 12 aliodumu klabuni hapo.

Kama ilivyokuwa kwa Bw. Fuller, Carrick alicheza sambamba na nyota waliofanya vizuri sana kipindi anatua klabuni hapo mwaka 2006 pale alipoamua kwenda kuyasaka mataji mbalimbali Old Trafford. Kundi la kina Paul Scholes, Cristiano Ronaldo, Ryan Giggs, Ji Sung Park, Luis Nani ambao walikuwa kwenye ubora mkubwa kiasi kwamba waliathiri sana jina la Michael Carrick kwenye midomo ya mashabiki.

Ni kama ambavyo inatokea pia pale Barcelona kwa Sergio Busquets. Jamaa nae amekosa bahati ya kuimbwa kabisa na anaonekana ni mchezaji aliekosa heshima anayostahili ikilinganishwa na mchango mkubwa alionao hasa pale anapokosekana kwenye timu.

Unajua shida nini? Ni kundi la wachezaji waliomzunguka wakiwa kwenye ubora mkubwa kiasi kwamba imekuwa ni ngumu kwa Busquets kuweza kunukia kwenye midomo ya watu.

Amekuwa sambamba na viungo bora kabisa pembeni yake, Xavi Hernandez na Andres Iniesta lakini ni pale anapokosekana yeye ndipo inapokuwa haina tofauti na chai iliokosa Sukari. Barcelona unaiona inayumba hasa kiulinzi lakini amefunikwa na ubora mkubwa uliomzunguka kwenye idara tofauti klabuni hapo akiwemo mfalme Leo Messi pia. Ni ngumu kwa Busquets kuimbwa kamwe pale Nou Camp.

Basi ndio Carrick pale United. Kuna vitu adimu sana analeta uwanjani lakini ubora mkubwa wa wachezaji waliomzunguka kwa nyakati tofauti kwenye safari ya kuipa mafanikio United imekuwa ni sababu Carrick ni shujaa asieimbwa pale kwenye mji wa Manchester kaskazini mwa nchi ya England.

Kama ambavyo Fuller alisambaza ujuzi wake juu ya Alzheimer ni wazi kuwa umefika wakati Michael Carrick afanye hivi kupitia benchi la ufundi la Manchester United. Ana uzoefu wa kutosha lakini pia anajua sifa za mchezaji anaetakiwa kuichezea klabu kubwa kama United hivyo ni wazi Mourinho ana mtu anaeweza asiwe na uzoefu na ukufunzi lakini ni mtoto wa nyumbani na anaijua mitaa yote atamwonyesha njia kwaiyo kazi kwake sasa.

Na kama ambavyo taasisi na shule 2-3 zilivyoitwa baada ya Fuller. United imefanikiwa kumpa heshima ya unahodha lakini pia mechi maalumu (Testimonial) Michael Carrick licha ya ukweli kwamba hatokuwa mchezaji anaeimbwa baada ya kuondoka pale Old Trafford.

Mashujaa wasioimbwa wana wimbo wao niliouchambua na kumpata fundi wa kurudisha au kuzindua akili dhaifu Solomon Carter Fuller na mtaalamu wa pasi za kushambulia zenye usahihi mkubwa, Michael Carrick.

Report

Written by haatimabdul

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

PIERRE AMEKUJA SIMBA MUDA AMBAO SIYO SAHIHI

Tanzania Sports

HIKI KITABU CHA GEORGE WEAH TUTAKIANGALIA NA KUKIPUUZA.