Nahodha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mecky Mexime amelishukuru shirikisho la soka, TFF, kwa kuthamini mchango wake wa miaka nane aliyoichezea timu hiyo.
Mexime alisema hakutarajia angeweza kuthaminiwa kwani ni wachezaji wengi walistaafu kuichezea timu hiyo, lakini hawakufanyiwa mambo kama alivyofanyiwa yeye ikiwemo kuandaliwa mechi ya kirafiki ya kimataifa kwa ajili ya kuagwa na kupewa zawadi za sanamu ya mchezaji, viatu na jezi.
“Sikutegemea kabisa kama ninaweza kuthaminiwa hivi. Nimefurahi sana na ninaomba wasiishie hapa kwangu na waangalie kwa wachezaji wengine wakiamua kustaafu kwa hiyari yao kwenye timu ya taifa,“ alisema Mexime.
Hatahivyo, baadhi ya wapenzi wa soka wamepinga Mexime kuagwa katika mechi ya timu ya taifa ya Bara, Kilimanjaro Stars, badala ya timu ya taifa yenye mjumuisho wa wachezaji wa Zanzibar pia.
Venance Mwamoto, mchezaji wa zamani wa Lipuli ya Iringa aliliambia Lete RAHA wakati wa mechi kati ya Kilimanjaro Stars na Zambia katikati ya wiki kuwa Mexime alitakiwa kuandaliwa mechi kubwa zaidi.
�Hii sio mechi ya kumuaga mchezaji huyu, kwani alistahili kuwemo katika kikosi cha Stars, lakini tunashindwa kuelewa kwa nini walifanya hivi,� alisema Mwamoto kumzungumzia beki huyo wa Mtibwa Sugar inayoshika nafasi ya pili kwenye ligi kuu ya Bara.
- SOURCE: Lete Raha
Comments
Loading…