in , ,

Messi atapika uwanjani


*Tanzania sare na Namibia, England washinda
*Cameroon wabugizwa 5-1, Algeria wao  safi

 
NYOTA wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi ametapika uwanjani wakati akiwakilisha Timu ya Taifa ya Argentina dhidi ya Romania na mechi kumalizika kwa sare tasa.

Hii ni mara ya tatu kwa Messi kutapika uwanjani, na hali ya sasa inayokuja baada ya kuwa nje kwa majeraha na kushuka kiwango inaacha hofu miongoni mwa wadau wa soka wa Barca na kwao Argentina.

Usiku wa Jumatano haukuwa mzuri kwa mpachika mabao huyo kwa sababu si tu hakuweza kuzifumania nyavu, lakini kitendo cha kutapika kilishitua wengi na bila shaka kitakuwa na athari za kisaikolojia kwa sababu ilikuwa hadharani katikati ya dimba.

Messi alipata kutapika kwenye mechi ya Super Cup nchini Hispania 2011 kabla ya kufanya hivyo tena akicheza nchini Bolovia 2013.
Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Ufaransa, Zinedine Zidane alipata kutapika uwanjani, muda mfupi kabla ya kuzitikisa nyavu kwa penati dhidi ya England katika mashindano ya Euro 2004.

Argentina walishindwa kufanya kile kilichotarajiwa licha ya kuanza na washambuliaji watatu hatari katika  Messi, Gonzalo Higuain na Sergio Aguero na hata Angel Di Maria alishindwa kuonyesha cheche anazoonyeshaga akiwa na Real Madrid.

Romania walionesha mchezo mzuri dhidi ya Argentina usiku huo Afrika Kusini wakicheza nyumbani walibugizwa 5-0 na Brazil katika mechi ambayo nyota chipukizi Neymar alipiga hat-trick.

Tanzania wakicheza chini ya Kocha Salum Madadi katika Uwanja wa Sam Nujoma, Namibia, walipata sare ya 1-1, bao la Taifa Stars likifungwa na Mcha Khamis.

Hii ilikuwa mechi ya kwanza kwa Stars tangu kuondoka kwa kocha wake, Kim Poulsen ambaye mkataba wake ulikatishwa kwa makubaliano baina yake na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
 
 
MATOKEO YA MECHI ZA KIMATAIFA

Katika mechi nyingine za kimataifa za kirafiki zilizochezwa Jumatano hii, England waliwafunga kwa tabu Denmark kwa bao la dakika za mwisho la Daniel Sturridge wa Liverpool.

Hispania waliwafunga Italia 1-0, Ufaransa wakawashinda Uholanzi 2-0, Ureno wakawatandika Cameroon 5-1, Australia wakapigwa na Equador 4-3, Ujerumani wakawafunga Chile 1-0, Uswisi na Croatia wakaenda sare ya 2-2.

Marekani walifungwa 2-0 wakiwa wageni wa Ukraine, Uturuki wakawakong’ota Sweden 2-1 wakati Colombia wakienda sare ya 1-1 na Tunisia, Misri wakalala 0-2 nchini Bosnia-Hercegovina, Montenegro wakawafunga Ghana 1-0, Algeria wakashinda mbele ya Slovenia 2-0 huku Jamhuri ya Czech wakienda sare ya 2-2 na Norway

Cyprus ilikwenda suluhu na Ireland Kaskazini, Poland wakaanguka 0-1 mbele ya Scotland, Jamhuri ya Ireland wakafungwa 1-2 na Serbia, Wales wakawatandika Iceland 3-1, na Georgia wakawafunga Liechtenstein 2-1.

Mechi nyingine iliwakutanisha Urusi waliowachapa Armenia 2-0, Azerbaijan wakawafunga Ufilipino 1-0, Lithuania wakaenda sare ya 1-1 na Kazakhstan, Bulgaria wakawapiga Belarus 2-1 na Albania wakawafunga Malta 2-0.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Carles Puyol: Nang’atuka Barca

Kutoka TFF Leo……….