Simba ina asilimia zaidi ya 80 ya kuchukua ubingwa msimu huu kama wakimalizia vizuri mechi saba walizo bakiza kwenye Ligi Kuu.
Mnyama ana ongoza Ligi kwa tofauti ya alama 2 baada ya michezo 24 aliyo shuka dimbani, Wekundu wa Msimbazi wapo kileleni kwa pointi 54 huku akifatiliwa kwa karibu na mpinzani wake Yanga mwenye alama 52.
Simba wanasaka ubingwa mwaka huu baada ya kuukosa kwa miaka 4, mara ya mwisho kwao kulichukua taji hilo ikiwa ni msimu wa 2011/2012
Wekundu wa msimbazi wamebakiza mechi 7 kumaliza Ligi kwa msimu huu, kwa mechi hizo zilizo salia, Mnyama ana mechi 4 tu ngumu kama akitoka salama kwenye mechi hizo anaweza kutawazwa bingwa mpya.
Ungana na makala hii inakuletea mechi 4 zitakazo ipa Simba ubingwa msimu huu
Simba vs Mbeya City
Mechi hii itapingwa wikendi hii katika uwanja wa taifa, mechi hii ni muhimu kwa Simba kushinda ili kuendelea kujitengenezea mazingira ya kushinda taji hilo, ni mechi ngumu kwa kila upande hasa kwa Simba kuliko Mbeya City ambao wao hawana kitu cha kupoteza kuelekea mchezo huo
Kagera Sugar vs Simba
Mechi itapingwa katika dimba la Kaitaba mjini Kagera, ni mechi ngumu kwa Simba sababu ya kiwango alicho nacho Kagera msimu huu, chini ya mwalimu Mexime timu imeimalika kila idara kuanzia eneo la ugolikipa hadi ushambuliaji, pia Wakata miwa hawa wanaisaka nafasi ya tatu kwani hawako mbali nayo hivyo mechi haitakuwa nyepesi
Mbao vs Simba
Mechi nyingine ya ugenini kwa Mnyama, Simba watakuwa Kirumba mkoani Mwanza dhidi ya Mbao Fc, ugumu wa mechi hii kwa Simba ni uimara aliyokuwa nao klabu ya Mbao hasa wanapo cheza na timu kubwa
TOTO Africa vs Simba
Kwa miaka ya hivi karibuni Simba amekuwa na rekodi mbovu dhidi ya TOTO kwenye dimba la Kirumba, pia nafasi aliyoko TOTO ni hatari ya kushuka daraja hivyo kwenye mechi hiyo TOTO wataingia kupambana ili kupata pointi zitakazo waweka kwenye mazingira mazuri