in

Maximo ajiuzulu kufundisha Stars

Kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbrazil Marcio Maximo amejiuzulu kufundisha timu hiyo.

Watu walio karibu na Maximo waliitonya Nipashe jana kuwa kocha huyo amefikia uamuzi huo kufuatia shinikizo la wapenzi na wadau wa soka nchini kufuatia timu hiyo kuchapwa na timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, Jumamosi iliyopita.

Maximo inasemekana aliwasilisha barua yake kwa viongozi wa juu wa soka na nakala yake kupelekwa Ikulu.

Stars ililala 1-0 kwa Kenya, Jumamosi iliyopita, jijini Nairobi, Kenya katika mchezo wa kwanza wa mashindano mapya ya Kombe la Mataifa ya Afrika yanayohusisha wachezaji wanaocheza katika ligi za ndani.

Kufuatia kipigo hicho wadau na wapenzi wa soka walimlaumu Maximo kwa timu hiyo kufanya vibaya na kudai alikuwa hana uwezo wa kuinua kiwango cha timu hiyo.

Baadhi ya mashabiki wamefikia kukumbushia jinsi timu hiyo ilivyocharazwa na Senegal 4-0 na pia kuboronga kwa timu ya Tanzania Bara katika michuano ya soka ya Kombe la Chalenji iliyofanyika hapa nchini mwaka jana.

Maximo inadaiwa amekasirishwa na shutuma za wadau kwa madai watanzania walikuwa wanalazimisha matokeo mazuri ya haraka wakati bado angali anaisuka timu.

Maximo na msaidizi wake, Itamar Amorim wanatazamiwa kuondoka leo alfajiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC) kurejea kwao Rio de Jeneiro, Brazil kuwahi kusherehekea Sikukuu ya Wajinga inayoadhimishwa duniani kote na kurejea baadae saa nne asubuhi ya leo wakati sikukuu hiyo itakapokuwa imemalizika.

  • SOURCE: Nipashe

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Champions League – Ronaldo and Rooney conquer Rome

Champions League – Barca grind out win in Gelsenkirchen