Menu
in , , ,

Mashabiki wa Yanga wanataka kumjua kocha wao

Tanzania Sports

LIGU Kuu Tanzania imeanza kwa kishindo, huku bingwa mtetezi Yanga akifungua mlango wa mabao kwa nia ya kutetea ubingwa wao. Yanga wameingia msimu huu wakiwa na kocha mpya Romain Folz ambaye anaongoza benchi la ufundi lenye ukubwa wa kila idara. Yanga wana wachezaji muhimu ambao wanaweza kuipa ubingwa msimu huu. Hata hivyo ubingwa wao unategemea na ufundi wa kocha ambaye atahitajika pale ambao wachezaji wanakuwa wamekwama kimbinu. Kama alivyowahi kusema aliyekuwa kocha wa Simba, Fadlu Davids kuwa Yanga wana wachezaji wengi wenye uwezo wa kuamua matokeo ya mchezo wowote iwe dhidi ya timu kubwa au ndogo hasa pale ambapo inakabiliwa na kupata ushindi. 

TANZANIASPORTS katika tathmini yake imebaini kuwa kwa mashabiki na viongozi wa Yanga wanatamani kuendeleza ubabe katika Ligi Kuu. Lakini upande wa mashabiki wana mashaka ya umahiri wa kocha wao baada ya kuitazama timu yao katika michezo mitatu waliyocheza ya ushindani. Ingawaje kocha wao Romain Folz ameshinda lakini maoni ya wengi yanaonesha mashaka juu ya uwezo wa kocha wao. Kifupi maelfu ya mashabiki wa Yanga wana hofu ikiwa kocha wao ataweza kulinda heshima na hadhi waliyotengeneza kwa misimu minne mfululizo.

‘Derby’ ya kwanza

Katika mchezo wa kwanza wa watani wa jadi wa Kariakoo, kocha Romain Folz aliibuka na ushindi dhidi ya Simba. Katika mchezo huo wa Ngao ya Jamii, Yanga waliendeleza ubabe kwa kuibuka na ushindi wa 1-0. Kocha Romain Folz alifanikiwa kupata mbinu za kumwadhibu kocha mwenzake mara ya kwanza. Ushindi katika mchezo wa Derby una maana kubwa sana kwa mashabiki wa timu zote mbili. Simba wanaonekana kukubali kuwa Yanga wapo mbali na wana timu tishio na wachezaji wakubwa katika mchezo wa soka. Hata hivyo Simba hawaridhishwi na kufungwa mara kwa mara na Yanga, huku wenzao wakiwa na kicheko zaidi. 

Mashabiki Yanga na Romain Folz

Tangu alipowasili nchini na kutambulishwa kuwa kocha mpya, Romain Folz mashabiki wa Yanga wakuwahi kuona ufundi wa kocha huyo katika mechi za ushindani. Mechi nyingi mechi alizocheza ni za kirafiki ili kuiandaa timu yake. mashabiki wa Yanga wanaingia kwenye Ligi Kuu wakiwa na hamu ya kuangalia ‘uchawi’ wa kocha huyo katika kuipasisha timu yao. Kwa shabiki wa Yanga hakuna raha kama kuifunga Simba na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu. Kwa maana hiyo tangu mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu mashabiki wa Yanga wanatamani kuona mwenelezo wa mbinu zinazotumiwa na kocha wao Romain Folz ili wampime kwa kazi yake. 

Wapinzani wa Yanga

Kwa upande wao wapinzani wa Yanga nao wanacho kibarua cha kufanya tathmini juu ya ubora wa timu hiyo chini ya kocha mpya. Wapinzani wanatamani kuona namna kocha huyo mwenye sifa za kufundisha soka la burudani atafanya nini mbele ya makocha wenzake, na pia wanataka kuendeleza ubabe na kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu. Sasa basi Ligi Kuu imeanza na Yanga wamecheza mechi yao dhidi ya Pamba Jiji na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0. Licha ya ushindi huo bado mashabiki wa Yanga wanaendelea kupima kazi ya kocha huyo katika mfululizo wa mechi zijazo huku wiki hii wakiwa na kibarua cha kucheza mchezo wa kwanza msimu huu wa Ligi ya Mabingwa Afrika katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Wabotswana. 

Romain Folz ataweza kufanya kazi yake vizuri? 

Swali hili wanalo mashabiki wa Yanga na wapinzani wao. Makocha wa timu mbalimbali wanatamani kumdhihirishia Romain Folz kuwa wao ni mafundi kuliko yeye na kwa hiyo watakuwa na kazi ya kumfunga Yanga. Hata uongozi wa Yanga nao utakuwa unafuatilia kwa karibu kazi ya kocha huyu ili kuamua kama anafaa kuendelea kwenye benchi la ufundi la klabu yao. kwa upande mwingine wachezaji watataka kuona kocha wao mpya anawapa mbinu za ziada ili kuibuka na ushindi. Katika mazingira hayo ni matokeo mazuri tu ndiyo yatambakisha Romain Folz katika klabu ya Yanga. endapo timu hiyo itachapwa kwenye Ligi ya Mabingwa bila shaka atafungashiwa virago mapema sana. je ataweza kudumu Yanga? Ni suala la kusubiri na kuona.

Written by Israel Saria

I have been involved with sports in Tanzania as a Volleyball Coach for many years—and was a Tanzania Amateur Volleyball Association (TAVA) leader. I studied sports management at Leipzig University in Germany and understand the science behind sports. That led me to work as a football pundit, with the BBC ( Swahili service) in London. That experience and exposure took me to covering the 2010, World Cup in South Africa. This provided me with a great insight into international level football commentary and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics.I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany, Italy, Belgium, Ireland, France, Kenya etc, and visited almost all of the key football stadiums across United Kingdom, and Europe.

Leave a Reply

Exit mobile version