Aliyekuwa Tanzania One amerudi katika klabu iliyomkuza na kumtambulisha katika Ligi Kuu Tanzania. Aishi Manula amejiunga na klabu yake ya zamani ya Azam Fc akitokea kwa mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu Simba. Taarifa ya kuhamia Azam FC huenda haishutui wengi katika soka, lakini zipo sababu kadhaa ambazo Aishi Manula amesukumwa kujiunga na klabu hiyo. TANZANIASPORTS inakuletea sababu za msingi na adimu kusikika miongoni mwa vyombo vya habari.
Mwarobaini wa Azam?
Hili ni miongoni mwa maswali yanayoulizwa na wadau wa soka sehemu mbalimbali. Azam Fc imekumbwa na matatizo makubwa katika eneo la golikipa tangu kuondokewa kwa Aishi Manula. Lango la Azam halikuwahi kuwa salama tangu aliyekuwa golikipa namba moja Aishi manula alipotimkia Simba.
Kwa muda mrefu Azam wamekuwa wakiishi katika kivuli cha Aishi Manula na kusababisha wadua wa soka kusema diada hiyo imekuwa changamoto kwao na hakuna golikipa aliyefanya vizuri kumzidi kijana huyo. Aishi Manula amecheza kwa mafanikio katika klabu ya Simba na Timu ya Taifa kiasi kwamba alijitengenezea ufalme ambao si rahisi kumpokonya.
Mbele ya Mousa Camara, Aishi Manula aligeukuwa kuwa golikipa namba mbili, na zaidi tangu alipofungwa mabao 5 na watani wa Simba, Yanga walisababisha nyota huyo aweikwe kando. Licha ya kusumbuliwa na majeraha kisha kupona lakini Manula hakurudi kwenye nafasi yake na sasa ni dhahiri ametupa taulo kukubali yaishe kwa sababu Moussa Camara ni golikipa wa daraja la juu ambaye kila timu ingetamani kuwa naye.
Namba Moja Taifa Stars, AFCON
Hakuna ubishi Aishi Manula anawinda namba yake katika kikoi cha timu ya Taifa ya wanaume. Kuwekwa benchi mara kwa mara kumempotezea namba yake katika kikosi cha timu ya taifa huku akishuhudia aliyekuwa msaidizi wake katika klabu ya Simba, Ali Salim akiitwa mara kadhaa. Uwezo wa Aishi Manula si w akutiliwa shaka, lakini hali ya mambo imebadilika mno. Simba walipoamua kumweka kando maana yake alikuwa anatakiwa kufanya kzi ya ziada kurudisha kiwango na namba yake.
hili limeshindiakana na ametupa taulo kwa kuhamia Azam. Aishi Manula anaweza kupoteza namba yake katika kikosi cha Taifa Stars kwa Yakoub Suleman wa JKT Tanzania. Kueleka kwenye mashindano ya AFCON mwaka 2027, Aishi Manula amenusu harufu ya kuyakosa mashindano hayo ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji ikishirikiana na Kenya na Uganda. Kwa msingi huo mashindano ya AFCON ni miongoni mwa kipaumbele cha golikipa huyo.
Manula alishakosa mashindano ya COSAFA mbako Suleiman alikuwa golikipa namba moja na ameonesha ufundi ambao unahitaji utulivu tu na hivyo kumpoka namna Manula moja moja kwa moja. Wakati Suleiman akiwa golikipa anayeanza kuvutia mashabiki na wadau hilo limefahamika kwa Manula kwa sababu anaona bayana ufalme wake umetikisa, na sasa anakwenda Azam kujaribu karata ya mwisho kwa kulenga mashindano ya AFCON 2027.
Mashindano ya Kimataifa
Azam FC watashiriki mashindnao ya Kombe la Shirikisho la CAF. Hii ni nafasi adimu kwa Aishi Manula kwani amekuwa chaguo la tatu katika klabu ya Simba. Lakini katika klabu ya Azam akifanya kazi vizuri kama zamani anakwenda kujichukulia namba moja yake katika klabu hiyo na kutangaza vita kali ya kuwania namba moja ya Taifa Stars. Katika klabu ya Azam atakuwa na nafasi ya kucheza kwenye mashindano hayo kuliko kusugua benchi pale Simba.
Akiwa na Azam atafanikiwa kusafiri kwenda Nchi mbalimbali kadiri itakavyowezekana kuliko kuhamia timu ambayo haishiriki mashindano ya kimataifa. Kwahiyo Azam imempata golikipa wake mwenye njaa ya kurudisha ufalme katika maeneo makuu mawili; kwanza kurudisha namba yake kwenye kikosi cha timu ya taifa, na kisha kuwaonesha wadau kuwa bado yupo sana kwenye kandanda na ndiye nyanda anayetakiwa kufikiriwa linapokuja suala la mashindano ya kimataifa kwa makipa wa ndani. Aishi Manula atakuwa na vita vya kuhakikisha wanaoitwa timu ya taifa wakuwa nyota wenye uwezo muzidi vinginevyo watazidiwa na atajichukulia namba yake kwa mara nyingine.
Benchi la ufundi Taifa Stars
Ukiangalia becnhi la ufundi unagundua kuwa wanamhitaji Aishi Manula ndiyo maana licha ya kusugua benchi pale Simba aliitwa mara kadhaa katika kikosi cha timu ya Taifa badala ya Ali Salim anayechukua nafasi ya pili pale Msimbazi.
Hata hivyo Aishi Manula amekuwa akiitwa kwa imani ni kipa mzuri ambaye alikuwa amekosa mechi za kumwimarisha tu. Kwa maana hiyo idara ya makipa Taifa Stars bado ina makipa wachache waliofikia daraja la Aishi Manula. Benchi la ufundi la Taifa Stars bila shaka limechekelea uamuzi wa Manula kwenda kugombania namba katika klabu ya Azam ambako atakuwa chini ya Florent Ibenge. Ni suala la muda tu.


Comments
Loading…