Mjini Morogoro katika usiku wa sikukuu ya Eid pili ya mwaka huu ndani ya ukumbi wa Tanzanite wapenzi na mashabiki wa ngumi walikusanyika kwa ajili ya kuangalia mapambano mbalimbali ya ngumi ambayo yalipiganwa siku hiyo. Pambano kuu lilikuwa pambano la bondia Twaha Kiduku dhidi ya bondia kutoka taifa la India. Pambano lingine ambalo lilikuwepo lilikuwa pambano la bondia toka mji kasoro bahari namzungumzia bwana Karim Said ama maarufu Karim Mandonga. Yeye mwenyewe hupenda “mtu kazi” dhidi ya bondia toka Chanika bwana Mada Maugo. Katika pambano hilo bwana Mandonga alipigwa kwa knockout na akashindwa kuendelea na pambano.
Amekuwa ni nembo ya mchezo wa ngumi nchini Tanzania kwani kwa kipindi cha hivi karibuni mapambano makubwa mengi ambayo yaliandaliwa nchini Tanzania basi yamemshirikisha kama mchezaji katika mojawapo ya mapambano hayo na hata baadhi ametumika kama mhamasishaji kama vile pambano maarufu ambalo liliandaliwa jijini Dar es salaam ambalo lilijulikana kama Dar boxing Derby alitumika kama mhamasishaji katika pambalo hilo licha ya yeye kutokupanda ulingoni waandaaji wa pambano hilo walimuita katika mkutano na waandishi wa habari na aliongea na kisha kuwahamasisha wapiganaji wapambane kwa nguvu zao zote na halikadhalika aliwahamasisha wapenda mchezo wa ngumi kujitokeza kwa wingi kwenda kuangalia pambano hilo ulingoni.
Kwa uhakika katika mabondia wenye ushawishi katika ukanda huu wa kusini mwa jangwa la sahara hauwezi kukosa jina lake likitajwa. Umaarufu wake uliibuka kwa kasi sana pale ambapo alipigana pambano katika mkoa wa Ruvuma pale ambapo alipigana na bondia machachari kutoka maeneo ya mbagala jijini Dar es salaam anayefahamika kama Shaban Kaoneka. Pambano hilo litaingia kwenye kurasa za mapambano ambayo yameacha alama katika mchezo wa ndondi katika ukanda wa afrika mashariki. Pambano hili lilikuwa ni pambano la utangulizi na wala sio pambano kuu lakini lilikuwa na msisimko ambao sio wa kawaida. Msisimko wake ulianza pale ambapo bondia Mandonga alianza kujibidhaisha(branding) kwa kutengeneza video fupi zikimwonyesha akifanya mazoezi ya hali ya ju na katika mazoezi hayo akawa anatoa jumbe zito ambazo alikuwa anatoa mkwara kwa bondia Kaoneka. Akatengeneza misamiati mipya katika jitihada zake za kujigamba kama vile “bendera kuzimu” “mtu kazi”, “mzizi wa mihogo” na kadhalika. Ubunifu wake wa kutengeneza misamiati hiyo ulinogesha pambano hilo na kufanya mashabiki wengi kulisubiria kwa hamu kubwa sana. Aliweza kuwaaminisha mashabiki wengi kwamba atamuuwa mpinzani wake. Ilipofika mda wa pambano mashabiki wengi hawakuamini macho yao namna bondia huyo alivyopigwa kwa urahisi bila ya kutoa upinzani wa aina yoyote ile. Kupigwa kwake kwa urahisi kukawa gumzo nchi nzima na vipande vya video ambavyo vinaonyesha namna alivyopigwa na kuanguka vikawa ni maarufu sana. Na alitoa kauli ya kuonyesha kwamba hajakataa tamaa pale aliposema kwamba “man don’t cry and sea never dry”. Kauli ile iliteka sana hisia za mashabiki na vyomvo vya habari vikaanza kumwalika katika vipindi mbalimbali kwa ajili ya mahojiano. Makampuni ya biashara nayo hayakukaa nyuma kwani nayo yakaanza kumtumia kama balozi kwa ajili ya kutangaza nembo zao za bidhaa.
Hali yamandonga ikaanza kubadilika kwani mapromota wakaanza kumpa mikataba ya mapambano akapelekwa mikoa mbalimbali kama vile kigoma, akajumuishwa kwenye tamasha la kiserikali la SENSABIKA ambapo akapewa mapambano dhidi ya mabondia mbalimbali. Makampuni ya biashara nayo hayakuwa nyuma yakaanza kumchukua kama balozi wa nembo za biashara zao na ikafiikia hatua hadi kuwa mojawapoo ya mgeni katika siku ya kilele cha YANGA DAY. Umaarufu huo ulizidi kukua mpaka wasanii mbalimbali kama Belle 9 na wengineo kuandika nyimbo za kumsifia bondia huyo. Hali hiyo ikamchukiza bondia Kaonekana na hadi uvumilivu ukamshinda hadi kuropoka kwenye vyombo vya habari hadharani na kuwatuhumu waandishi wa habari kwamba ni wanafiki kwani hawamuoji na kumpa nafasi yeye ambaye alishinda pambano na badala yake wanamuhoji Mandonga bondia ambaye amepigwa pambano na hakuwa na rekodi ya kushinda pambano. Aliongea kwa hisia kali ambapo alionyesha kuchukizwa na kitendo hicho. Na baadhi ya vyombo vya habari vilipomhoji mandonga akawajibu hiyo ni riziki na mda wake umefika wa kupata riziki kupitia mchezo wa ngumi.
Baada ya mda akawa anapata mapambano mengi kuliko bondia mwingine yeyote yule Tanzania na hata akawa anapambana nje ya mipaka ya Tanzania. Mojawapo ya pambano ambalo lilishika hisia za watu miongoni mwa mapambano yake ya ndani ya nchi lilikuwa pambano lake dhidi ya bondia Said Mbelwa alikuja na kauli mbiu ya ngumi inayoitwa “ndoige” ambayo kauli hii ilimfanya azidi kupata umaarufu hadi nje ya mipaka ya nchi. Kwa namna moja ama nyingine mapromota wakamtumia kwenda kuamsha ari ya mchezo wa ngumi nchini Kenya pale alipoandaliwa pambano dhidi ya bondia kutoka Kenya Daniel Wanyonyi na pambano lake hilo liligusa hisia za mashabiki wengi wa ngumi katika ukanda wa afrika mashariki na kati. Kauli yake ya “sugunyo” ikawa ya moto na ilibebwa na wapenda ngumi wengi katika ukanda huo na alipokelewa na mashabiki wengi sana na pambano lake liliuza tiketi zote hadi zikaisha mapema sana. Kupigana mapambano mengu kukamfanya apate upinzani wa kihoja kutoka kwa watu wengi sana ambao walianza kumsema kwamba kupigana kwake huko ovyo kutamletea matatizo ya ubongo huko siku za mbeleni. Hatua hiyo ilimpelekea akafungiwa kucheza ngumi za kulipwa kwa mda. Si mda mrefu sana toka afunguliwe na aliandaliwa mapambano machache na la mwisho lilikuwa la dhidi ya Mada Maugo na alipigwa na licha ya hivyo halijaweza kuwa lenye mvuto sana ukilinganisha na mapambano yake ya huko nyuma. Dalili zinaonyesha umaarufu wake umeanza kupungua kwa siku za hivi karibuni. Swali ambalo nakuachia msomaji wangu Je mtu kazi ameisha kazi?
Comments
Loading…