“Timu inakosa vitu vingi, haina njaa, ari, nguvu, hamasa wa ule utamaduni wa Manchester United kuwachachafya wapinzani. Old Traford imegeuka kuwa laini,”
“Tuko pamoja, mshikamano wetu ni mkubwa. Kuanzia wakurugenzi, wafanyakazi, benchi la ufundi na wachezaji wote tumeungana na nguvu yetu moja. Tunaelekeza nguvu kwa ajili ya matokeo mazuri ya timu. Wachezaji wamepania kufanya vizuri,”
Hayo yalikuwa maneno ya kocha wa Manchester United, Eric Ten Hag mara baada ya timu yake kushuhudia vipigo Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ten Hag anasisitiza mshikamano uliopo ndani ya timu ni mkubwa na matarajio ni makubwa hivyo Man United imepania kufanya vizuri. Mwishowe Ten Hag alisema anatambua kuwa timu haijapata matokeo mazuri hivi karibuni, lakini ana imani.
Wakati Ten Hag akisema hayo, staa wa zamani wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic katika mahojiano na Piers Uncensored alimshangaa kocha Ten Hag na kuhoji ikiwa anao uwezo wa kuongoza klabu hiyo. Zlatan alijaribu kutofautisha kati ya kuwa kocha wa Ajax Amsterdam na Manchester United. Hali kadhalika staa mwingine mkongwe wa zamani Kevin prince Boateng naye amehoji uwezo wa Kocha Eric Ten Hag, na kudai hakutenda haki kumwondoa Cristiano Ronaldo. “Timu inakosa vitu vingi, haina njaa, ari, nguvu, hamasa wa ule utamaduni wa Manchester United kuwachachafya wapinzani. Old Traford imegeuka kuwa laini,” alisema Boateng katika mahojiano na channel ya FIVE ya Rio Ferdinand ambaye ni staa wa zamani wa Manchester United.
UTAMADUNI WA MAN UNITED
Kama kuna mchezaji amezungumza kwa kina na hoja basi Kevin Prince Boateng amefukua mzizi wa tatizo la Man United. Kocha wa timu hiyo mwanzoni mwa sakata la Jadon Sancho alisema alipopewa ajira ya kuinoa Manchester United aliambiwa afanye kila anachoweza kubadili hali ya mambo ya klabu hiyo. Aliombwa kubadili utamaduni uliozoeleka miaka ya karibuni tangu kustaafu kwa Sir Alex Ferguson. Kimsingi hoja ya Boateng ina umuhimu mkubwa sana na kwamba kunatakiwa kufanyika mabadiliko makubwa ikiwemo kufuondoa wachezaji ambao wameshindwa kule mchango mkubwa kwa klabu yenyewe licha ya kukumbatiwa na kuaminiwa kuwa wana vipaji vya kusakata kandanda.
HAKUNA MSHAMBULIAJI
Marcus Rashford pamoja na kusfiwa kwa mengi lakini kijana huyu ahwezi kuwa mfumania nyavu mahiri. Uchezaji wake si wa nambari wala 10. Amechezeshwa pembeni alikolilia bado hajaonesha makali walau kufikia viwango vya mawinga wenye uchu na ushindi. Amepngwa winga wa kulia nako hakuna mafanikio. Antony Martial hawezi kuifikisha kokote Manchester United. Safu nzima ya ushambuliaji tangu ujio wa Eric Ten Hag hairidhishi, inahitaji kuongezewa nguvu zaidi. Licha ya ujio wa Rasmus Hojlund kuibua hamasa lakini safu ya ushambuliaji inahitaji wachezaji wapya wenye hadhi ya kuichezea Manchester United.
SAFU YA ULINZI NI MATOBO
ANDRE Onana ni mchezaji wa mwisho linapofika suala la hatari zinazoelekezwa langoni mwa Manchester United. Inawezekana amefanya makosa kadhaa lakini ni golikipa mwenye uwezo mkubwa. Tatizo la Manchester United safu ya ulinzi ni nyororo mno. Kwanza ni safu isiyoeleweka kombinenga yake. Wachezaji wanabadilishwa badilishwa kulingana na mechi. Lakini hata uwezo wao pia hauridhishi na kuifanya Man United kuwa na ukuta mgumu. idara ya Ulinzi imekuwa ikiyumba mara nyingi, si kwa mashambulizi angani (mipira ya krosi) wala ya kutandaza kandanda chini. Ni safu inayogeuzwa geuzwa kama chapatti.
VIUNGO BILA MABAO
Ubunifu wa safu ya kiungo mshambuliaji nayo iko chini. Utengenezaji wa mabao kwa Man United uko chini. Nahodha Bruno Fernandez anaonekana kucheza kama mchezaji huru, lakini bado hajaonesha kuwa anaweza kuipeleka mbele klabu hiyo. Hekaheka zake nyingi zinakosa wamaliziaji au kukosa kombinenga ya kiungo ushambuliaji ambayo ingeweza kuwalisha mipira mingi ya mabao w ashambuliaji. Ni eneo jingine ambalo linaonesha wazi klabu hiyo inatakiwa kufanya mapinduzi makubwan ya kiutamaduni na uchezaji ili kulinda hadhi ya klabu yao.
VIUNGO WALINZI
Carlos Casemiro kwa kawaida anahitaji washirika katika eneo la kiungo. Soafine Amrabat amesajili kwa mkopo kuisaidia eneo la kiungo la Manchester United. Lakini amekuwa akipangwa upande wa kushoto kutokana na wachezaji wa nafasi hiyo kuwa majeruhi. Ni Luke Shaw na Malacia. Lakini Amrabat anacheza eneo hilo ili kusaidia nafasi ya kiungo ambayo inahitaji kumsaidia Casemiro kuliko kumwacha akicheza peke yake. Ikiwa Casemiro anazidiwa na viungo wa timu pinzani maana yake injini ya timu inayumba na kuanguka. Hapo tayari unakuwa mzigo kwa mabeki. Tena kwa mabeki ambao uwezo ungali chini.
MABEKI WA PEMBENI
Mfumo wa Eric Ten Hag ni kama ule wa Mikel Arteta, Pep Guadiola au lilivyo soka la kisasa ambapo wengi wao wanatumika kuwa wabunifu katika kusaidia mashambulizi ya timu. Kwa maana hiyo mabeki wa pembeni wa Man United ukiondoa Luke Shaw, bado hawajaonesha umahiri katika kuzitumikia nafasi hizo. Ndiyo maana mchezaji mmoja akikosekana ni kama gharika kubwa hutokea kwenye kikosi chao.