Hull City yatoa kipigo cha mbwa mwizi..
Manchester City wamekamata uongozi wa Ligi Kuu ya England (EPL) baada ya ushindi mwembamba dhidi ya Crystal Palace.
Wakicheza nyumbani, vijana wa Manuel Pellegrini walipata ushindi wa 1-0 ambao ni mdogo kuliko yote waliyopata nyumbani na kadiri siku zinavyokwenda wanaonakena kuvutwa shati.
Bao la City lilifungwa na Edin Dzeko katika dakika ya 50, ambapo wenyeji walitawala katika kipindi cha kwanza na kipa wao, Joe Hart akaumia karibu na jicho.
Man City sasa wenye pointi 41 wapo pointi mbili juu ya Arsenal ambao Jumapili hii wanashuka uwanjani ugenini kumenyana na Newcastle.
Hadi sasa City hawajapoteza mechi katika uwanja wa nyumbani, lakini walikuwa na wakati mgumu mbele ya Palace ambao walicheza kwa kujihami sana.
Palace wamebaki nafasi moja juu ya zile za kushuka daraja baada ya Fulham kupata kipigo kizito cha 6-0 kutoka kwa Hull.
Katika mechi nyingine, Manchester United walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Norwich kwa bao la Danny Wellbeck, West Ham wakatoka sare ya 3-3 na West Bromwich Albion.
Astona Villa pia walikwenda sare ya 1-1 na Swansea kama ilivyokuwa kwa Cardiff waliotoka 2-2 na Sunderland.
Comments
Loading…