in , , ,

Man United, Man City zimejikatia tamaa

PAMBANO kati ya mahasimu wa jiji la Manchester limefanyika wikiendi hii ambapo matokeo yalimalizika kwa suluhu ya 0-0. Pambano hilo nje ya uwanja linaonekana kuw amaarufu kama mabapambano mengine ya debi za majiji. Kwa mfano dabi kama vile ya Simba na Yanga, AC Milan na Inter Milan au Liverpool na Everton zote za jijini Liverpool. 

Katika mapambano ya mahasimu wa jadi ni jambo la kawaida kukutana na hekaheka nje ya uwanja. Dabi nyingine huwa zinatisha ndani ya uwnaja na kuwafanya wachezaji kucheza chini ya presha kubwa. Mashabiki wanakuwa na kiu kubwa ya kuona wanaibuka na ushindi, viongozi wanakuwa kwenye hamasa ya kutaka timu zao zishinde. Lakini upo wakati zenyewe huwa hazishindi kwa sababu ya ubora wao ama kiwango cha chini.

Kuagawa Kevin De Bruyne

Katika pambano hili Kevin De Bruyne amecheza hadi mwisho wa mchezo. Ni mchezo wake wa mwisho wa dabi ya Manchester baada ya kutangaza kuondoka katika klabu yaMan City. Kiungo huyo katika mchezo huo alijaribu kuonesha umahiri wake, lakini ukweli wa mambo kikosi cha Man City kipo katika kiwango kibovu mno.

De Bruyne hakuwa na zile pasi zenye macho makali, ama mashuti yanayowatisha makipa wa timu pinzani. Lakini alionesha kuwa bado ni mchezaji anayweza kwenda hata Ligi ya Saudi Arabia na akacheza kwa muda mrefu. Kuagwa kwa KDB ni wazi Man City inatengeneza timu mpya ambayo huenda ikaonekana kuanzia msimu ujao. Hapo tunaweza kusema kwaheri.

Kuporomoka kwa timu za Manchester

William Shakespeare, nguli wa fasihi aliwahi kusema kila kitu kizuri lazima kifike mwisho wake. kwa timu za Manchester, kiwango bora, mataji ya kutosha na tuzo mbalimbali z awachezjai binafsi zilimiminika katika nyakati tofauti kwenye jiji hilo. Alex Ferguson aliifanya Man United kuwa timu tisho, lakini tangu alipoondoka mwaka 2023 timu hiyo imekuwa ikihaha kurudi kwneye makali yake. 

Man City ambayo ilikuwa kwa miaka mingi ilikuwa msindikizaji lakini tangu ilipompata mmiliki mpya ilibadilka kuwa tishio. Kuanza kwa Pellegrini, Roberto Mancini hadi Pep Guardiola kwa nyakati tofauti wameifanya timu hiyo kuwa moto w akuotea mbali. Msimu wa huu timu za jiji la Manchester zimepitia nyakati ngumu na vipigo vingi kuliko ilivyotarajiwa. Makocha wote wawili, Ruben Amorim ambaye amepokea timu katikati ya msimu toka kwa Eric Ten Hag huku Pep Guardiola akiona hali ngumu kwenye kikosi chake, umeonesha jinsi timu hizo zilivyopromoka kisoka. 

Wachezaji wameingia na kutoka katika klabu ya Man United, lakini kule Man City wachezaji wao karibu wote wapo, lakini sio wale ambao walitetemesha EPL na UEFA tena. Man City imekutana na vipigo visivyotarajiwa kuanzia EPL hadi UEFA ikiwemo cha 4-1 dhidi ya Sporting Lisbon wakati ikifundishwa na Ruben Amorim. 

Katika mechi nyingi wachezaji wake wameonesha kuchoka na kupoteza hali ya kujiamini na kuifanya timu kuwa nyanya mbele ya wapinzani wao. Swali ambalo linapaswa kuuulizwa sasa ni je timu za jiji la Manchester zitaweza kurudi kwenye ubora wao wa awali? Hili ni jambo la kusubiri nma kuona.

Mzigo wa kuwatema wachezaji

Makocha wote wawili wanakabiliwa na mzigo wa kuwatema wachezaji ambao wanaonekana kushindwa kurejesha viwnago vyao ama wamefika ukomo wa uwezo wao katika soka. Ruben Amorim alimwondoa Marcus Rashford na kumpeleka kwa mkopo Aston Villa ambako ameanza kuonesha cheche zake. 

Kumekuwa na mjadala kuhusu uamuzi huo, lakini Amorim amekiri kuwa hakuna namna nyingine ya kuisaidia timu yao kama kubadilisha mambo kikosini ikiwemo kuachana na baadhi ya wachezaji. 

Mzigo wa uamuzi wa kuachana na wachezaji unamkabili pia Pep Guardiola ambapo anaelekea kuwakosa Kevin De Bruyne, Ilkay Gundogan, Kyle Wlaker, Ederson na Bernado Silva ni miongoni mwa wachezaji ambao wanatarajiwa kuondoka kikosini hapo.

Mbinu zenye hofu

Katika mchezo wao wa jumapili timu zote zilikuwa zinajilinda kwa kutumia mabeki watano (5-2-2-1) ili kutoruhusu bao. Man United walipokuwa wanashambuliwa walitumia mfumo w amabeki watano huku viungo watatu wakiranda randa nje ya eneo lao la 18. Mbinu hii ilikuwa na malengo ya kuzuia kupachikwa bao lolote na inaweza kufafanuliwa ni kujihami. Wakati Man United wakijihami hivyo, Man City hawakuwa na makali yoyote yaliyozoeleka kwani mashambulizi yao mengi hayakuwa yakipangiliwa kama ilivyo kawaida yao. 

Viungo hawakuwa na ubunifu ule uliozoeleka wala safu ya ushambuliaji ikiwa na Omar Marmoush haikuwa tishio kwa Man United. Kipindi cha pili timu zote zilishambuliana kwa zamu, lakini Man United walionekana kutamani kupata angalau bao la kuongoza. Hata hivyo hawakuwa na maarifa ya kupenya ngumo ya Man City iliyokuwa inaongozwa na Ruben  Diaz. Kimsingi pambano hili lilijaa hofu ya kutofungwa, mbinu zilizkuwa za kujilinda angalau kupata alama moja tu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

17 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Simba wana Kombe la Shirikisho mkononi

Tanzania Sports

Kuna siri moja kwa Simba