in , , ,

Man United kwenye mstari wa kushuka daraja

MARA baada ya mchezo kati ya Manchester United na Arsenal, fikra zangu zilikwenda mbali hadi kuikumbuka Leeds United na Juventus Turin ya Italia. Vilabu hivi viwili ni vikongwe ambavyo vimewahi kupitia dhahama kubwa kwenye mchezo wa soka. Si kwamba Man United walikuwa wabaya kwenye mchezo wao na Arsenal lakini kama wahenga waswahili walivyosema mzaha mzaha hutumbua usaha, ndicho naweza kusema. 

Leeds United ilivuma, ilitetemesha vigogo, ilizalisha vipaji vya hali ya juu, lakini ikaporomoka kidogo kidogo hadi kupotea Ligi Kuu. Tukibaki hapahapa England, West Ham ni klabu yenye kila sifa ya ubora kuanzia shule ya soka hadi uzalishaji wa vipaji wamesifika sana. halafu unaweza kuongeza timu kama Nottingham Forest, Aston Villa, Crystal Palace ama hata Reading kama timu kongwe mchezo wa soka England. Ni timu hizo ndizo zilikuwa zikichachafya miaka 1980 na mwanzoni mwa miaka 1990, lakini zikaja kupotea kwenye umahiri wao. 

Nchini Italia Juventus haikupotea sana lakini kilichowakuta hadi kushushwa daraja ndicho nataka kukifananisha na Man United. Juventus walikuwa na kesi tofauti, kwani wao walikutwa na makosa ya kupanga matokeo, hivyo walikatwa pointi pamoja na kushushwa daraja. Juventus walikubali kushuka daraja, huku wakipnguza kiwango cha mishahara ya wachezaji ambao baadhi yao waliamua kuhama na wengine walikubali kulipwa nusu mshahara. 

Fikiria kama mchezaji analipwa pauni 100,000 kwa wiki maana yake alipunguziwa hadi 50,000 kwa wiki. Waliobaki kama akina Pavel Nedved na Gianluig Buffon walipendwa zaidi na mashabiki wao kwa kile walichokionesha. Nataka kusema Juventus walishuka kimzaha mzaha tu, kwani wadau wa soka hawakutegemea.

Sasa tukirudi kwa Man United, hawakucheza vibaya dhidi ya Arsenal, lakini kuna kitu kimeondoka katika klabu hiyo ambacho kwa lugha ya kiingereza kinaitwa “Passion’. Timu nzima inaonekana kama vile haina “passion’. 

Mfano Arsenal tangu mwanzo walikuwa wanacheza mchezo wao wa kasi, aria ma uchu fulani na kukamia mchezo. Unawaona kabisa Arsenal wanataka kufanya kitu, na wanaucheza mpira na kuamrisha ufanye watakavyo. Bahati mbaya lango la Man United halikuruhusu bao. 

Kwa Man United unawaona wanacheza ili kuziba mianya tu, ni timu ambayo iko mbali na “passion”. Wanapiga pasi nyingi, lakini wanakoelekea ni wapi? Wamesajili wachezaji walioamini wataleta mafanikio lakini baadhi yao kwa hakika hawakustahili. 

Angalau kocha wao mpya Ruben Amorim anawaambia wana matatizo ya vipaji ndiyo maana hata benchi huwa anawaweka makinda wengi kutoka timu B. ule umwamba wa Man United umepotea kidogo kidogo. Ile hofu waliyokuwa nayo wapinzani wanapokuja dimba la Old Trafford imepungua kwa kiasi kikubwa. 

Ni kama vile wapinzani wanajua tatizo hili, na Man United wanachelewa sana kutatua matatizo ya ndani. Unapokuwa na klabu inayoweza kufukuza wafanyakazi 250 kwa sababu ya matokeo ya ndani ya uwanja ambayo yanapunguza mapato ni dhahiri hali si shwari. Kuanza kupunguza gharama maana yake timu inakusanya mapato ambayo hayakidhi kuhudumia kila kitu. 

Man United imebaki kuwa klabu yenye ushawishi nje ya uwanja lakini ndani kuna changamoto nyingi zinazotakiwa kurekebishwa. Kwa mfano wanaposhambuliwa huwa wanatumia mfumo wa 4-4-2 ili kuimarisha ulinzi na kurudisha 5-2-2-1. Hadi leo hawana mchezaji tegemeo wa kumaliza mechi. Ni timu inayoundwa bila silaha ya mwisho ambayo ingeweza kuwasaidi kumaliza mechi nyingi yaani kuwapa ushindi. 

Tanzania Sports
Msimamo wa Ligi kuu ya England, baada ya mzunguko wa #28

Wachezaji wenye silaha za kuamua matokeo hawapo, mawinga hawapo, washambuliaji hawapo na badala yake wachezaji waliopo si  wote wenye kuhangaikia kuireudisha Manchester United kwenye mstari wa mafanikio. Jitihada za wachezaji hazikileti matokeo mazuri na kuifanya timu hiyo kama vile inahangaika kutoshuka daraja. Hapo ndipo yanakuja mawazo, kimzaha mzaha hivi Man United inaweza kushuka daraja. 

Katika mechi zao kila wanapocheza iwe ushindi ama sare huwa wanashika nafasi ya 13, 14, 15. Kama wanashika nafasi ya 15 maana yake ni nn za juu katoka mstari wa kushuka daraja. Kwa  maana hiyo kuanzia nafasi ya 17, 18, 19 na 20. Timu zinazokuwa kuanzia nafasi ya 15 zinapambana kutoshuka daraja. Sasa Man United ikishika nafasi ya 15 maana yake bado ipo hatarini kushuka daraja. 

Katika mazingira hayo, Man United inajikuta kwenye changamoto kuu tatu; kuonesha umahiri wa kocha wao Amorim, kutoshuka daraja, na kulinda hadhi ya klabu ya Man United yenyewe. Katika mazingira haya ni dhahiri timu inapitia nyakati ambazo wachezaji wengi  mahiri watakuwa wanaikwepa kwa vile haielekei kuwapa ndoto zao za ubingwa bali kupambana kutoshuka daraja. Hii ni timu ambayo ilikuwa inaogopeka. Hii ni timu ambayo imekuwa ikifukuza makocha wengi sana, lakini matatizo yao yapo palepale. Kwa walipofikia sasa, Man United wanapaswa kuwa na roho ngumu, vinginevyo wataula wa chuya.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Siku ya burudani na malalamiko imewadia

Tanzania Sports

LIGI KUU IHESHIMIWE