in , , ,

Man U wamekaa vibaya

*City, Arsenal wavutwa shati

Ilikuwa ni kama udhalilishaji kwa Jose Mourinho aliporudi Stanford
Bridge Jumapili hii akiwa na Manchester United, kwa jinsi alivyopokea
kichapo cha 4-0 kwa Chelsea katika mechi ya Ligi Kuu ya England (EPL).

Mitandao ya jamii imejaa kejeli kwake na wachezaji wake, baadhi ya
picha zikionesha Chelsea kama jogoo na Man U mtetea, nyingine
zikionesha nyani aliyejificha ndani ya gunia lenye chapa ya
Manchester.

Wanasema yeye si ‘The Special One’ tena na kwamba huenda kocha mpya wa
Chelsea, Mtaliano Antonio Conte akamsababishia madhara. Lakini
walionekana wakinong’onezana mawili matatu baada ya mechi hiyo. Ni
Mourinho huyu huyu aliyefutwa kazi na Chelsea msimu uliopita na
kuchukuliwa na Man U kubeba mikoba ya Louis van Gaal.

Ajabu ni kwanba Manchester United walitawala mchezo kwa asilimia 56,
tena wakipiga mashuti mengi kuliko wapinzani wao, lakini hawakupata
bao na wakaishia kuloweshwa jinsi hiyo.

Iliwachukua Chelsea sekunde 30 tu kufunga bao kupitia kwa Pedro
kutokana na makosa ya walinzi, Garry Cahil akafunga la pili baada ya
United kuruhusu kona yake kuingia kwenye eneo boksi lao.

Arsenal waliambulia sare ya 0-0
Arsenal waliambulia sare ya 0-0

United hawakuonekana kufanyia kazi makosa yao kiulinzi na wakamwacha
Eden Hazard kufunga kutoka yadi 15 na beki N’Golo Kante alipanda na
kushindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la United.

Kwa ushindi huo Chelsea wanakuwa pointi moja tu nyuma ya Manchester
City na Arsenal wanaoongoza kwa pointi 20 sawa na Liverpool. Tottenham
Hotspur nao wana pointi 19 sawa na Chelsea, hivyo kuonesha mchuano
kuwa mkali miongoni mwa timu tano za juu, kwani tofauti iliyopo ni
pointi moja tu.

Arsenal walipoteza nafasi ya kuwa juu kwa wiki hii baada ya kubanwa na
Middlesbrough Jumamosi na kwenda sare nyumbani Emirates, wakati kocha
wao,m Arsene Wenger akitimiza miaka 67 ya kuzaliwa.

Kukosekana kwa Santi Cazorla kwenye kiungo ni sababu kubwa ya hali
hiyo, kwani rekodi inaonesha kwamba mechi anazocheza hushinda zaidi
ikilinganishwa na zile ambazo hayupo. Ana majeraha kidogo lakini
alitarajiwa angekuwa timamu, ila ikabidi apumzishwe asije kujitonesha
zaidi.

Manchester City walioanza ligi vyema nao waliendelea na mdororo wao
kwa kwenda sare ya 1-1 nyumbani Etihad walipocheza na Southampton.
Katika mechi nyingine wikiendi hii, Everton waliduwazwa nyumbani kwa
Burnley kwa kufungwa 2-1 huku Hull nao wakiteseka nyumbani kwa
kufungwa 2-0 na Stoke.

Mabingwa watetezi, Leicester, wanaofanya vyema kwenye Ligi ya Mabingwa
Ulaya walianza kufufuka kwenye EPL kwa kuwararua Crystal Palace 3-1,
Swansea wakatoshana nguvu na Watford kwa 0-0, West Ham wakaanza kupata
nguvu kwa kuwafunga Sunderland 1-0 na Liverpool wakashinda 2-1 dhidi
ya West Bromwich Albion.

Baada ya mechi tisa kila timu, Sunderland wamebaki mkiani wakiwa na
pointi mbili, Swansea wanazo tano na Hull wana saba. Stoke kwa ushindi
wao wamejinasua kwenye eneo la kushuka daraja wakati sare ya
Middlesbrough kwa Arsenal nayo imewasaidia kupata pointi saba sawa na
Hull.

Middlesbrough wana tofauti ya mabao 10 na Hull ambao ndio waliofungwa
mabao mengi zaidi katika ligi hii, licha ya kuianza vyema.
Walitarajiwa wafanye vibaya kwa sababu hawakufanya usajili wa maana na
walianza bila hata kuwa na kocha.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Ushindani mkubwa EPL

Tanzania Sports

Mkutano Arsenal pasua kichwa