in , , ,

Man U kutosajili hovyo

*Loic Remy akwama Liverpool
*Chambers asajiliwa Arsenal

 

Kocha wa Manchester Utd, Louis van Gaal amesema atachukua muda kusajili wachezaji wapya licha ya kwamba wanahitajika.

Mdachi huyo amesema kuna mtu alijaribu kuivunja timu hiyo lakini akawahi kusema kwamba si Sir Alex Ferguson, hivyo kuna kila dalili kwamba alikuwa akimsema David Moyes.

Van Gaal ametumia mfumo wa 3-4-1-2 katika mechi za kwenye ziara ya kabla ya msimu nchini Marekani, na amesema wazi kwamba bado kikosi hakina uwiano unaostahili.

Changamoto iliyo mbele yake ni kuchota kutoka kwa akina Wayne Rooney, Juan Mata na Robin van Persie wanaoonekana kuwa muhimu katika kuirejesha timu hiyo kwenye uimara wake iliopoteza chini ya Moyes.

Mdachi huyo amesema kwamba anaweza kuwatumia hata Javier Hernandez, Danny na Will Keane kama washambuliaji wakati na kuwa Rooney anawezea namba 10, tisa au hata saba au 11 kwenye wingi.
Mchezaji wao, Rafael, ameumia na kuondoshwa kwenye ziara hiyo kwa ajili ya kurudi Uingereza kupata matibabu.

LOIC REMY AKWAMA LIVERPOOL

Mshambuliaji wa Queens Park Rangers (QPR), Loic Remy amekwama katika safari yake ya kujiunga Liverpool.

Mchezaji huyo aliyesafiri na familia kujiunga na vijana wa Brendan Rodgers anadaiwa kwamba hayupo fiti baada ya kuchukuliwa vipimo vya afya.

Remy alikuwa ajiunge Arsenal lakini akadai mshahara mkubwa mno ambao Arsene Wenger alikataa, ndipo Rodgers akamchukua lakini sasa amekwama.

Mchezaji huyo ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo Newcastle, aliingia Uingereza akitoka Marseille ya Ufaransa na ni mpachika mabao mahiri aliyekuwa pia na Timu ya Taifa ya Ufaransa majuzi nchini Brazil.

Hata hivyo, kocha wa QPR, Harry Redknapp amesema haamini kwamba mchezaji huyo amekwama kwa sababu ya afya, kwani amekuwa fiti tangu Marseille hadi London.

Redknapp alishakubaliana na Liverpool mauzo ya mchezaji huyo kwa kiasi cha pauni milioni 8.5.
Remy (27) ambaye amekuwa akitaka klabu inayocheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu ujao alikwama rasmi juzi nchini Marekani lakini Redknapp anasema kuna sababu nyingine ambayo Liverpool hawataki kuitaja.

Alifunga mabao 14 katika mechi 27 alizochezea Newcastle msimu uliopita na Redknapp anasema kukwama kwake huko ni faraja kwa QPR kwa sababu ni mchezaji muhimu ambaye alisema tangu msimu uliopita anaweza kufunga hata mabao 20.

CHAMBERS AJIUNGA ARSENAL

Arsenal wamemsajili mchezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana ya England, Calum Chambers kutoka Southampton kwa pauni milioni 16.

Chambers (19) anaweza kucheza kama beki wa kulia na kati huku akiwa na uwezo mkubwa wa kusukuma mashambulizi.

Kocha Wenger amesema kwamba kijana huyo alizoea haraka Ligi Kuu ya England msimu uliopita na kuonesha kiwango kikubwa cha soka.

Arsenal pia wameulizia juu ya uwezekano wa kumsajili kiungo Mfaransa Morgan Schneiderlin (24) kutoka klabu hiyo hiyo.

Chambers anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa msimu huu baada ya mshambuliaji wa Barcelona, Alexis Sanchez, beki wa kulia wa Newcastle, Mathieu Debuchy na kipa wa Nice, David Ospina.

Chambers ameondoka na kikosi cha Arsenal pamoja na Debuchy na Ospina – kwa ajili ya mazoezi nchini Austria. Sanchez alitarajiwa kuwasili kwenye uwanja wa mazoezi wa Arsenal ulipo Colney Jumanne hii.
Kuwasili kwake kunaweza kuharakisha kuondoka kwa beki wa kati na nahodha, Thomas Vermaelen anayetakiwa na Manchester United.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Kipa Ospina asajiliwa Arsenal

La Liga kuibomoa England