MSIMAMO wa Ligi Kuu ya England (EPL) katika nafasi tano za juu umebaki
bila kubadilika baada ya baadhi ya mechi za mzunguko wa 26.
Huku timu zilizo juu kabisa zikiwa bado na mechi 25, Jumamosi
imeshuhudia Manchester United wakifungwa 2-1 ugenini walikocheza dhidi
ya Sunderland.
Yalikuwa matokeo ya kusikitisha kwa kocha Louis van Gaal ambaye sasa
anasema kwamba huenda vijana wake wakaishia kucheza Ligi ya Europa
msimu ujao kutokana na kuzidiwa nguvu.
Sunderland waliongeza matumaini yao ya kujinusuru na kushuka daraja
baada ya Wahbi Khazri kutangulia kufunga bao dakika ya tat utu kwa
mpira wa adhabu ndogo ambao ulienda wavuni moja kwa moja.
Anthony Martial wa Man U alisawazisha akimzidi nguvu kipa wa zamani wa
Arsenal, Vito Mannone, aliyekuwa ameutema mpira wa Juan Mata.
Sunderland wanaofundishwa na Sam Allercyice ‘Big Sam’ hawakukubali
kuwaangusha watazamaji waliofika kuwaunga mkono, kwani Lamine
Konealifunga kwa kichwa kizuri mpira wa kona wa Khazri ambapo
ulimgonga kipa David de Gea na bao kuandikwa kwa jina la kipa huyo.
Huu ulikuwa ushindi wa kwanza katika EPL kwa Sunderland dhidi ya
Manchester United hapo kwenye Stadium of Light katika mechi 14.
United sasa wana pointi chache zaidi katika wakati kama huu kuliko
ilivyopata kuwa nazo kwenye EPL misimu iliyopita
Katika mechi nyingine, Chelsea wamevuna mabao matano dhidi ya
Newcastle na kuwatupa kwenye eneo la kushuka daraja, Chelsea walifunga
kupitia kwa Diego Costa, Pedro mawili, Willian na Bertrand Traore.
Newcastle walifuta machozi kupitia kwa Andros Townsend.
Katika mechi nyingine, Bournemouth wakiwa nyumbani walinyukwa na Stoke
3-1, Crystal Palace wakaangukia pua kwa 2-1 walipowakaribisha Watford.
Everton waliongea idadi ya timu zilizofungiwa nyumbani kwani walikula
1-0 kutoka kwa West Bromwich Albion sawa na Swansea kwa Southampton
wakati Norwich walilazimisha sare ya 2-2 mbele ya West Ham.