in , , ,

Man City wanaweza kuzuia kishindo cha Liverpool?

HAYAWI hayawi sasa yamekuwa ambapo bingwa mtetezi wa Ligi Kuu England (EPL), Manchester City wakiongozwa na Pep Guardiola watakuwa na kibarua kigumu ya kuzuia kishindo kikali cha Liverpool msimu huu. Liverpool wakiwa chini ya Arne Slot wanaongoza kwenye mashindano karibu yote. 

Kwenye Ligi ya Mabingwa wao ndiyo vinara kisha kwenye Ligi Kuu pia wanaongoza kwa tofauti ya Pointi 8. Lakini Manchester City wanalo jukumu la kupunguza pengo la pointi baina ya miamba hiyo kutoka EPL.  Tangu alipoanza kazi ya kuinoa Liverpol Arne Slot ameifanya kuwa timu imara na yenye kuwavutia wengi kila inapocheza. Jinsi wanavyouchukulia mchezo, mbinu zao, uwezo wao na nguvu walizonazo kuwadhibiti wapinzani wao ni habari nyinine kabisa. Kocha huyo jinsi alivyoichukua Liverpool kutoka kwa Jurgen Klopp ambaye ni kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo inaonesha jinsi mrithi huyo alivyotazama kazi iliyoandaliwa na Mjerumani huyo. 

Tanzania Sports
Mara ya mwisho hizi timu kukutana VAR ilikuwa gumzo

TANZANIASPORTS katika tathmini yake imebaini silaha za siri za Liverpool ambazo zimeifanya timu hiyo iweze kung’ara msimu huu, ambapo jumapili leo Man City watakuwa na kibarua cha kufuta aibu ya kufungwa mechi ya sita mfululizo,kupunguza pengo la pointi,kuvunja mwiko wa kutofungwa kwa vijana wa Arne Slot. Liverpool wao watakuwa na kazi ya kuhakikisha wanaeneleza ubabe na kuongeza pengo la poinbti kati yao na wapinzani wao.

Siri ya Van Dijk

Katika mchezo wa miamba hiyo, Man City wanapaswa kufahamu kuwa hakuna nafasi ya kumpa beki wa kati na nahodha wa Liverpool, Virjil van Dijk kukokota mpira kwa muda mrefu hadi eneo la hatari kwani amekuwa silaha muhimu ya kupata ushindi kwa timu yake. Beki huyo wa Liverpool amekuwa akitumia ujanja wa kupiga mipira mirefu kwenda kwa Mohammed Salah ambao unavuka eneo la viungo. 

Kwa kawaida inategemewa pasi ipigwe kwenda kwa viungo kisha wao watengeneze mbinu za shambulizi. Lakini hali ya mambo ni tofauti pale mpira unapokuwa miguuni mwa Van Dijk ambaye hupiga pasi ndefu yadi 40 kwenda kwa winga wao Mohammed Salah. Tumeona mbinu hiyo ikitumika jumatano wiki hii dhidi ya Real Madrid, ambao walijikuta wakiwa wamesambaratishwa zaidi na kukosa mwelekeo sahihi wa kudhibiti kasi ya Liverpool.

Miguu na maarifa ya Ryan Gravenberch

Nyota huyu anayo aina yake ya upigaji wa chenga na kuwatoroka maadui. Huwa anapokea mpira na kuwapiga chenga ya mwili na kuwazunguka kisha kutoa pasi haraka. Ryan husimama mbele ya safu ya ulinzi akiwa linda dhidi ya hatari zozote kuelekea kwao. Ni mchezaji ambaye Man City watanakiwa kumchunga kwani hawana mtu wa aina yake. Gravenberch atakuwa eneo la kiungo mkabaji sambamba na Curtis Jones ambaye amekuwa mchezaji wao mzuri sana msimu huu, pamoja na Alexis Mac Allister, kwa pamoja wanaunda safu ya kiungo imara zaidi na kuipa uhai Liverpool kutamba dhidi ya timu yoyote.

Silaha ya Beki wa kulia

Imezoeleka nafasi hiyo ikichezwa na Joe Gomez na Trent Alexander Arnold, lakini katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa, kocha wa Liverpool alimpanga Conor Bradley. Kinda huyo alikabiliana vilivyo na nyota wa kimataifa wa Kifaransa Kylian Mbappe. Katika mchezo wote Conor Bradley alionesha umahiri na ukomavu mkubwa huku kiwango chake kikiwavutia mashabiki na wachambuzi wa soka barani Ulaya. 

Uchezaji wake uliwachanganya Real Madrid, kwani licha ya kucheza kama beki wa kulia alikuwa na jukumu la kuingia eneo la kiungo na kuongeza kuwa na viungo wanne badala ya watatu. Hii ni silaha nyingine ya siri inayotumiwa na Liverpool kutokea pembeni-nyuma kulia. Mbinu hi inawaongezea kasi ya mchezo, kwnai hata wakati alipofunga bao la kwanza dhidi ya Real Madrid kulitokea gonga safi kati ya Bradley,Jones na Mac Allister akamalizia kazi nzuri na yenye kasi. Kwahiyo Man City wanakabiliana na mpinzani ambaye ana maarifa ya hali ya juu na kasi kubwa ya mchezo anapotafuta ushindi.

Rodri ni mchawi wa Man City?

Tanzania Sports

Wengi wanaamini Man City imekuwa mbovu hadi kufungwa mechi tano mfululizo, lakini hawasemi lolote kuhusiana na uamuzi wa kumwondoa mchezaji wa akiba Kalvin Philips ambaye alisajiliwa kutoka Leeds United lakini akakosa namba ya kudumu wala kutumika katika mechi ambazo Rodri alitakiwa kupumzishwa.

 Hata hivyo Rodri imedhihirika ni mchezjai wao muhimu na alihitajika mchezaji wa kusaidia baadhi ya mechi. Sasa jumapili hii wanakwenda kwenye dimba la Anfield huku wakitakiwa kuleta majibu ya kukosekana kwa nyota wao na mshindi wa tuzo ya Balon D’or. Mashabiki na wachambuzi wa kandanda wanatamani kuona namna Pep Guardiola anavyoleta majibu ya swali la nani anachukua nafasi ya Rodri mbele ya wapinzani wakali kama Liverpool.

Makosa binafsi

Baadhi ya mechi ambazo Man City anafungwa hutokana na makosa binafsi. Kwa mfano wiki hii Man City walikuwa mbele kwa mabao 3-0 dhidi ya Feyernood ya Uholanzi kwenye Ligi ya Mabingwa, lakini dakika 90 za mchezo zilipomalizika matokeo yalikuwa 3-3. Huu ni wakati wa Man City kusimama pamoja na kushikamana, kwani wachezaji wanaofanya makosa ni wengi. Hata golikipa wao namba moja Ederson huwa anafanya makosa na mengine yalionekana kwenye mchezo dhidi ya Feyernood. 

Mastaa wa Man City wanaaminika?

Kocha Pep Guardiola ana changamoto ya kuchagua wachezaji wa kuwaamini. Kikosi chake kimeyumba kutokana na majeruhi lakini pia kimekuwa kikicheza chini ya kiwango huku baadhi ya nyota wao wakiporomoka kiuwezo kwa kiasi kikubwa. Mfano Kevin De Bruyne ni miongoni mwa nyota wanaozungumziwa kushuka kiwango hivyo kumuumiza kichwa kocha wao, kutafuta suluhisho na kuimarisha timu. 

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Taifa Stars

Rekodi ya COSAFA kwenye AFCON 2025

Taifa Stars

Safari ya Tanzania katika mapinduzi ya michezo