*Wapigwa faini, kuwekewa zuio
Mabingwa wa England, Manchester City wametiwa hatiani kwa kwenda kinyume cha matumizi ya fedha katika soka na sasa wameadhibiwa.
City watatakiwa kutaja kikosi cha wachezaji 21 tu kwa ajili ya Ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao na pia hawaruhusiwi kutumia zaidi ya pauni milioni 49 kusajili wachezaji wapya.
Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa) limewapiga City faini ya pauni milioni 49 na mishahara kwa wachezaji wake kwa msimu wa 2014/15 haitakiwi kuzidi ile ya msimu huu.
Klabu hiyo imetoa kauli kwamba hata mwaka huu ilitaja kikosi cha wachezaji 21 tu kwa ya UCL, haikuwa ikitarajia kutumia zaidi ya pauni milioni 49 kwa usajili wala kuongeza kiasi cha mishahara, jambo ambalo linaonekana kama ni kujikosha tu.
City wanajulikana kwa kutumia fedha nyingi kwenye usajili kwa kujikusanyia wachezaji nyota ambapo tayari inaelezwa wameanza kusaka kwa ajili ya msimu ujao.
Kanuni hizo za Fair Play zinasema kwamba klabu hazitakiwi kutumia kiasi kikubwa cha fedha kuliko zinachozalisha na zinatakiwa kutimiza matakwa ya uhamisho wa wachezaji na malipo ya waajiriwa wake muda wote.
Man City wamekuwa wakitumia fedha kutoka mfukoni mwa wamiliki ambao ni matajiri wa nchini Qatar, jambo linaloonekana na klabu nyingine kwamba si haki.
Mabingwa wa Ufaransa, Paris St-Germain waliokwenda kinyume na kanuni hizo nao wamepata adhabu sawa na ya City.
Comments
Loading…