Ni timu gani ya EPL inafanya usajili mzuri? Timu ipi inaambulia usajili mbaya? Ni usajili upi unaoshangaza zaidi? Mchezaji gani mpya anapanda bei ya mauzo yake? je, usajili wa bei mbaya ni chanzo cha mchezaji kufanya vibaya? Je, ni nani anayefukuzia kila hatua ya mchezaji kuhamia timu fulani?
Hayo ni miongoni mwa maswali ambayo yanaulizwa na wadau wa michezo wakitaka kufahamu undani wa usajili wa wachezaji kila dirisha la usajili linapofunguliwa hadi kufungwa kwake. Wanataka kufahamu kinachokuwa nyuma ya pazia.
Baada ya usajili kadhaa kufanyika sehemu mbalimbali za miji inakotoka klabu inayoshiriki Ligi Kuu England kufumngwa jumatatu ya wiki iliyopita, Tanzaniasports, imefanya uchunguzi na kupata majibu ya maswali hayo yote hapo juu kupitia mawakala wa wachezaji ambao ambao wanasimamia dili za usajili wa wateja wao.
Kwa siku kadhaa, Tanzaniasports imetumia maswali 15 kuwauliza mawakala 18 kwa nyakati tofauti, na kwa masharti ya kutotajwa majina yao walikubali kuzungumia undani wa dili za usajili kiungwana na kubainisha kinagaubaga.
Aidha, tumewauliza ikiwa wanapokea kitita kikubwa cha fedha kuliko uhalisi wa kazi yao, kutokana na malalamiko yaliyotolewa na Gary Lineker mwanzoni mwa wiki hii ambaye amedai kuwa ni wakati sasa sheria,kanuni na taratibu za usajili wa wachezaji zibadilike, kwani mawakala wanatakiwa kulipwa na upande mmoja tu, badala ya sasa ambapo wanalipwa fedha na pande
nyingi kwenye usajili mmoja. Sahau kuhusu “nioneshe fedha”. Ni wakati wa kuwaonesha majibu.
1.Usajili upi ni bora zaidi?
“Kwa kuzingatia kuongeza hadhi ya klabu, hisia za kupenda na utayari wa kulipa, nafikiri inachukua mapigo kadhaa; mpango wa muda mrefu unaweza usilete faida katika timu, lakini mpango mfupi unahitaji kuangalia matokeo yaliyopo tayari kwa sasa. Ni mchezaji nyota, ameshajijenga tayari. Everton haisajili wachezaji waliokataliwa na timu sita za juu, wamesajili mchezaji wa kiwango cha juu kama yuko bora kiafya na anahamasishwa”
Huo sio wakati ambao James Rodriguez, ambaye amekuwa chachu ya mwanzo mzuri wa Everton katika msimu wa 2020/2021, kutajwa katika dili la usajili wa klabu hiyo yenye makazi katika viunga vya Merseyside.
Nyota huyo kutoka Colombia amepata asilimia 22 ya kura kutoka kwa mawakala. “Amefanikiwa kuiboresha Everton na amewafikisha kwenye ngazi nyingine ya juu,” anasema wakala mmoja.
Ingawaje nyota wa Liverpool Thiago Alcantara ameibuka na asilimia 28 ya usajili bora zaidi, “Mchezaji mahiri kabisa amepatikana kwa bei ndogo na dau lake lilipangiliwa vema.” Anasema wakala mwingine, na kumekuwa na sifa kedekede kutoka Everton kuhusiana na usajili wa Thiago.
“Allan yupo Everton anaongeza ubora kwenye klabu hiyo. Angalia takwimu zake akiwa Italia jinsi anavyopora mipira kutoka kwa wapinzani wake. Ni matunda ya fedha waliyolipa kupata huduma inayowapa wanayohitaji katika timu yao,” anasema wakala mmoja.
”Allan kwa Everton, kuanzia vyumba vya kubadilishia nguo, uwepo wake uwanjani, yuko upande huu au ule, lazima akuoneshe ubora wake. Carlo Ancelotti anamfahamu kijana huyo na hakika atapandisha thamani ya Everton kwa sasa,” anaongeza wakala mwingine.
Mawakala wengi wameitaja klabu ya Newcastle United imetoa fedha ambazo zimeleta huduma mzuri kutoka kwa Callum Wilson, mshambuliaji asiyetia shaka EPL kutoka Bournemouth kwa pauni milioni 20. Upande mwingine dili la usajili lililotazwa ni ujio wa Gareth Bale katika klabu ya Tottenham Hotspurs, “kwa sababu kinachomaanisha kwa Spurs na Mourinho wametaka usajili huo uende kwao” na Thomas Partey kujiunga Arsenal siku ya kufungwa dirisha la usajili. Mawakala wamemwita Thaoms Partey ni bingwa wa kubadili matokeo.
2. Je, upi ni usajili mbovu zaidi katika dirisha hilo?
Maneno mawili; Edinson Cavani. “Je usajili huo unaonesha maana ya matumizi sahihi ya bajeti? Man United watafanya mambo mengi kwa kipindi atakachokuwepo klabuni hapo? Kumleta kwenye kikosi chao inaonekana haina maana kabisa. Ni dili bovu.” Anasema wakala mmoja.
Baadhi ya mawakala wameita usajili wa Cavani ni wa papara, licha ya nyota huyo raia wa Uruguay kupata asilimia 28. Wakosoaji wanasema uamuzi wa kumsajili Cavani ni hasara. “Muda wa kumsajili, mawakala, umri, mshahara, kila kitu. Ni kama „tutawezaje kuuza jezi sehemu nyingine duniani?
Usajili mwinginde uliofanyika Old Trafford ni Donny van de Beek, ametajwa na mawakala kadhaa, ingawa maoni yao hayana cha
kufanya dhidi ya uwezo wake, na mikakati gani waliyonayo Man United kwenye usajili huo.
“Sielewi Van de Beek. Ni mchezaji mzuri lakini sio aina ya wale wanaohitajika Man United.
Kuna pauni milioni 35 za Wolves zimetumika kulipia katika usajili wa Fabio Silva, “kuwa mshambuliaji wa akiba” umetajwa na wakala mmoja, wakati maswali mengine ikiwa Arsenal watanufaika na fedha walizowekeza kwa usajili wa Thomas Partey.
Kwa ujumla, ingawa kuna hisia kwamba mlipuko wa ugonjwa wa corona umechangia klabu kuwa waangalifu kwenye ,matumizi ya makubwa ya fedha, ikiwa na maana mawakala hawakuwa na machaguo mengi kwenye suala la kuwapeleka au kuwauza wateja wao.
“Hakuna usajili mbaya sana,” anasema wakala mmoja. “Klabu za Ligi Kuu zimejaribu kuhakikisha zinanunua wachezaji wanaohitajika kwa bei nafuu na kujizuia kusajili kwa gharama kubwa. Ikawa sawa na kucheza kamari. Zimesajili wachezaji wenye viwango vya juu na kuwa na thamani ya kuuzwa pia. Lakini kama nikitaja jina, basin i Nelson Semedo.”
Nyota huyo kutoka Ureno amenunuliwa kwa pauni milioni 27.6 kuchukua nafasi ya Matt Doherty. Kiuhalisi, uamuzi wa Wolves kumuuza Doaherty kwenda Tottenham umeelezwa kuwa wa hovyo, ambapo mawakala wanasema hawaelewi kwanini klabu hiyo ilikubali kumuuza Doherty, na namna gani ataweza kuingia katika mfumo wa Spurs, ikikumbukwa nafasi ya anayomudu ni beki wa kushoto kuliko beki wa kulia.
Usajili wa Cavani sio pekee ulioitwa wa hovyo. “Totenham wamemchukua Carlos Vinicius kwa mkopo wa msimu mmoja. Mpango wao ulikuwa kumchukua Ollie Watkins na yeye alitaka kujiunga Spurs, lakini Daniel Levy hakuridhishwa na dau lililotakiwa kumsajili na masharti ya kucheza kikosi cha kwanza. Daima usajili wa dakika za mwisho unaziba mapengo, sio lazima kumpata mchezaji sahihi au klabu husika.” Anasema wakala mmoja.
3. Ni usajili upi umeshangaza zaidi?
“Chelsea wamenishangaza zaidi usajili wao. Hatujaona usajili sampuli ya Kai Havertz kipindi hiki. Ana miaka 21, ni mchezaji mzuri na walikuwa tayari kulipa gharama zozote. Wameonesha ubabe wao kwenye usajili, lakini wametengeneza presha kwa kocha wao Frank Lampard.
Usajili wa Partey umetajwa mara nyingi na mawakala, amepata asilimia 25, kwa sababu ya gharama za usajili na mshahara wake, ambapo wengi wamesema si kawaida ya Arsenal kulipa mshahara wa namna hiyo hasa baada ya kuhisi dili lingekufa.
“Kwa sababu wamefanikisha usajili. Partey hakuwa mchezaji wa bei nafuu, mshahara wake ni mkubwa mno, sikufikiria kabisa kama Arsenal wanaweza kukubali kumlipa. Hainingii akilini kwenye dili hili kwa jinsi Arsenal walivyo.
Akiwa amepata asilimia 19 ya kura, kurejea kwa Gareth Bale kwenda Spurs ni jambo kubwa. “Sio kwa sababu Totenham wamemsajili Bale, walichotoa ni halali. Lakini ukweli ni kwamba madili mengi ya usajili hayakuwa yanaenda vizuri, hivyo inabidi usajili kwa vile huna namna,”aanasema wakala mwingine.
Kama kuna usajili ambao umefikirisha wengi ni wa Fabio Silva kutoka Porto kwenda Wolves. “Huo ni usajili bora zaidi kufanywa na Jorge Mendes katika dirisha hili la usajili, kwani alipata malipo ya pauni milioni7 kufanikisha dili hilo,” anasema wakala mmoja.
Wakala mwingine anasema, “Suala sio usajili wenyewe, kwa sababu sote tunajua kuna mkono mrefu wa ushirikiano hapo. Lakini dau lenyewe. Linavutia mno,”
Jina la Rhian Brewster nalo limetajwa kwenye kipengere cha usajili mbovu. Ilidhaniwa Liverpool wangemtoa kwa mkopo, lakini ameuzwa kwa pauni milioni 23.5. “Kuna hasara kidogo kwenye masharti ya kuuzwa Brewster kwenda Sheffield United. Lakini hasara hiyo ipo kwa mchezaji mwenyewe pia kujiunga timu ambayo haijapata pointi tangu kuanza msimu huu,” anasema wakala mmoja.
4. Timu gani imefanya usajili bora?
“Everton. Lakini Aston Villa na Leeds United zimefanya biashara nzuri, na Totenham wamemaliza kwa uzuri zaidi.
Usajili wa Chelsea umeleta hisia tofauti na mawakala wamezitaja timu tano zenye usajili mzuri. Everton wamepata asilimia 33, Aston Villa wamepata asilimia 22. Timu zote mbili zimetajwa kuboresha vikosi vyao kimalengo kuliko zingine.
Villa wamenunua Ollie Watkins, Matty Cash, Emiliano Martinez, Bertrand Traore na Ross Barkley, inaonesha wamejifunza kutokana na kile kilichotokea msimu uliopita, ambapo walinusurika kushuka daraja.
Kwa upande wa Everton, wamesajili Allan,James Rodriguez, Abdoulaye Doucoure. “Everton na Spurs zinaonekana kuwa imara
zaidi, huenda wakaimarika zaidi kuliko walivyoanza msimu.” Anasema wakala mmoja
Bale, Sergio Reguilon, Vinicius na Pierre-Emile Hojbjerg ni nyota wapya waliotua Spurs. “Spurs wameziba mapengo mengi na wamenunua wachezaji wenye uzoefu na njaa ya mafanikio” anasema wakala mwingine
Chelsea imetumia fedha nyingi baada ya kutoka kwenye kifungo cha usajili. “Kwenye ulinzi, wanaonekana wana kasoro. Lakini kuboresha safu ya ushambuliaji wameleta nyota wapya, ambao wanachangia ugumu kwa wengine kupata namba kikosi cha kwanza,”
5. Ni klabu ipi imeboronga kwenye usajili?
Bila kupepesa macho Manchester United imetajwa kuwa klabu iliyoharibu zaidi kwenye dirisha usajili lililopita. Man United imepata asilimia 32, ikifuatiwa na Burnley yenye asilimia 28 na Fulham asilimia 20, kuwa klabu zilizoboronga kwenye usajili.
“Man United wamemkosa chaguo lao la kwanza. Jadon Sancho, ni hasara kubwa sana kwao. Man United sio kwa sababu ya nani amesajiliwa bali kwa sababu wachezaji waliowataka hawajawapata. Hilo ni jambo bay asana kwa namna fulani. Inaashiria kushindwa kwa kocha Ole Gunna Solskjaer. Klabu kubwa inatakiwa kutikisa soko la usajili,” wamesema mawakala mbalimbali.
Burnley haijasajili mchezaji yeyote, ikiwa na maana watarudi nyuma zaidi badala ya kusonga mbele,”
Si kwamba Burnley haijasajili yeyote, isipokuwa imewachukua wachezaji ambao wanaonekana hawana lolote, kwa mfano Dale
Stephens amenunuliwa kutoka Brighton na Will Norris amenunuliwa kutoka Wolves, lakini tathmini inaonesha dirisha la usajili lililopita kocha Sean Dyche, amefeli kuwasajili wachezaji aliowataka kama vile Harry Wilson kutoka Liverpool na imeonesha ni udhaifu wa timu hiyo kufanya biashara nzuri.
Fulham imesajili wachezaji kadhaa lakini macho ya mawakala yanasema nao wameboronga. West Ham wamemuuza Grady Diangana kwenda West Brom, lakini mipango yao ya kusajili beki wa kati imefeli. Majaribio yao yalikuwa kuwasajili kati ya Antonio Rudiger, Fikayo Tomori au James Tarkowski yaligonga mwamba.
6. Je, ugonjwa wa Corona umebadili soko la usajili?
Takwimu zinaweza kuonesha klabu zimetumia pauni bilioni moja na kuwa hali ileile katika soko la usajili na kwamba ugonjwa wa Corona haujabadili lolote.
“Chelsea wametumia bajeti kubwa na wametawala soko. Lakini corona imebadili masuala ya fedha kabisa kwa sababu klabu zilitegemea kutoka kwa wamiliki wao kusajili wachezaji. Idadi ya wachezaji waliosajiliwa kwa mkopo inaeleza hali halisi kuwa timu zimekosa fedha. Timu nyingi zimetumia mbinu ya pili au tatu kuimarisha vikosi9 vtao. Hakuna iliyokuwa tayari kuwekeza fedha nyingi kwenye manunuzi EPL, hali ambayo imezinufaisha timu kubwa,”
Mawakala wanasema “Mauzo ya wachezaji yamekuwa magumu. Timu zimehangaika kuuza hata wachezaji isiowataka kwa sababu suala la fedha lilikuwa gumu kwa klabu nyingi. Corona imebadili mbinu za kuingia mikataba. Mawakala hawakuwa na nguvu na klabu zilitumia ugonjwa huo kama kisingizio cha kukwepa kulipa dau kubwa.”
Baadhi ya mawakala wameonesha picha kubwa, kutoka juu EPL hadi chini, ambako ugonjwa wa corona umeathiri pakubwa soko la wachezaji.
“Mambo yamebadilika sana, hasa klabu za daraja la kwanza, ni balaa kubwa, na zinasua sua kwa sasa. Mara nyingi habari za top four au top six au EPL ndio zinabamba. Lakini timu zote zinazokuwa kundi hilo zina madeni makubwa, biashara mbovu nab ado zinatakiwa kufanya vizuri sokoni. Kwenye ligi za chini wanazingatia namna ya kusonga mbele kupitia hali walizonazo.
7. Ni usajili upi umefeli sasa na huenda ukatimia Januari?
“Kijana mmoja aliyeumizwa na usajili ni Max Aarons. Ameivutia klabu za Barcelona,lakin Norwich waligoma kufanya biashara kwa sababu ya dau dogo. Barcelona wakaamua kumsajili Sergino Dest, lakini kama Aarons atakuwa wiki nane au tisa nzuri, basi timu nyingine inaweza kubisha hodi mlangoni kwao januari.
Rudiger, anaweza kuondoka Chelsea ifikapo Januari, dili linaweza kubadilika ikiwa atacheza mechi nyingi kwa miezi miwili ijayo. Tarkowski anaweza kujiunga Leicester, na haitashangaza Jadon Sancho akijiunga Man United.
“Tetesi kuhusu Sancho zitarejea kwa kasi. Taarifa za ndani zinasema anataka uhamisho mkubwa. Sina uhakika kama Man United watafanikiwa kumsajili. Jadon Sancho kuhama Dortmund ni suala linalowezekana lakini huenda likatimia zaidi dirisha kubwa la usajili ujao. Ila huenda asjiunge Man United.
Fikayo Tomori na Billy Gilmour wanaweza kuhama Chelsea januari mwakani. Brandon Williams hataki kuwa beki wa kushoto chaguo la tatu Man United, kiakili amejiandaa kuhama lakini sio kujiunga timu kama Leeds au Southampton.
8. Usajili gani unaangaliwa kwa kiasi kikubwa kuleta matunda?
Hili lilikuwa swali gumu kwa mawakala kujibu. “Hakuna usajili uliowekwa kwenye matazamio. Lakini hakuna aliyetegemea Thomas Partey angeenda Arsenal, hilo linaweza kuwa kubwa kwao”
Ross Barkley umekuwa usajili maarufu Aston Villa akiwa na asilimia 16 ya kura. Baadhi ya mawakala wameeleza kuwa usajili huo wa mkopo wa msimu mmoja ni kurudi nyuma kwa sababu haukutegemewa kuvutia wengi.
“Zipo dalili usajili wake unaweza kuleta matunda, hasa baada ya kucheza nafasi ya kiungo huru. Ross anatakiwa kuthibitisha thamani yake.”
“EBerechi Eze pale Crystal Palace atashangaza watu, na Gabriel wa Arsenal atathibitisha kuwa na thamani iliyolipwa kwake” anasema wakala mwingine
Eze, pamoja na Timothy Castagna wa Leicester ni wachezaji pekee waliotajw amara mbili zaidi ya Barkley. Majina mengine ni mshambuliaji Raphinha aliyejiunga Leeds akitokea Rennes na Ryan Fraser aliyehamia Newcastle kutoka Bournemouth.
“Nafikiri Ryan Fraser kujiunga bure Newcastle ni usajili bomba. Iwapo atakuwa fiti, atakuwa miongoni mwa wachezaji bora 10. Klabu nyingi zilitaka kumsajili. Inaonekana alitaka kujiunga na timu za Top six lakini ndoto yake haijafanikiwa.”
9. kama ingewezekana kubatilisha usajili mmoja, ni upi ungezuia?
Kitu cha kwanza, hakuna anayefurahishwa na muundo wa sasa ulivyo.
“Iwe ndefu hadi machi au fupi ni muhimu kuwa na dirisha moja la usajili. Ukizingatia kile kiichotokea sasa wakati wa corona, kuna timu daraja la kwanza zinahitaji pauni 50,000 kulipia deni lakini zinakosa. Nafikiri ilibidi kufanya mabadiliko. Pengine sio mwezi
machi bali februari, hasa pale mchezaji anapoambiwa hayuko kwenye mipango ya kocha. Mchezaji hana nafasi na anaishia jukwaani, na hawezi kuhama hadi dirisha kubwa au dogo. Je kwanini huyo asiondoke mapema mfanbo Novemba kama sio sehemu ya mipango ya kocha?”
Baadhi ya mawakala wamedai kuwa dirisha la usajili ni kama biashara yenye vikwazo. Wengine wanaamini muundo wa sasa ni mrefu mno huku timu zikiwa hazijafanya usajili wa maana.
“watu wengi walichanganywa na siku ya kufungwa usajili Oktoba 5. Ni upuuzi huwezi kutoka EPL kwenda EFL sasa, wala kutoka EFL kwenda EPL.”
“soko sasa litatazama muundo wa usajili kwa jicho tofauti. Hatujui lini mambo yatakuwa sawa baada ya ugonjwa. Timu zinahitaji muda kutengamaa. Tatizo ni mfumo wa usajili unachangia presha kubwa.”
10. Ni kocha yupi atakuwa wa kwanza kupoteza kazi yake?
“Wapo wawili, lakini mmoja amefanikiwa kwenda mbali kwa sasa. Solskjaer anakabiliwa na presha kubvwa kwa sababu dirisha la usajili halikwenda vizuri kwa upande wake. Lampard yuko kwenye presha kubwa pale Chelsea. Kuna kijana mmoja hana kazi kwa sasa, na huenda akachukua ya moja. Ni Mauricio Pochettino.
Lampard na Ole Gunnar wame[ata asilimia 32 ya makocha ambao wanaweza kufukuzwa wakati wowote. mwingine ni Scott Parker wa Fulham amepata asilimia 40. Sean Dyche naye amepata asilimia 12. Wengine ni Slaven Bilic, Chris Wilder na Graham Potter.
11. nani atanyakua taji la EPL?
“Wiki iliyopita ilikuwa na maajabu, lakini bado naamini Liverpool watachukua ubingwa. Wanafahamu namna ya kurekebisha mambo, wana wachezaji mahiri, kocha mwenye uwezo wa kupindua matokeo Juregn Klopp. Manchester City, Man United, Chelsea zina matatizo yao, lakini Everton haiwezi kushindana na Liverpool” wamesema mawakala hao.
Mawakala wengi wameonesha kushangazwa na ki[pigo cha mabao 7-2 ilicho[pata Liverpool kutoka kwaAston Villa. Lakini Liverpool wamepata asilimia 68 ya timu yenye uwezo wa kunyakua ubingwa.
12. Timu zipi zitamaliza nafasi nne za juu?
Kuna timu 7 zinazopigania kumaliza nafasi nne za juu. Everton imepata asilimia 16 na inatajwa kuwa na maendeleo mazuri na huenda ikaonesha maajabu.
Manchester City na Liverpool zinaongoza. Chelsea (72%), Spurs (67%). Manchester United, wamepata asilimia ndogo kuliko Everton.
13. Nani atashuka daraja?
Fulham, West Bwom,Leeds United, Burnley, Sheffield United, Brighton ni miongoni mwa timu zinazotajwa hunda zikashuka daraja msimu huu na kwedna kushiriki EFL.
14. Je, mawakala wanalipwa fedha nyingi kuliko kazi halis?
“Namna tunavyolipwa fedha zetu imepotoshwa kwenye vyombo vya habari. Mashabiki hawaelewi nini tunachofanya. Tunafanya kazi ya kuwasaidia wachezaji na kusapoti familia zao. Tunafanya kila kitu kwaajili yao, sio suala la kuingia mkataba tu. Tupo kwaajili ya wachezaji kusaidia namna ya kuingia mikataba, nasi tunalipwa. Mengi yanayosemwa ni kupotosha msingi wa wachezaji kuwa na wakala wake. Wachezaji wanahitaji wakala. Ingawa tunakubali kuwa wapo mawakala wabaya wanaharibu kazi zetu,” wameeleza baadhi ya mawakala.
“Kama unafikiria kiasi cha fedha anacholipwa Mino Raiola, inabidi usahau. Watu wanapoongelea gharama za nyumba England, hawazungumzia asilimia 0.01 ya nyumba kama Mayfair ambazo zinauzwa pauni milioni 20. Wanaongelea nyumba za bei nafuu, na kuna kazi wakala anakuwa ameifanya kuhakikisha mchezaji wake anafanikisha kila kitu bila mizengwe.
15. Je, ni sahihi mawakala kulipwa na pande nyingi?
Gary Lineker aliandika Twitter akishauri ni wakati wa FIFA kuwazuia mawakala kulipwa fedha na pande nyingi kwenye dili la usajili. Nyota huyo wa zamani wa England anasema mawakala wanapaswa kulipwa na wachezaji wao ambao ndio wateja husika kwenye dili.
“Kuna matatizo mengi. Kama una timu ya daraja la kwanza inamtaka mchezaji wako ambaye hataki kulipwa mshahara chini ya pauni 2500, lakini unatumia wiki kadhaa kumshawishi
mchezaji kuwa ni fursa sahihi, hiyo ni kazi ngumu sana, kisha unatakiwa kuzungumza na uongozi wa timu pamoja na pande zingine. Kuna wakati wakala analipwa kwa niaba ya klabu na mchezaji, haina maana kuwa anapokea fedha hizo kama za kwake, bali wapo wahusika wanaotakiwa kupewa.”
“Uwakilishi pacha umefutwa na FA, ukaidhinishwa na HMRC na inawanufaisha wachezaji kwa kiai fulani kuhusu masuala ya kodi. Inaokoa fedha za klabu pia.
Comments
Loading…