in , , ,

MALINZI AZINDUA KAMPENI YA ISHI HURU

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
amezindua programu ya kutoa elimu ya kupambana na matumizi ya dawa za
kulevya kwa vijana iitwayo Ishi Huru.

Programu hiyo iliyozimduliwa jana (Januari 10 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam iko chini ya taasisi ya Africa Inside Out inayoongozwa na Rebecca
Young wakati washirika (partners) ni TFF na kampuni ya Rhino Resources ya
Marekani.

Rais Malinzi amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini yamekuwa
yakiongezeka, hivyo kuwa kikwazo kwa maendeleo ya vijana ambapo
ameipongeza Africa Inside Out kwa programu hiyo kwa vile itazuia vijana
wengi kujiingiza katika matumizi ya dawa hizo.

“Moja athari kubwa za matumizi ya dawa za kulevya ni kupata maambukizi ya
virusi vya Ukimwi kutokana na kuchangia sindano za kujidunga dawa hizo.

“TFF tutatoa ushirikiano wa kutosha katika programu hii. Lakini pia
tutaingiza Ishi Huru katika programu zetu za mpira wa miguu kwa vijana.
Tutahamasisha jamii katika kupambana na dawa za kulevya,” amesema.

Katika uzinduzi huo, pia Rais Malinzi alizundua semina ya waelimishaji na
kuwaeleza kuwa wamepata fursa hiyo kwa vile ni vijana wanaojituma, hivyo
watafikisha vizuri ujumbe wa Ishi Huru katika shule na vituo vya vijana
nchini.

CAPTION: Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal
Malinzi akizungumza kwenye uzinduzi wa programu ya Ishi Huru jijini Dar es
Salaam.

RAMBIRAMBI MSIBA WA MTANGAZAJI SULTAN SIKILO
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo
cha mtangazaji wa michezo wa Radio Abood, Sultan Sikilo kilichotokea jana
alfajiri (Januari 11 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

Sikilo ambaye pia aliwahi kufanyia kazi Radio Times na Radio Kheri na hadi
umauti unamkuta alikuwa Mweka Hazina Msaidizi wa Chama cha Waandishi wa
habari za Michezo Tanzania (TASWA) amezikwa jana jioni katika makaburi ya
Kibada, Kigamboni.

Msiba huo ni mkubwa katika sekta ya habari na mpira wa miguu kwani kwa
nyakati tofauti Sikilo alifanya kazi na TFF kwa kuripoti shughuli zetu
nyingi za mpira wa miguu, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.

TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Sikilo, Radio Abood na TASWA na
kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba
huo mzito. Pia TFF imetoa ubani wa sh. 100,000 kwa familia ya marehemu
kama rambirambi zake.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Chelsea, Man U watesa EPL

Ronaldo bora duniani kote